PreGE2025 Msukuma: Kuna fukuto la kumuondoa Tundu Lissu CHADEMA

PreGE2025 Msukuma: Kuna fukuto la kumuondoa Tundu Lissu CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Wont be the same

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,564
Reaction score
2,483
Mbunge wa Geita Vijijini, Mhe. Joseph Musukuma, amesema kuwa kampeni ya No Reforms No Election inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) haina nafasi ya kufanikiwa kwa sababu haina uwezo wa kuzuia uchaguzi mkuu. Aidha, amedai kuwa kuna mipango inayoendelea ndani ya chama hicho ya kutaka kumwondoa Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Akizungumza na waandishi wa habari katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, Musukuma amesema kuwa siasa siyo kususia uchaguzi bali ni kushiriki kwa ushindani, na madai ya kususia uchaguzi yanatokana na hofu ya kushindwa.

"Bila wao, sioni kama kuna raha. Watu wanasubiri tu hiyo kauli ya No Reform No Election, lakini ndani ya CHADEMA kuna jambo kubwa zaidi ya 'No Election'. Tuendelee kuwa hapa tu, natamani mwezi ujao tuone yatakavyokuwa. Hii G-55 si watu wajinga; kama ni chama chenye demokrasia, Mwenyekiti alipaswa kusitisha ziara na kuwasikiliza wanachama wake, si kuwaita wajinga,

Unatangaza kuzuia uchaguzi bila kueleza mbinu. Kama kuna Rais ambaye amewapa uhuru mkubwa wana-CHADEMA, ni Rais Samia Suluhu Hassan. Nimekuwepo wakati wa Kikwete na Magufuli, hawakuwa na uhuru huu. Sasa mnapopewa uhuru, mnaanza kuweka masharti. Sisi tayari tumejiandaa kwa uchaguzi." Amesema Musukuma.
Maoni ya dawa
Amani ipi watu wanatekwa hakuna hatua zinachukuliwa, vijana hawana ajira maisha magumu tozo utitiri na matumizi mabaya ya fedha za umma lakini no actions taken
Haya mambo ya kila kitu ni hisani za Raisi inabidi yakomweshwe! Tunataka katiba mpya.
 
Kumuondoa kivipi? Kumvua uenyekiti au kumuua? Maaja hawa CCM wakishindwa hoja wanakimbilia bunduki. Huyo samia kwamba ndio ataishi milele? Unaweza fanya ubaya wote ila vyeo havidumu, Lissu alimwagiwa risasi ngapi ila aliyekua Rais tena mzima wa afya alimtangulia.

Afrika haitawahi kupata maendeleo sababu ya mindset za namna hii.
 
Hapo hata mm nimejiuliza
 
watakao jaribu na kutamani kumuondoa Lisu kwa namna moja ama jingine wataondoka wao kwa vyovyote vile
 
Kwa mtu mwenyeakili anaweza angalau kujua upande hupi unamsimamo gani juu ya LISSU.
 
Mbunge wa Geita Vijijini Josephat Msukuma ameibuka na kuzungumza juu ya sakata la No Reform , No Election kampeni ambayo imeonekana kushika kwa kasi hivi sasa

Msukuma amesema kampeni hio inalengo la kuvuruga amani kwenye nchi na uchaguzi unakaribia kufanya miezi michache ijayo.
View attachment 3299773
Mtu mwenye Elimu ya memkwa ni ngumu sana kuelewa. Serikali iboreshe Mtaala yao zaidi jamani. Msukuma.
 
Haya mambo ya kila kitu ni hisani za Raisi inabidi yakomweshwe! Tunataka katiba mpya.
 
Back
Top Bottom