Msomi usikate tamaa – badilika, usibadilishwe

Msomi usikate tamaa – badilika, usibadilishwe

Prof_Adventure_guide

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2023
Posts
519
Reaction score
1,463
Wasomi wengi wameishia kuwa na huzuni ya ndani, hali ya kisaikolojia inayoitwa existential frustration, kwa sababu waliaminishwa kuwa vyeti ni tiketi ya maisha bora. Ukweli ni tofauti – dunia ya sasa haiangalii tu cheti, bali uwezo wako wa kutatua matatizo na kuleta thamani.

Elimu uliyonayo ni msingi, siyo mwisho. Usiogope kuingia kwenye biashara au kazi ambayo haiko kwenye taaluma yako. Tumia ujuzi wako kwenye mazingira halisi. Kama umesoma uhasibu lakini huwezi kuajiriwa, unaweza kufundisha wengine au kuwasaidia wafanyabiashara wa mtaani kupanga mahesabu yao.

Acha kuwa mtu wa kulalamika. Dunia haitaki masikini wa fikra. Tumia muda wako kujifunza vitu vipya kupitia mtandao kama digital skills, freelancing, content creation, au hata kilimo cha kisasa.

Kataa maisha ya kusubiri serikali. Fanya kazi yoyote halali – hata kuuza vitumbua ni hatua sahihi kuliko kusubiri bila mwelekeo. Kazi ni kazi kama inaleta kipato. Usidharau mwanzo mdogo.

Jizungushe na watu wenye fikra chanya. Tafuta kundi la vijana wanaotafuta suluhisho, siyo lawama. Na zaidi ya yote, linda afya yako ya akili. Kukosa ajira si mwisho wa dunia – ni wito wa kujitambua, kubadilika na kuchukua hatua.
 
Hakika, waswahili wanasema mtoka bure si sawa na mkaa bure, huenda akaokota! Unaweza kuokota mawazo, au technohow au connections. Pili, kamwe usione aibu kujieleza, share ideas and your experiences ila sio UCHAWA na ujuaji. Kisha jitahidi sana uwe na limited speech, changia unapoona unajua unachochangia na sio kudakia kila kitu. Asubuhi Njema
 
Umeongea kitu kikubwa sana mkuu,
Tena mi naona graduates wakiingia mtaani kufanya shughuli yoyote ya kiuchumi wanatoboa fasta maana wanaifanya kwa uelewa uliotanuka zaidi.
 
Hakika, waswahili wanasema mtoka bure si sawa na mkaa bure, huenda akaokota! Unaweza kuokota mawazo, au technohow au connections. Pili, kamwe usione aibu kujieleza, share ideas and your experiences ila sio UCHAWA na ujuaji. Kisha jitahidi sana uwe na limited speech, changia unapoona unajua unachochangia na sio kudakia kila kitu. Asubuhi Njema
Shukrani
 
Back
Top Bottom