Mtaalamu wa siasa katika chuo kikuu cha Dar es salaam Dr. Benson Bana amesema kushindwa kwa ccm katika uchaguzi mdogo wa arumeru kunaonyesha jinsi gani chama cha mapinduzi kimepoteza mvuto kwa wananchi kutokana na kukiuka misingi ya kuwatumikia wananchi. Mtaalamu huyu wa siasa ambaye pia ni bingwa kutoa tafiti zinazoibeba CCM katika chaguzi zote amekisifia waziwazi chama cha CHADEMA na kusema kuwa kinakubalika na kina mvuto mkubwa wananchi hivi sasa.Ameyasema haya katika mahojiano yake na redio dochwvele ya ujerumani ambapo pia amekanusha kusema kwamba ccm kinampasuko huku akidai kwamba wabunge wake ndio wanatofauti na si ccm.Dr. Bana amesema hatashangaa kuona chama kingine kikishika dola mwaka 2015 kutokana na mwenendo huu wa chama tawala.
Source. Radio DW UJERUMANI IDHAA YA KISWAHILI.