Msitumie ubaguzi wa rangi kutuaminisha mchina ndiye chanzo cha Dar kukosa maji

Hismastersvoice

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
18,670
22,261
Zimejitokeza shutuma nzito dhidi ya raia wa China akikomba maji mto Ruvu na kutupigia hesabu ya lita elfu elfu! Huyo mkulima ambaye ni mmoja wapo wa wakulima na wafugaji wanaokomba maji mto Ruvu.

Tatizo lililopo si hawa watumiaji bali ni serikali kutokuwa na mpango wa maana unaoonesha uwezo wa wahusika kielimu.

Mimi binafsi sina elimu ya maji lakini nimekuwa mara nyingi nikiandika kuwa bila bwawa tatizo la maji halitaisha. Hayo maji yasingetumiwa na huyo mchina* ni wazi yangeishia baharini, lskini tatizo la maji Dar lipo tangu miaka ya sitini na miaka ya sabini tulishuhudia tukiletewa tope na visingizio kibao!
 
Morogoro inapata maji toka bwawa la Mindu huku Dar inapata maji toka mtoni! Haiingii akilini.
 
Wanahangaika Sana kuhalalisha mgao,eti mchina Mara wafugaji.
Kwani tumeanza Leo kufuga ng'ombe?.
Wapigaji mtazila hizo pesa ila na nyie jasho la pua litawatoka.
 
Mara nyingi watumishi wa uma (serikali na taasisi zake) hufanya kazi bila kutumia akili za kawaida.
Kwenye chanzo cha maji ya matumizi mijini kama ruvu lazima mto ukingwe kuwe na mlango wa kudhibiti mtiririko wa maji hadi tone la mwisho.
 
Hayo maji yanayaopotea hovyo baharini kama serikali ya ccm Ingekuwa ipo seriously isingekuwa inakimbizana na machinga au bodaboda
 
Zimejitokeza shutuma nzito dhidi ya raia wa China akikomba mani mto Ruvu na kutupigia hesabu ya lita elfu elfu.

Huyo mkulima ambaye ni mmoja wapo wa wakulima na wafugaji wanaokomba maji mto Ruvu. Tatizo lililopo si hawa watumiaji bali ni serikali kutokuwa na mpango wa maana unaoonesha uwezo wa wahusika kielimu.

Mimi binafsi sina elimu ya maji lakini nimekuwa mara nyingi nikiandika kuwa bila bwawa tatizo la maji halitaisha.

Hayo maji yasingetumiwa na huyo mchina* ni wazi yangeishia baharini, lskini tatizo la maji Dar lipo tangu miaka ya sitini na miaka ya sabini tulishuhudia tukiletewa tope na visingizio kibao.

Zinatafutwa sababu za kuhalalisha. Hizo sababu huitwa visingizio.

Hata Tiganga kama Siyani na Luvanda anafanywa hivyo hivyo.

Wanaita the end justifies the means.
 
Haya ndio madhara ya kuwa "Reactive" badala ya "Proactive". Yaani kusubiri janga litokee ndo unakurupuka, badala ya kuwa na mikakati ya muda mrefu kuhusiana na jambo husika likiwemo hili la maji.
 
Zimejitokeza shutuma nzito dhidi ya raia wa China akikomba mani mto Ruvu na kutupigia hesabu ya lita elfu elfu! Huyo mkulima ambaye ni mmoja wapo wa wakulima na wafugaji wanaokomba maji mto Ruvu.

Tatizo lililopo si hawa watumiaji bali ni serikali kutokuwa na mpango wa maana unaoonesha uwezo wa wahusika kielimu.

Mimi binafsi sina elimu ya maji lakini nimekuwa mara nyingi nikiandika kuwa bila bwawa tatizo la maji halitaisha. Hayo maji yasingetumiwa na huyo mchina* ni wazi yangeishia baharini, lskini tatizo la maji Dar lipo tangu miaka ya sitini na miaka ya sabini tulishuhudia tukiletewa tope na visingizio kibao!
Tatizo kubwa ni jiwe aliyepindisha mpango wa kujenga Bwawa la Kidunda. Ilifahamika tangu zamani kuwa huo mto unakauka na wala si kwa kuchepusha maji na hivyo bwawa lijengwe Ili kufanya maji yatiririke kwa kiwango sawa wakati wa kiangazi. Jiwe aliyekuja na pepo la kuachana na miradi ya mtangulizi wake ndio matokeo ya chaos zote hizi. Ukweli usemwe tu.
 
Back
Top Bottom