Msiwaonee wababa...

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,770
59,118
Juzi kuna mtu (mwanamke) alikua analalamika jinsi mume wake alivyosababisha mpaka akabadilika na kua tofauti kabisa na alivyokua mwanzo....wapo waliounga mkono...waliotoa pole pia kushauri.Tatizo ni kwamba ile mada ilikua inatetea wanawake na kuponda wanaume.Sasa je wanaume wao ndo hawakutwi na situation kama hizo!?!Wangapi wanakua walevi baada ya muda ndani ya ndoa?! Wangapi wanakua na hasira za haraka ambazo hazikuwako mwanzo?! Wangapi wanakimbia nyumba zao walizozipenda mwanzo!!?!Mwangapi wanakua wachachu (bitter) tofauti na kabla ya ndoa??!!Na nyie wadada/wamama hua mnawafanya nini mpaka wababa/kaka zetu wanabadilika na kua hivi?!Na inapotokea hua mnafanya jitihada gani kuwasaidia warudie hali zao za kawaida kabla ya kuanza kulalamika fulana kawa mlevi mara sijui mkorofi?!Samahanini kwa maswali mengi ila jamani kuweni waungwana kwa wenzi wenu.Kama hutaki abadilike katika hali ambayo ni chanya kuelekea hasi jitahidi usiwe kisababishi cha yeye kua hivi!!Na ikitokea kua responsible na tafuta suluhisho badala ya kulalamika!!!
 
dogo lizzy ktk mahusiano kila pande hudhurika, na stail ya madhara ni ile ile either iwe upande wa wanababa au ule wa wanamama, umetaja baadhi ya mambo hapo juu ambayo kimsingi ndio maudhi yaliyopo ktk mahusiano. Kinamama wapunguze kuchonga kwani hata wao huwaumiza kina baba bia kwa namna 1 ama nyingine!
 
Juzi kuna mtu (mwanamke) alikua analalamika jinsi mume wake alivyosababisha mpaka akabadilika na kua tofauti kabisa na alivyokua mwanzo....wapo waliounga mkono...waliotoa pole pia kushauri.Tatizo ni kwamba ile mada ilikua inatetea wanawake na kuponda wanaume.Sasa je wanaume wao ndo hawakutwi na situation kama hizo!?!Wangapi wanakua walevi baada ya muda ndani ya ndoa?! Wangapi wanakua na hasira za haraka ambazo hazikuwako mwanzo?! Wangapi wanakimbia nyumba zao walizozipenda mwanzo!!?!Mwangapi wanakua wachachu (bitter) tofauti na kabla ya ndoa??!!Na nyie wadada/wamama hua mnawafanya nini mpaka wababa/kaka zetu wanabadilika na kua hivi?!Na inapotokea hua mnafanya jitihada gani kuwasaidia warudie hali zao za kawaida kabla ya kuanza kulalamika fulana kawa mlevi mara sijui mkorofi?!Samahanini kwa maswali mengi ila jamani kuweni waungwana kwa wenzi wenu.Kama hutaki abadilike katika hali ambayo ni chanya kuelekea hasi jitahidi usiwe kisababishi cha yeye kua hivi!!Na ikitokea kua responsible na tafuta suluhisho badala ya kulalamika!!!

...Lizzy wafaa kuwa defence lawyer wangu. Ahsante kwa kuwaambia ukweli hao!
Wamejiharibia wenyewe maisha!

"Nobody screws your life unless you give him/her the screw driver!"-
MwanajamiiOne, June 2011.
 
Haka kajukuu siku nyingine huwa kanamwaga mapwenti...khaa!

"Nobody
unscrews your life unless you give him/her the screw driver!"- MwanajamiiOne, June 2011; Edited by babu ODM Asprin June 28th 2011
 
take screw driver n do the nidful on me pls...!!!!!!!!!!
 
Hii inatokea kwa pande zote mbili Lizzy, kila mmoja ana wajibu wa kuwajibika kwa mwenzake kutunza lile agano waliloweka pamoja,kama upande mmoja ukifanya kazi peke yake lazima kuna ambaye ataumia .

Naweza kukuambia mambo si marahisi hivo,iwe kwa wanaume/wanawake tunapigania hasa iwe kwa maombi,ushauri na mambo mengi ili mradi tu kuifanya nyumba yako isimame na inapofika sehemu unaona imeshindikana huwa tunatafuta njia mbadala kuliko kujifia na pressure.

Lizzy tunahitaji kuwajibika ipasavo kwa wale tuwapendao sio kuweka lawama zetu mbele bila kuangalia wao wanahitaji nini kutoka kwetu.
 
Lizzy asante kwa kuwakilisha,

ila haya mambo magumu bana, sometimes mwanamke akiwa poa mwanaume hovyo, na vile vile inaweza kutokea mwanaume akawa poa mwanamke hovyo kabisa so inategemea. Kila mtu analaumu kwa upande wake, mwanamke aliotendwa atalaumu vivyo hivyo mwanaume akitendwa analalamika.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom