Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,367
- 2,407
Taifa litaloshindwa kuwajibika kwa raia wake linakaribisha milango yote ya kutawaliwa na mataifa yanayoweza kutawala (aka mabeberu) iwe ndani ya Afrika au nje. Tanzania katika utawala wa CCM imeshafikia na kutimiza masharti yote ya kuingia katika uwanja wa kutawaliwa.
Wapi CCM ilikosea? Dhana ya kutoshirikisha wadau wenye mawazo mbadala wa kuendesha nchi, ni kosa kubwa CCM inalolifanya. Pamoja na udhaifu wa katiba tuliyonayo sasa hivi, lakini ipo wazi kabisa kuwa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na imeruhusu kuwa na vyama vingi. Unaposhindwa kuwaheshimu viongozi wa vyama vingine ambao wanawafuasi wengi tu, ni kutokuwajibika kwa wananchi wako. Hili ni kosa kubwa sana na litaigharimu Tanzania leo au kesho. Na vyote vinavyotengenezwa sasa hivi ikiwemo miundo mbinu inaweza kuharibiwa kwa miezi tu.
Wadau wa siasa wanauamuzi wa kutumia njia yeyote ile kutimiza malengo yao, kama njia ya kidemokrasia itafungwa. Hii imeshuhudiwa pahala pengi. Ni wajibu wa serikali iliyopo madarakani kutumia hekima na busara, na kutumia vizuri nguvu waliyonayo ikiwa ni pamoja na matumizi ya Vyombo vya Dola, Polisi, Jeshi na usalama wa taifa kwa faida ya wote hasa wakati huu wa uchaguzi.
Kitendo cha kuwakamata viongozi wa vyama na kuwapiga/kuwatesa wakiwa chini ya ulinzi ni udhaifu mkubwa kabisa wa serikali iliyopo madarakani. Halikadhalika kuua, kutesa na kuwapiga raia wako kwa kutumia Vyombo vya Dola ni kutokuwajibika kwa serikali kwa raia wako.
Huu ni wakati muafaka wa serikali kuamka wakati nchi za nje au jumuiya tofauti zimepaza sauti juu ya uonevu unaofanywa na serikali kupitia vyombo vya dola kwa wananchi wake. Ni dhahiri kuwa kwa sasa hawa viongozi wa vyama na wananchi walioteswa na kupotelewa na jamaa zao, wataziona hizi nchi za nje na jumuiya tofauti kama watetezi wao. Sitoshangaa kama nikiwasikia waliodhulumiwa wakisema bora mkoloni yule kuliko huyu asiyetusikiliza kabisa. Hapo tutakuwa karibu sana na kutawaliwa kuliko wakati mwingine wowote ule.
Kuepuka hilo, Serikali ya CCM lazime ianzishe mazungumzo ya maridhiano na wadau wenzake wa siasa. Uamuzi ni wao ama wanataka tujitawale au tutawaliwe. Muda hatuna, ningependa kuisikia serikali inatoa tamko hilo leo la Maridhiano ya kitaifa. Nitashangaa kuona kama serikali itaendelea na mtazamo wake walionao sasa hivi wakidhani watashinda.