Msikilize Nape akiinadi CHADEMA

Vp unatutajia walopokaji a.k.a premature, lema, mcgwa, sugu hawa nao wanawakilisha wananch? Sion wakisemea matatizo ya wananchi zaid ya kuropoka. Unauliza CCM imefanya nin? Mkubwa kichiz hata hujui! Mburula wewe. Sahz unaandika jf bila ccm ungejua kuandika wewe? Ndo sbb hamkubalik, et toka uhuru serikali haijafanya k2!
pumba tupu hizii
 
nina wasiwasi nawe yawezekana una urithi wa bendera hapo kwenu haiwezekani ukawa huoni waala tambua ushenzi na uzandiki wa ccm ndani ya nchi hii amakweli kuona kusikia na kutendewa na kutenda ni vitu usivyovitofautisha tusaidie mbunge wko nani? au wewe pia ni mbunge toka ccm maana huko ndiko walikojaa ma capt na ma canal japo jeshini walikuwa wapishi tu
 
Hivi wanabodi bado munadhani kweli CCM wana cha kuwaambia wananchi? CCM ni kama bondia aliyezidiwa hawezi peleka mashambulizi zaidi ya kujikinga na ngumi zaidi,ndicho wafanyacho sasa wamezidiwa,wamesogezwa kwenye kona na sasa wanafanya wasiyotaka ili angalau wasikilizwe........sijajua wakiwa na familia zao hali inakiwaje maana huwezi perform vizuri kwa mkeo wakati kichwani umejaa mawazo tena khs CDM maana bila shaka yanakusumbua kwa kiwango kikubwa......presha tupu.
 
Who is nape hata vichwa vyetu vimfikilie.he is just a houseboy for lumumba house.shut up us mouth
 

Kwa kweli inasikitisha sana kuona kiongozi wa ngazi ya juu kabisa anahutubia watu kwa kutengeneza uchochezi wa waziwazi kabisa. Hivi ccm wanaposema wanadumisha amani hivi ndivyo kweli. Mimi sielewi na sitaki kuamini kabisa kwa mtu kama Nape anayedai ana master's degree anaweza kuwa anaongea vitu vya kujenga chuki kwa wananchi kwa tuhuma ambazo hakuna chombo chochote cha usalama - mahakama, polisi n.k ambavyo vimewahi kuwatia hatiani chadema kwa kufanya mauaji? yaani bila hata ya aibu unadai chadema wamepanga kufanya maandamano yatakayoambatana na kumwaga damu - hivi Nape unayasema haya kwa vile hatulipii kuongea au umechukua muda wa kufikiri? Mbona unaendesha siasa za kuwajenga hofu watu badala ya kuwaelimisha waweze kuchambua pumba na chenga? Kwa hakika unaimaliza ccm badala ya kuijenga! Unakosea sana kudhani kuwa siasa za hofu zinaweza kuisafisha ccm? Km unakitakia chama chako mema you need to change now? Hautaweza kuwadanganya watu wote kwa wakati wote, unajidhalilisha sana, hata sielewi kama huwa unampelekea mwenyekiti wako wa chama mikanda ya hotuba zako? km ndivyo na anaiona iko sawa basi hatuna viongozi? Mbona viongozi wetu hawawezi kuongea kujenga hoja kwa sera? Nilitarajia Nape angewakosoa tu chadema kwa kuanzisha kanda kwa kutoa sababu jadidi badala ya kusingizia kuwa viongozi wametoka mifukoni mwa mwenyekiti? Hivi Nape alikuwa sehemu ya vikao vilivyoamua? Nape ni nani kudai madaraka kwenye kanda ni mgogoro? Nape hebu niambie sera ya kutotawalika unayodai iko ukurasa gani? walau nami niisome? Lakini pia sielewi ni kigezo gani Nape anatumia kudhani maandamano ni kitu kiovu- kitu ambacho kipo kisheria/kikatiba? CCM wakiandamana wanaita 'msafara' sasa chadema kuita maandamano ni nongwa? Nape wewe mvivu kabisa wa kufikiri na walahi sijawahi kuona katibu mwenezi wa hovyo kama wewe. Ni mara mia angepewa nafasi yako Tambalizeni.
 
Kuna mwanamuziki mmoja aliimba kuwa duniani kuna watu na viatu. Nahisi huyo N.pe ni kiatu. Badala ya kueneza sera za chama watu wakuelewe unaelezea chama pinzani. Duh kazi ipo.
 
Nape anasema " Wakati wa maandamano wanakuwa mstari wa mbele, risasi zikinguruma wanachomaka wanapotelea mbali" Nimemwelewa kwamba kila maandamano ya chama anachokizungumzia ni lazima risasi zingurume na huo lazima ni mkakati. Je hiyo ni sera ya kuwaeleza wana makambako au vitisho? Wananchi wanahitaji viongozi wa kuwasaidia kutatua matatizo waliyo nayo na wala hawahitaji uende kueneza sera za chama pinzani. Bwana Nape kama wewe ni msomi basi endana na usomi.
 
Back
Top Bottom