Elections 2010 Msiwachague wasiojali umaskini wa wananchi

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Msiwachague wasiojali umaskini wa wananchi

Na Godfrey Mushi


18th October 2010




p { margin-bottom: 0.08in; }
Makamu wa Askofu Mkuu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG), Magnus Mhiche, amewataka Watanzania kufanya maamuzi magumu Oktoba 31, mwaka huu, kwa kutowachagua viongozi ambao hawajali umaskini wa Watanzania.
Askofu huyo amewahimiza Watanzania kutokubali kurubuniwa na kuwachagua viongozi wenye uchu wa kujilimbikizia mali na ambao hawatambui mzigo mzito walioubeba wananchi kutokana na umasikini.
Askofu Mhiche alikuwa akizungumza katika mahafali ya kwanza ya kidato cha nne cha Shule ya Seminari ya Wavulana ya Ebenezer iliyopo Kijiji cha Nduli, nje kidogo ya mji wa Iringa.
Alisema dawa ya kuwakataa viongozi wasiotambua mzigo wa umasikini walionao watanzania, viongozi wanaoeneza maneno ya uchochezi na kuhatarisha amani ya nchini ni kujitokeza kwa wingi siku ya upigaji kura na kuonyesha maamuzi yao kwa kutowachagua.
“Msibakie tu kulalamikia matatizo yenu, tujitokeze kwa wingi siku ya upigaji kura, tukaonyeshe maamuzi yetu kwa kutowachagua viongozi wanaoeneza maneno ya uchochezi kwa kuwa ni hatari kwa amani ya nchi,” alisema na kuongeza:
“Wapo wengine wenye uchu wa kujilimbikizia mali na kusahau umasikini tulionao…tuwachague watu watakaotupeleka mahali pazuri. Wanaonuka kwa rushwa wasipewe nafasi.”
Alisema viongozi wanaopaswa kuchaguliwa ni wale wanaotambua umasikini wa wananchi wao na kujitoa kwa moyo katika kutatua kero zinazowakabili na si kukimbilia madaraka kwa lengo la kujilimbikizia mali zinazotokana na rasilimali za Watanzania.



CHANZO: NIPASHE
 
Back
Top Bottom