Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,324
- 152,136
Mimi sina imani kabisa na waheshimiwa wa chama fulani na mara nyingi mkiona wamecharuka basi mjue tatizo linaweza kuwa ni maslahi japo hawatamki hadharani kuwa tatizo ni ukata.
Juzi juzi wote tumesoma kwenye vyombo vya habari waheshimiwa wakilia hali ngumu kutokana na serikali kutopeleka fedha zaidi ya shilingi bilioni 8 kiasi kwamba walikuwa wanapiga deshi,kuhama kutoka kwenye mahoteli na kuamia guest house,n.k.
Yote mnayoyasikia sasa bila shaka yanachochewa na mambo kadhaa likiwemo hili la ukata na pengine na swala la bwana Bashite.
Kwa mtazamo wangu,mpaka hivi sasa bwana mkubwa atakuwa ameshajua au ameshatonywa kuwa tatizo kubwa hapa ni nini na ili kukata mzizi wa fitini basi ameshaambiwa nini cha kufanya hivyo nae atajiongeza kwa kuwapa wanachokitaka ili nae awe salama hata kama hapendi.
Nawaambieni waheshimiwa hawa wakipozwa tu kwa kuongezwa mishahara na marupurupu hata kwa kupewa ahadi tu watatulia kama maji ya mtungi na wakiibuka tena mjue basi ahadi haijatimizwa.
Nina imani na wale wachache lakini sio hawa wengi.Katika wale wengi nina imani na mmoja tu mpaka sasa.
Waheshimiwa hawa wanaweza wakaungana kwenye swala la Bashite tu lakini sio kwenye maswala mengine ya kitaifa.