Msimamo wa CHADEMA kujiweka karantini siku 14 na namna walivyoandamwa na viongozi wa mihimili mikuu ya nchi

Areus

JF-Expert Member
Jul 27, 2016
324
403
Habarini wana Jf. Hongereni kwa kuendelea kuchukua tahadhari ya COVID 19.

Nimemsikiliza mbowe kwa umakini Sana wakati akieleza namna ushauri wao waliowahi kutoa wiki mbili au tatu zilizopita kabla ya kujiweka karantine siku 14 wabunge karibia wote wa Chadema. Mbowe amesema walishauri wabunge wote wapimwe Kwasababu ya kuanza kuwa na wasiwasi ya vifo vya wabunge wenzao vilivyotokea siku za karibuni ambavyo sababu zake zinaibua utata mkubwa.

Lkn amesikitishwa na namma Kiongozi wa Bunge alivyotumia nguvu kubwa kutoa majibu na wakati mwingine yanayomlenga Mbowe personally. Pia amesema kuwa Ushauri ambao Chadema wanautoa km Chama kuhusu Corona Wamekuwa wakiambiwa kuwa wanalichukulia Jambo la korona kisiasa kwamba kila kitu wanachoshauri ni siasa .

Amesema hiyo haijalishi ili Cha msingi viongozi hao Ni kutumia utu na heshima pale wanapotoa majibu yao bila kuvunjiana heshima.

Mbowe anasema wao wameenda bungeni kwa Kazi ya siasa, kwahiyo kuwaambia kila kitu wanachukulia kisiasa sawa tu lkn waangalie siasa Yao Ina mantiki gani Katika kujenga nchi.

Kwahiyo nilichomuelewa mbowe Ni kwamba zijibiwe hoja na sio kum attack yeye personally na kuacha kuwaambia wao kila kitu wanachukulia siasa wakati wameenda bungeni kwa sababu ya siasa.
 
Makonda aliposema wakamatwe mbona walikuwa dar kwenye Corona wanakula Bata karantini gani kwenda kwenye mji wenye wagonjwa wengi? Acha kudanganya umma.
 
Kwa hiyo Kama walikuwa Dar na makonda aliagiza wakamatwe. Je Ni Nani alikamatwa? Au barua ya polisi Ili mu address Nani pale na kwa kifungu gani Cha sheria

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya tamko la makonda, heche alionekana jioni chalinze nyama akinunua nyama, akiwa safarini kutoka dar kuelekea dodoma.
 
Back
Top Bottom