Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Mwaka 2014 mwezi March Uli Hoeness rais wa zamani wa klabu ya Bayern Munich alihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela baada ya kugundulika amekwepa kodi.
Alikiri mahakamani kwamba alikwepa kulipa jumla ya euro milioni 18.5 ambazo alipaswa kuzilipa kwa benki moja ya Uswisi, ambapo ameweka fedha zake. Kwa shabiki wa kawaida wa Bayern Munich na mjerumani mwenye kuifahamu vizuri historia na mchango wa Uli Hoeness kwenye soka, habari ya kufungwa kwake ilikuja na mshtuko kwa kuzingatia heshima aliyonayo.
Baada ya kutumia nusu ya muda wa kifungo, hatimaye mwaka 2015 akaachiwa huru. Hapa kuna funzo zito sana kwetu sisi watanzania. Tangazo la mheshimiwa rais hurudiwa tena muda ule ambapo watu wanajiandaa kuangalia taarifa ya habari ya kutwa nzima. Kuomba risiti ndio umekuwa utamaduni mpya.
Ikiwa mpaka mtoto mdogo wa darasa la kwanza anakwenda kununua gazeti mtaani halafu anaomba kupewa risiti maana yake anajengewa utamaduni wa kutambua mchango wa ulipaji kodi kwenye maisha yake. Ipo haja kwa TRA na serikali kwa ujumla kukuza zaidi ule utaratibu wa watu kufahamu kwamba ulipaji wa kodi sio mzigo.
Wajerumani walimsikitia Hoeness wakati akienda kutumikia kifungo cha miaka mitatu. Lakini hakuna mjerumani ambaye hafahamu maana ya yeye kuwa mlipa kodi. Kuna kila sababu kwa watu kupewa elimu pana zaidi ya faida za kodi. Rais anajenga hoja kwa kutumia mfano wa mrejesho wa fedha za kodi kwa faida ya kuboresha huduma za jamii. Lakini kodi inayokusanywa kutoka kwa watu wenye ufahamu wa maana na umuhimu wa ulipaji wake, inatumika zaidi ya kuboreshea huduma za kijamii.
TRA na serikali mnalo deni kubwa la kutoa elimu pana ya masuala ya kodi, ili sisi tunaofundishwa umuhimu wa kudai risiti, tusione kwamba ulipaji kodi ni mzigo maishani mwetu.