DELETED ACCOUNT
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 9,805
- 15,470
Moja ya jambo ambalo wengi hamjashtuka lililofanywa na Simba kuanzia mwishoni mwa msimu uliopita waliposaini mkataba na JayRutty hadi usajili wa sasa wa wachezaji wa Mamelodi, ni kuipa pressure ya kifedha Yanga.
Hizi timu mbili zinapenda sana kuigana. Kuna wakati hadi nakereka jinsi wanavyopenda kufuatana fuatana. Mmoja akifanya jambo linaloonekana bora, mwingine hataki muda mwingi upite asije akaonekana hakufanya jambo fulani. Kwa miaka mingi Yanga imekuwa inazodolewa kwa kuwa nyuma katika mambo mengi mpaka yafanywe na Simba. Siku hizi, Yanga wanahakikisha hata kama watachelewa kufanya jambo fulani lililoanzishwa na Simba, ila watahakikisha nao wanalifanya msimu huo huo ndani ya muda mfupi.
Mkataba wa JayRutty uliorodhesha mambo mengi ambayo kwa timu hizi mbili hayajawahi kufanywa. Hapa nitaorodhesha matatu.
1. Mkataba rasmi wa jezi na brand ya kimataifa (Diadora)
2. Basi la kisasa la Irizar
3. Uwanja
Nilivyosikia tu haya mambo yanapangwa nikasema Yanga wataenda kujipanga ili Simba ikianza tu kuyafanya, nao wajitutumue wafanya bila kuchelewa.
Kwenye jezi, inasemekana Yanga imeenda kufanya janja janja na wanakaribia kutangaza mkataba wa jezi na Adidas kupitia kwa GSM. Ikumbukwe Sheria Ngowi aliwahi kusema tayari ana design za jezi za Yanga za misimu kadhaa mbele zipo tayari, ila baada ya Diadora kutangazwa, wakaachana na Sheria. Wameingiwa na pressure.
Kwa wachezaji wa kutoka timu kubwa kama Mamelodi naona hilo limewashinda ila ngoja tusubiri, wanaweza nako wakajitutumua wakamshusha Mokoena.
Hii pressure ya kifedha Yanga wataiweza? Wataweza nao kuleta Irizar msimu huu ili wasionekane wamechelewa? Wataweza nao kuanza ujenzi wa uwanja wao ili wasipitwe na Simba au watatumia wanasiasa na watendaji ili wakwamishe mipango ya Simba?