barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
Baada ya kuteuliwa kwa Ma-DAS wapya ambao baadhi yao ni Makada wa Chama Cha Siasa wakitoka ofisi ndogo na Makao makuu ya Chama,kumekuwa na mijadala mingi kuhusu uteuzi wao na nafasi yao ya kiutendaji ndani ya kofia ya Uanasaisa.
Wengi wa waliochaguliwa na Wajumbe wa NEC wa Chama Tawala ambao wanaendelea kushikilia nafasi zao hata baada ya kuteuliwa.Hali hii inazua mgongano wa kimaslahi kati ya utumishi wa Umma(Public Service) na Siasa.Tuangazie maelekezo ya Government Standing Order kuhusu Watumishi wa Umma walio ndani ya vyama vya siasa au wanaojihusisha na siasa.Na je Wizara ya Utumishi wa Umma chini ya Katibu Mkuu Dr.L.Ndumbaro ilijiridhisha juu ya wateuliwa hawa na ushiriki wao wa moja kwa moja katika siasa!??
Kuna haja ya watu walio karibu na Ofisi Kuu kuyatazama haya mambo kwa mapana..Mfano mdogo tu ni DAS wa Iringa ambaye ni Mjumbe wa NEC(MNEC) kupitia Shirikisho la Vyuo Vikuu Tz.