Msimamo wa Mheshimiwa Wenje juu ya Mwenyekiti wa NCCR. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Msimamo wa Mheshimiwa Wenje juu ya Mwenyekiti wa NCCR.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gwalihenzi, Jun 5, 2012.

 1. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  [TABLE="width: 879"]
  [TR]
  [TD="bgcolor: #ffffff"][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]Wenje achachamaa

  na Mwandishi wetu
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][TABLE="width: 599"]
  [TR]
  [TD]
  MBUNGE wa Nyamagana, Ezekiel Wenje (CHADEMA), amesema kamwe hatakiomba radhi Chama cha NCCR-Mageuzi kwa kuwa anaamini Mwenyekiti wa chama hicho, James Mbatia, ambaye hivi karibuni ameteuliwa kuwa mbunge na Rais Jakaya Kikwete hana ujasiri wa kuikosoa serikali.

  Wenje alitoa kauli hiyo jana alipozungumza na Tanzania Daima kuhusu tamko la Chama cha NCCR-Mageuzi kumpa mwezi mmoja kuwaomba radhi kutokana na kauli dhidi ya Mbatia kwamba chama hicho ni CCM B.

  Alisema hata wakimpa mwaka mzima, hataomba radhi kwa kuwa anaamini katika msimamo wake.
  "Naomba nitoe msimamo wangu kwamba mimi Wenje nilitoa maoni kama Wenje na si kwa niaba ya CHADEMA na kama Mtanzania mwenye haki ya kutoa maoni yake.

  "Kauli niliyosema na narudia na sijutii na sifuti ni kwamba Mbatia ambaye ni mpinzani, Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi kuteuliwa na Rais Kikwete ambaye ni Mwenyekiti wa CCM kuwa mbunge, maana yake Kikwete amempa ajira ya kwenda bungeni," alisema.

  Wenje alidai kuwa Mbatia hawezi kuwa jasiri wa kusimamia na kukosoa serikali ya Kikwete ndani ya Bunge, ambaye ndiye amempa mamlaka na ajira ya kuja bungeni.

  "Yani hapa duniani, hakuna mtu aliyewahi kuwa mkali dhidi ya bosi wake. Huu ujasiri utautoa wapi? Mimi bosi wangu ni watu wa Nyamagana walionipigia kura na CHADEMA walionipa ridhaa ya kugombea. Leo hii mimi siwezi kusimama ndani ya Bunge nikaipiga CHADEMA mkwara.

  "Hivyo hivyo wabunge wa Viti Maalumu wanafanya kazi kwa niaba ya vyama vyao. Kwa hiyo Mbatia mamlaka yake ya kuja bungeni yametokana na huruma, fadhila na utashi binafsi wa Rais Kikwete, sasa haiwezekani Mbatia kuwa na ujasiri wa kuikosoa serikali yake. Hapa ni kudanganyana na mimi kama Wenje msimamo wangu ndio huo," alisema.

  Aidha, alikanusha madai kuwa amekiita chama hicho CCM B na kusisitiza kuwa alichosema ni kutokuwa na imani na Mbatia.

  Chama hicho, kimesema kuwa ndani ya mwezi mmoja endapo Wenje hataomba radhi kitamburuza mahakamani.

  [​IMG]

  juu[​IMG] [​IMG]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono kauli ya Wenje, yale yanabaki kuwa maoni yake hinafsi na si msimamo wa CDM, na yule mbunge Machali yule dawa yake nayo inachemka 2015. M4C wakapige kambi jimboni mwake aone mtiti wake.
   
 3. Olaigwanani lang

  Olaigwanani lang JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 26, 2012
  Messages: 480
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  msimamo ni kitu kizuri sana.......!
  uwe mfano wa kuigwa.....!
   
 4. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hivi hata ukisema ukweli napo inabidi uombe radhi?
   
 5. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  very short and clear,wenje kajibu kwa ufasaha sana majibu yake yanajitosheleza,kwanza yanabaina kuwa ni kauli yake na si chama,pili yanapigilia msumari tamko la kwanza,tatu yanaonesha kujiamini kwake,nne yanatoa onesha mahakama ipo kwaajiri ya haki hivyo yupo tayari,tano yanaonesha Wenje anakijua anacho kisema.WAKATI NDIO SASA,UNANGOJA NIN?
   
 6. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kibaraka kimepewa fadhila kinataka kiombwe radhi, kwani uwongo?.
   
 7. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yuko sahihi Wenje,yule Mkosamali nilimdhaniaga mtu makini kumbe hovyo kabisa no wonder ndo maana anampiga vita hata mwenzie Kafulira
   
 8. MANGUNGO

  MANGUNGO JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 1,538
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 133
  Moses Machari ccm B
   
 9. Mandingo

  Mandingo JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 22, 2011
  Messages: 3,381
  Likes Received: 318
  Trophy Points: 180
  Kula 5 mbunge wangu Wenje!
   
 10. E

  EL MAGNIFICAL JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 939
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  wabunge wengine vilaza kweli huu ni ujinga kauli aliyotoa anasema ni yake yeye kama yeye ni si chadema wakati huo huo aliyepewa madaraka ni mbatia sasa kwanini ahukumu nccr si angemsema mbatia kama mbatia lakini kwa kuwa yupo upande wa chama chenye nguvu basi imekua nongwa !
  Acheni wananchi ndo tupime !
  Inawezekana yule diwani mliyetema pale mwanza bado anakuchanganya akili !
   
 11. R

  RUTARE Senior Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni Moses Machali a.k.a ccm "B"
   
 12. K

  Kipimbwe JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 371
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ni Mosses kweli au mtu mwingine.Mosses najua huwa unapita pita humu nakuomba uwe unapima kwanza kabla yakumsikiliza mkombozi wa walima korosho(kama alivyojiita)
   
 13. S

  SANING'O LOSHILU Senior Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naunga mkono msimamo wa wenje manake kweli hiyo kwa mbatia ni ajira sasa katika logic ya kawaida mtu hawezi kumkosoa bosi! Jamani hili hata mwenye mawazo mafupi anaelewa si kila kitu kinahitaji elimu ya chuo kikuuu!
   
 14. K

  KISAKA MORIS JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 372
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ha'ha'ha inamaana Mbatia japokuwa nimetoka naye kijiji kimoja bado anataka tumhesabu kuwa ni mpinzani? Ama kweli kila mtu anatafuta kula yani kwa sasa yupo CCM lakini na upande wa upinzani bado yupo. Dunia ina mambo, niliambiwa nikue niyaone sasa nimekua na ninayaona.
   
 15. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  nataka nimuone siku ya kwanza bungen braza jemu atakataa upande gani,upande wa mwenyekiti bosi wake,au upande wa wapinzani?kwa kuwa anaenda kumwakilisha mwenyekiti wa ccm yafaa aitwe ccm A negative! Pia hatoweza kushiriki vikao vya wabunge wapinzani,na hatoweza kuingia vikao ya wabunge ccm. Namshauri viikitishwa vikao vya wabunge kivyama,yy asiende ukumbi wa msekwa wala wa kiongoz wa upinzani bali amtafute chibuda wakacheze golf au mchezo wa kufukuza panzi nje mpaka vikao vya wabunge halali vihishe! Mbatia ccm A negative!
   
 16. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  ni bora mbunge kilaza kuliko mwandishi taahira!ni wapi mbunge ametamka nccr kuwa ccm b kama si ww mwenye mchango wa kilaza?
   
 17. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Naona fahari kuishi jimbo hili la nyamagana,sijawahi kuijutia kura yangu ya ubunge,Viva E.D.Wenje
   
 18. Duble Chris

  Duble Chris JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 3,487
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  soma vizuri makala yake between lines utaelewa tu nadhani hapa umekurupuka
   
 19. M

  Mkwanda Senior Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 123
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Machali nilikua namkubali sna,kuna kipindi nilijua ni mbunge wa chadema badae nikagundua ni nccr nikasema kumbe nccr bado kuna majembe,he!ckuamini namna ambavyo akitetea ujinga live,nimepoteza imani na MOSES MACHALI kabisa hata kusoma upepo ameshndwa?safi sana kamanda WENJE.
   
 20. agatony8l

  agatony8l JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nami nilijua huyu mtu ni mpambanaji na nilikuwa namkubali sana lakini jinsi siku zinavyokwenda naanza kuona ni kama anategemea fadhila fulani toka kwa mwenyekiti wake wa chama kwani amekuwa mstari wa mbele kumtetea. Kiujumla namuunga mkono Mh. Wenje kwa kauli yake na msimamo aliouonhyesha. Kwa kweli hata mtoto wa darasa la kwanza anaweza kujumlisha moja na moja akapata mbili. Anatakiwa ajibu hoja je Mh. Mbatia ni mbunge wa upinzani au wa chama tawala???? Je anaweza kupinga kwa nguvu zote hoja kandamizi za magamba???? Hayo ndo maswali ya msingi. Yawafanyie kazi ili kutuprove Wrong sio kupoteza muda kwenda mahakamani.
   
Loading...