Msiwalaumu sana viongozi, wanatetea ugali wao

Msiwalaumu sana viongozi, wanatetea ugali wao

HUSSEN KAMBI

Senior Member
Joined
Dec 4, 2023
Posts
196
Reaction score
250
Msiwalaumu sana kwani wanatetea ugali wao hakuna kitu muhimu kama kula ndio maana tunaona viongozi wengi kabla ya kuzungumza mada husika kwanza anachukua muda mwingi kusifia sijui anaupiga mwingi sijui nani kama yeye sijui kafungua nchi sijui katoa bilioni kadhaa yani kama anatakiwa azungumze masaa mawili basi lisaa limoja na nusu anasifia tuuu dakika thelathini ndio anaingia kwenye hoja

Tatizo kula na mamlaka matamu hata wenyewe wanatambua wanapokuwa majukwaani wanajua kabisa hili naongopa ila kwa ajili ya kutetea ugali wangu ngoja nimsifie kwanza alionipa cheo hiki ili aendelee kuniweka hapa ili niendelee kula

Kwa hiyo tusiwalaumu sana wanatetea matumbo yao ndio maana muda wote wanaongea pumba wanapokuwa majukwaani.
 
Kuna wengine wakiwa majukwaani huwa hawaongei Pumba Mkuu ila wanaongea Takataka kabisa (Rubbish).

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Back
Top Bottom