Mwaka 2015 kuna kiongozi mmoja wa CHADEMA ngazi ya Jimbo alikwenda kwenye Kijiji fulani ndani ya Jimbo lake na kukuta uongozi wa Kijiji hicho ni CHADEMA. Akashangaa Sana.
Alipouliza imekuwaje viongozi wa Kijiji kile kuwa wa CHADEMA, akaambiwa ni wananchi wenyewe waliamua wawe CHADEMA na kupambana kuweka viongozi wa Kijiji toka CHADEMA.
Viongozi wa CHADEMA huwa wanashangazwa na jinsi wananchi wa kawaida kabisa wanavyoijenga CHADEMA.
CHADEMA ni watu wa kawaida kabisa wenye uzalendo kwa nchi yao. Imani yao Iko Kwa CHADEMA na siyo kwa watu wanaoiongoza CHADEMA pekee.
Ndiyo maana hakuna mtu atatoka CHADEMA halafu CHADEMA isiwe CHADEMA.