Msokotano mpya wazuka Zanzibar

KAMA WALIWEZA KULAZIMISHA UCHAGUZI WA MARUDI KINYUME CHA SHERIA WATASHINDWA KUBADILISHA HIYO KATIBA YENU? HIVI MNAWAJUA CCM AU MNAWASIKIA? WATABADILISHA LABDA MUNGU AINGILIE KATI LA SIVYO MTAJUA KIBURI CHA CCM NA JINSI WANAVYO JIVUNIA DOLA KUVUNJA KATIBA
 
Ngoja niipitie katiba kwanza ndio nichangie..nisije jikuta naingia kwenye ushabiki bila fact. 🙁
 
Ni kweli unavyosema, lakini kubadilisha katiba ni lazima ipigwe kura ya maoni Zanzibar, na kwa maana hiyo, uchaguzi mwengine ni lazima, kubadilisha katiba ama kuendelea na katiba! Kuendelea kutawala bila ya SUK ni kinyume cha sheria na kumchaguwa Makamo kutoka kwa wagombea ambao hawajatimiza ikadi nayo ni kuvunja sheria. Uchaguzi mpya unahitajika mpaka ikadi ipatikane. Venginevyo, CCM wanakula kiti moto mwezi wa Ramadhani mchana na hio wameona haitoshi, wameagiza kreti za bia. Haramu juu ya haramu. They put too much attention on cents while loosing shillings at the other end!
 
Natamani Hilo litokee,ila bahati mbaya naamini halitafanyila hata ikiwa katiba inekuwa moja tu dunia nzima
 
CUF waliposusia halafu ccm ikasomba mpaka watoto wakapige kura ili wapate ushindi wa kishindo, waliwaona CUF hamnazo sana
Kwa jinsi walivyo walafi wa madaraka watapiga kimya wao bora watu wafe lakin sio upinzan uongoze nchi!! Yanamwisho lakin..
 
Mimi difikirii kama wamekosea hesabu, matokeo haya yamepangwa yawe hivyo kwa malengo maalum ili kuacha nafasi ya majadiliano kwa Mara nyingine tens kati ya CUF na CCM.
Kura za ADC na CUF hazitofautiani sana, sasa kati ya Maalim na Hamad nani ni mtaji kwa CCM kusaidia utulivu wa Zanzibar? Hamad angepata kura zaidi ya 10% inamaana angekua makamu wa kwanza moja kwa moja, lakini Je, hali ingekua shwari Zanzibar? Unafikiri kweli wameshindwa kupika matokeo ya kumpa Hamad ushindi?
 
Hao wahafidhina wa CCM hivi sasa hawafuati tena katiba ya nchi, wanachojua wao ni ubabe na utemi, wakiamini kuwa vyombo vya dola 'wanavyovimiliki ' ndivyo vitakavyoendelea kuwawekea kinga na kuwalinda katika utawala wao wa kidhalimu.
 
Aamin...
 
udini na ukamilifu kwenye maisha manao nyinyi tuu ndio wasemaji na waonaji kwenye maisha ya siasa ya nchii hii? mshayasema mangapi na kulaani mangapi yamefanikiwa na yaloendelea!
kazi mlobaki kuendekea na fitina za kisiasa na kujifanya nyinyi ni wakamilifu hivi huo wema wenu na ubora wenu mnatusaidia nn ss wanyonge sii kutia fitina za kidini na kuapizaa tuu na kuwaona watu wote hawako sawa ila nyinyi na wazungu.
haya nasubiri uwo ukamilifu wenu wa kususa na kuanza kuapiza nione kama utapangua mchezo wa kihindi kuendeleaa
 
Kuna mchangiaji mmoja humu alisema CCM hawajui mahesabu vizuri lazima watakosea tu ktk kujumlisha matokeo, Na imekuwa hivyo
 
Umevurugwa wewe sio bure toka post ya kwanza mpaka ya kabla ya post hayo unayoongelea hayajaandikwa wewe umeyatoa wapi?
 
Wazanzibar mnatuzingua bhanaa imekuwa kila siku uchaguzi tu hamna shughuli zingine za maendeleo mkazifanya ???? Huo ugunyu sasa bhanaa
 
sahihi mana wao hawana maisha baada ya kila mda ni ushindani wa kisiasaa
 
Hapo ndipo tofauti ya kutumia akili inapokuja.
Ustaadh Jecha alikuwa na muda wa kutosha kupitia katiba na kujipanga vyema katika kile alichotaka kufanya.
Ila kwa sababu ni rahisi tu kupindisha mambo, hata hili nalo litapindishwa.
 
Hawa watu hawana mshipa wa haya ,watajifanya hawakumbuk katiba inasemaje,wanachojua wao ni kuingia ikulu tu kwa gharama yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…