Msikie huyu kilaza wa darasa

Tutorial 1X

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
1,908
2,036
Nilipokuwa shule ya msingi, kuanzia darasa la 4 hadi la saba, maksi zangu za hesabu kwenye mtihani zilikuwa zinacheza kuanzia 03% hadi 9% hazizidi zaidi ya hapo . Matokeo yalikuwa yanatangazwa mbele ya darasa!

Yanapotangazwa mwalimu huanza kugawa zile karatasi kuanzia maksi za chini kwenda za juu yaani (0-100), kwa hiyo darasa lote linajua kuwa vilaza wote huanza kupewa karatasi then wanafuata wale wenye maksi za juu,, wanafunzi wanajua kuwa karatasi zikiletwa ntaitwa kama si wa kwanza basi wa pili kutoka mwisho/ chini.

Siku moja mwalimu akaanza kuita majina, yaani mpaka anafikia kwenye maksi 40%,50%,60% 70% bado tu mi bado hajaniita. Watu wakaanza kuniangalia kwa shauku wakaanza kuniuliza, eheee umepasua nini mbona hujaitwa ilikuwaje?

Mzee, nikaanza kuvimba kichwa kuwa nimeshawakimbiza huku mwalimu anaendelea kuita majina na makaratasi,, yakabaki makaratasi mawili, yaani langu na la mwanafunzi mwingine hivi kati ya maksi 80% hadi 100%, jamaa akaitwa mi bado sijaitwa, watu macho kodo kwangu aisee…

Mara akabaki na karatasi moja mkononi! Yaani ya kwangu pekee. Watu wakajua nimepasua aisee.. Mwisho mwalimu akashusha pumzi ndefu kisha akasema kwa hasira `kuna ngo'mbe halijaandika jina kapata 0% aje achukue karatasi yake,, darasa buuuuuu!!!
 
Nmecheka adi nmetoa machozi...this is exactly what I needed to lift my mood up...
 
Back
Top Bottom