Msongo wa mawazo (stress)

Manyanza

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
10,076
15,883
Msongo wa Mawazo (Stress) Ni hali ya shinikizo la kiakili au kihisia linalotokana na mahitaji yanayofikiriwa.
Kila siku tunakabiliwa na hali nyingi ngumu ambazo unaweza kuona kama “vitisho” kwa mfano majukumu ya kitaaluma, kikazi na kifamilia.

Aina za Msongo wa Mawazo
1. Msongo Mkali ( Acute Stress)
Husababishwa na shinikizo na mahitaji ya kila siku ambayo sisi sote tunapitia. Msongo huu hudumu kwa muda mfupi.

2. Msongo wa vipindi ( Episodic Acute Stress)
Msongo huu huanza au kukoma katika vipindi, mara nyingi hutokana na mahitaji na malengo yasiyo halisi.

3. Msongo wa Muda Mrefu ( Chronic Stress)
Ni mvutano wa muda mrefu kutokana na matatizo ya ndani au nje na kusababisha matatizo ya afya na mfumo wa kinga dhaifu. Haya ni mafadhaiko kama vile majukumu mazito ya malezi, ndoa au kazi.

MAENEO MTAMBUKA YANAYOWEZA KUSABABISHA MSONGO WA MAWAZO (Stressors)
Ni kama vile Shule ( taaluma), Kazi, Familia, Mahusiano, Fedha, Afya na Hali ya maisha.

UTAJUAJE KAMA UNA MSONGO WA MAWAZO
1. Ishara za kimwili;
Maumivu ya kichwa mara kwa mara, Ugumu wa kulala, maumivu ya kifua, Mapigo ya moyo kwenda haraka, Maumivu ya Misuli,Kichefuchefu, Maumivu ya tumbo, Kuhara au kuvimbiwa, Uchovu wa mwili, kupoteza hamu ya kujiamini, kuhisi baridi mara kwa mara.

2. Ishara za utambuzi ;
Ugumu wa kuzingatia, Matatizo ya kumbukumbu, uamuzi mbaya, wasiwasi, kuchanganyikiwa na kupoteza hisia za ucheshi.

3. Mabadiliko ya Kitabia ;
Kula zaidi au kidogo kuliko kawaida, kulala sana, Kutumia pombe, Sigara au dawa za kulevya.

NINI KINACHOSABABISHA MSONGO WA MAWAZO
1. Migogoro
2. Kumpoteza mpendwa wako
3. Changamoto za kifedha na
kiuchumi
4. Changamoto za Kitaaluma
5. Changamoto za Kiafya
6. Vitendo vya Unyanyasaji na Ukatili kama vile ukatili wa kimwili, kihisia na kingono.

MSONGO WA MAWAZO UNAWEZA KUSABABISHA HALI ZIFUATAZO;
1. Ugonjwa wa kisukari ( Diabetes)
2. Magonjwa ya Moyo( Heart disease)
3. Kutokuhimili tendo la ngono/ndoa ( Sexual dis function)
4. Vidonda vya tumbo ( Ulcers)
5. Sonona ( Depression)
6. Wasiwasi ( Anxiety)
7. Magonjwa ya ngozi ( skin problem)
8. Matatizo ya hedhi kwa wanawake

MIKAKATI 5 YA KUKABILIANA NA MSONGO WA MAWAZO
Mfadhaiko ni sehemu ya maisha na wakati mwingine hatuwezi kubadilisha hali, lakini tunaweza kujufunza kutambua kile kinachotusababishia hali hii na kukabiliana na athari zake.

Tafuta njia mpya za kukabiliana na hali hiyo ili usitegemee mbinu zisizo za lazima kama vile kunywa pombe, kula kupita kiasi na kuvuta sigara.

1. Tambua Vichochezi;
Tengeneza orodha ya vyanzo vyote vya Msongo wa Mawazo katika Maisha yako.

2. Zingatia Mtindo wa Maisha;
Hakikisha unakula Lishe bora (Eat right), fanya Mazoezi mara kwa mara (ili kuondoa homoni za mafadhaiko kupita kiasi na kukusaidia kulala vizuri na kupata usingizi wa kutosha)

3. Tengeneza Ratiba yenye Uwiano;
Tenga wakati wa shughuli / kujumuika na watu wanaokuletea furaha na raha, jifunze kukataa madai ambayo yanaleta Msongo zaidi katika maisha yako.

4. Jenga Mazoezi ya kila siku ya Kujistarehesha .kama vile Kupumua kwa kina (deep breathing), Utulivu wa misuli, yoga au kutembea. Hata kwa dakika chache kwa siku zinaweza kusaidia kupunguza tatizo hili.

5. Badilisha Matarajio kuhusu Mafadhaiko ambayo hayawezi kubadilishwa; Jizoeze Kushukuru na urekebishe jinsi unavyolichukulia tatizo, rekebisha vigezo vyako ikiwa wewe ni mpenda ukamilifu.

Copied and Pasted
 
Elon Musk ni muhanga kwenye hili,.
Anashukuru dawa za Depression zinamsaidia saidia
 
Yah! Binafsi napenda sana ukamilifu
na ili Hali nakua kabisa sijakamilika
Kwenye baazi ya vitu muhimu
 
Back
Top Bottom