Msitegemee ajira serikalini - Waziri Simba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msitegemee ajira serikalini - Waziri Simba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Nov 2, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Na Agnes Mwaijega

  WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi.Sophia Simba, amewataka vijana kutegemea shughuli za ujasiriamali ili kujikomboa
  kiuchumi na kuondokana na umasikini badala ya kujenga tabia ya kutegemea kuajiriwa na serikali.

  Akifungua Tamasha la wanawake wajasiramali (MOWE) yaliyoandaliwa kwa ushirikiano kati na Shirika la Kazi Duniani (ILO) Dar es Salaam jana, Waziri Simba alisema hatua hiyo itawawezesha vijana kuondokana na umasikini.

  Alisema hivi sasa nafasi za ajira ni chache ikilinganishwa na idadi ya vijana hivyo dawa ni kuondokana na dhana potofu ya kusubiri serikali kuwapatia ajira wakimaliza masomo yao.

  "Nawaomba vijana wajikite katika ujasiriamali ili waweze kupambana na changamoto mbalimbali za maisha," alisema.

  Aliongeza kuwa shughuli za ujsiriamali ni muhimu na zinachangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa hivyo kuwataka watanzania kuendelea kujishughulisha zaidi katika ujasiriamali ili taifa liweze kuwa na maendeleo mazuri.

  Pia aliwataka wajasiriamali kuzingatia kanuni na taratibu za ujasiriamali ili waweze kuwa na mafanikio makubwa na kuhakikisha wanatumia fursa na huduma mbalimbali zinazotolewa na serikali taasisi mbalimbali ili kuweza kufikia viwango vya kimataifa.
   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Haya kama Serikali kuu haiajiri sasa vijana wetu wataenda wapi na wakati Ardhi na Madini tunawapa wazungu na waarabu?
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Labda wamtafute Ridhwani awaonyeshe jinsi ya kuishi kimjini mjini and becoming a millionaire.
   
 4. O

  Ogah JF-Expert Member

  #4
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  waache ku-recycle wazee.........
   
 5. v

  valid statement JF-Expert Member

  #5
  Nov 2, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  serikali ishawatupa wananchi wake hii.
   
 6. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #6
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Naona hujamuelewa Waziri. Pamoja na ajira za Serikali zipo fursa za vijana kujiajiri na kupata mafanikio zaidi. Suala la ajira binafsi si kwa nchi yetu pekee bali duniani kote na tafsiri yake siyo kwamba ni kukosa ajira ya Serikali bali ni kupanua wigo wa ajira, mfano; Ukimiliki Shule, utakuwa umejiajiri lakini wakati huo utakuwa umeajiri watanzania wengine ambao hawakubahatika kupata ajira ya Serikali.
   
 7. Hakikwanza

  Hakikwanza JF-Expert Member

  #7
  Nov 2, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,898
  Likes Received: 307
  Trophy Points: 180
  Hata ujasiriamali wenyewe unahitaji fursa na mazingira mazuri.
   
 8. K

  Kubingwa JF-Expert Member

  #8
  Nov 2, 2011
  Joined: Apr 23, 2010
  Messages: 502
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Jamani mitaji,angetupa jinsi ya kupata mitaji.Tukaibe ndo tuwe wajisiliamali?
   
 9. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #9
  Nov 2, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Mkuu serikali inanisaidiaje niweze kuwa mjasiriamali wakati sikopesheki na taasisi yoyote ya fedha? Serikali lazima itengeneze mazingira ya kuwafanya vijana wajiajiri sio kama hali ilivyo sasa hayo anayoyaongea waziri ni sawa na dhihaka..
   
 10. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #10
  Nov 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Viongozi wetu ni wepesi kuwaambia watu wasio na chochote wajiajiri wakati wao ambao wameshajilimbikizia kwa miaka mingi hawataki kustaafu na kijiajiri na kuajiri wengine. Safari bado ni ndefu kuifikia nchi ya ahadi.
   
Loading...