Msimbo wa Tarehe 29/10: Lengo, Kizingiti, na Mfumo wa Nne

Msimbo wa Tarehe 29/10: Lengo, Kizingiti, na Mfumo wa Nne

888I

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
445
Reaction score
553
Ndugu zangu wana-Jukwaa,

Kadiri kalenda inavyoelekea kwenye Tarehe 29.10, tunajiuliza:
Je, "Jibu" litatokea kama tunavyotarajia? Kuna ishara kwamba kadi ya kwanza huenda ikashinda safari hii na kuingia kwenye chumba cha Mfalme.

Tuseme kwa lugha ya hesabu, A atapata jibu linalohitajika kwenye jaribio. Huenda.

Lakini, Safari ya A inaonekana kuwa baada ya miezi 24. Ndiyo, miaka miwili ni muda mrefu sana kwenye dunia ya "kifungo cha madaraka." baada ya muda huo, Mfumo Mkuu unaweza kufanya mabadiliko ya ghafla.

Siyo tu kwamba Mtu wa Kwanza huenda asimalize mzunguko wake, iwe ni kwa sababu ya uchovu wa mfumo (A 'kufa' kiutawala au kiafya) au kupotea uwezo wa kushikilia Fimbo Kuu.

Mvutano wote huu unalenga Msaidizi wa Tatu. Kila dalili inaonesha kuwa, ikiwa A ataondoka mapema, yule wa Nafasi ya Tatu (tumuite C) ndiye atawekwa kukaa kwenye Kiti cha Enzi.

Lakini hata Msaidizi wa Tatu naye hayuko salama kabisa. Atakabiliwa na mawimbi makubwa sana — atakuwa taabani. Hii si kwa bahati mbaya. Kuna Kikundi cha Siri ambacho kimekuwa kikitengeneza meza kwa muda mrefu (Tumuite Msimamizi wa mtandao). Msimamizi wa Mtandao haumtaki A, wala B , wala C. Wao wanahitaji Mtu Fulani Maalum (tumuite D) ili aingie na kukaa kwenye Kiti cha Enzi, ili kuendesha mfumo wote kwa malengo yao ya Siri. 😂😂😂

Haya ni mawazo tu si uhalisia
 
Back
Top Bottom