Msukuma na Parachuti

Zero IQ

JF-Expert Member
Dec 21, 2016
13,917
24,674
Kulikuwa na Ndege ilikuwa inaanza safari ilivyokuwa Angani mara ghafra ikapata hitilafu,
Ndipo rubani akatoa taarifa kwamba ndege imepata hitilafu na itadondoka baada ya dakika 10.

Ndani ya ndege kulikuwa na watu watano Lakini maparachuti yalikuwa manne tu, Watu hao ni mchungaji, waziri, mwanajeshi, msukuma na mwanafunzi wa chekechea, Mchungaji akasema yeye anategemewa na kanisa hivyo hapaswi kufa.

Akachukua parachuti akaruka, Waziri akasema wananchi wanamtegemea alete maendeleo, Akachukua parachuti akaruka, Msukuma akasema familia inamtegemea akachukua parachuti akaruka faster.


Wakabaki mwanajeshi na mwanafunzi wa chekechea,
Yule mjeshi akamtazama mwanafunzi akamuonea huruma kisha akasema. Mimi najitolea kufa kwa ajili yako,
we chukua hilo parachuti lililobaki ujiokoe halafu mi nitakufa na hii ndege.

Yule mwanafunzi akajibu "usijali yamebaki maparachuti mawili"
yule mjeshi akashangaa akauliza mawili kivipi.?
Mwanafunzi akasema YULE MSUKUMA KACHUKUA BEGI LANGU LA SHULE ALIDHANI NI PARACHUTI.



_Jf Matawangu
 
Back
Top Bottom