Kuna sehemu nyingine duniani hizi dini zinashirikiana kwenye mengi tu hadi raha. US kanisa la watu weusi lilichomwa moto na Waislamu wakachangisha pesa nyingi ili kulifanyia kanisa matengenezo, pia kuna msikiti ulichomwa moto wakristo wakachanga pesa nyingi kuufanyia matengenezo na wayahudi wakawaruhusu Waislamu watumie jengo lao wanalofanyia ibada mpaka msikiti utakapokuwa tayari kutumika tena.