Msikilize Lema Upate Mshangao Jinsi Nchi Inavyoendeshwa

Msikilize Lema Upate Mshangao Jinsi Nchi Inavyoendeshwa

Hana kipyaa. Anafurahia kulelewa ugaibuni
Hivi Tanganyika na Zanzibar muungano wake kwa wananchi ukoje?? Je wantangnyika na wazanzibar ni wamoja au kila mtu anakwake?? Kama Moyo uko Zanzibar ukapewa watanganyika uwaongoze hauta wafanya wakambo kama moyo wako hauko Tanganyika??? Ninao wasiwasi na ukimsikiliza Lema yule mtu aliyekimbia nchi kwa usalama wake hasa kuhusu teuzi za mapolisi unaanza kuona uwakambo umetufika
 
Please listen to the end, utahudhunika na kuwashangaa wale wote wasemao nchi ina amani.

Nimesikia Ila duh...!.
ushauri wangu kwa watu hawa niliutoa hapa Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa, huwaletea hizi makala zangu za "Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni wito wa ustaarabu kwa Rais Samia, rais Samia Suluhu, sio malaika, ni binadamu kama binaadamu wengine wote na anaweza kukosea kama binaadamu wengine wote, kwa kufanya makosa ya kibinaadamu, hivyo nashauri, tusimfanyie nongwa, tusikalie kumlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa madogo madogo kabisa ya kawaida ya kibinaadamu, kwasababu binadamu wote huwa tunakosea, na hakuna mkamilifu.

Ila pale ambapo rais Samia amefanya makosa ambayo sio ya kwake, yale makosa ya kukoseshwa na wasaidizi wake au vyombo vyake, yakiwemo vyombo vya uteuzi vyenye jukumu la kufanya vetting, kwa baadhi ya watu wa hovyo hovyo kukwaa uteuzi, sio sawa, sio haki kumlaumu na kumshutumu mteuzi tuu yaani Rais Samia, nashauri kwanza, tumuonyeshe Mama Samia kuwa amechomekewa mabomu, kisha tumuonyeshe hayo makosa na makorokocho ya baadhi ya wateule wake walivyo wa hovyo, kisha tumvumilie kwa tumpe muda, atarekebisha mwenyewe yale makosa madogo madogo with time, tukiona ameambiwa makosa ya wateule wake, tukamuonyesha madudu ya wateule wake, na yeye akiwaona bado wanamfaa, tuheshimu maamuzi yake, tusimpangie kwa jinsi ile ile ambayo hatukumpangia mtangulizi wake.

Japo mkubwa ni jalala, na ukiwa kiongozi ni lazima uwe na ngozi ngumu, lakini tusimsakame saana Mama Samia kwa makosa ambayo sio makosa yake bali ni anakuwa ameshauriwa vibaya na wasaidizi wake.

Pili, Mama, Samia sio malaika ni binadamu tuu, kama binaadamu wengine, hivyo anaweza kukosea kama, binadamu wengine wowote, hivyo tujenge tabia ya uvumilivu kwa yale madogo madogo ya kibinaadamu.

Nakiri kupandisha bandiko kufuatia kelele nyingi za shutuma, lawama, kumsakama Mama Samia kwenye uteuzi wa baadhi ya ya wateule wake

Hitimisho
Kama ambavyo hatukumpangia Magufuli, nashauri pia tusimpangie Samia, tuepuke matukano, lugha za machukizo, ukali kebehi, kubagaza, tuendelee kumkosoa kwa lugha ya heshima, staha, kistaarabu kwa nia ya kujenga, huku tukikosoa constructively kwa nia ya kujenga huku tukishauri, the right thing to do.

Paskali
P
 
Back
Top Bottom