Msijidanganye, hakuna mwenye uwezo wa kuifuta CHADEMA

My Son drink water

JF-Expert Member
Joined
Nov 30, 2016
Posts
4,930
Reaction score
13,335
Kuna watu humu wanashangilia kimya kimya baada ya msajili wa vyama kuwalima barua nyingine CHADEMA akidai kuwa hakuridhishwa na majibu ya barua ya awali waliyojibu kuhusu vurugu za Kinondoni zilizopelekea kuuawa kwa Aquilina baada ya police kurusha risasi.

Kwanza nataka mtambue kuwa, CHADEMA siyo Tundu Lissu, siyo Mbowe, siyo Mnyika, siyo Halima Mdee, siyo Sugu, siyo Lema na wengineo ambao mnawaona Kero kiasi cha kushindwa hata kunywa maji vizuri.

CHADEMA ni umma wa watanzania waliochoshwa na utawala mbovu wa CCM wa miaka zaidi ya 50, utawala uliojaa ahadi hewa miaka nenda rudi.

Hao kina Mbowe ni wapiga kelele tu, ila kuna umma upo ambao ndo mtajua unafananaje siku mkisema eti tunaifuta CHADEMA.

Kufanya jaribio lolote la kuifuta CHADEMA, ni kuweka nyasi kavu juu ya makaa ya moto, ukijidanganya kuwa eti unafukia makaa hayo.

Ahadi ya Rais ni kuwa na Tanzania ya viwanda.
Nyie mnaolala mkiota eti CHADEMA itafutwa mtasubiri Sana.
 
Kuna watu humu wanashangilia kimya kimya baada ya msajili wa vyama kuwalima barua nyingine CHADEMA akidai kuwa hakuridhishwa na majibu ya barua ya awali waliyojibu kuhusu vurugu za Kinondoni zilizopelekea kuuawa kwa Acqulina baada ya police kurusha risasi.
Kwanza nataka mtambue kuwa, CHADEMA siyo Tundu Lissu, siyo Mbowe, siyo Mnyika, siyo Halima Mdee, siyo Sugu, siyo Lema na wengineo ambao mnawaona Kero kiasi cha kushindwa hata kunywa maji vizuri.
CHADEMA ni umma wa watanzania waliochoshwa na utawala mbovu wa ccm wa miaka zaidi ya 50,utawala uliojaa ahadi hewa miaka nenda rudi.
Hao kina Mbowe ni wapiga kelele tu,ila kuna umma upo ambao ndo mtajua unafananaje siku mkisema eti tunaifuta CHADEMA.
kufanya jaribio lolote la kuifuta CHADEMA, ni kuweka nyasi kavu juu ya makaa ya moto,ukijidanganya kuwa eti unafukia makaa hayo.

viwanda alivyoahidi ndo hivyo.vile viwanda hasa hana uwezo wala mbinu
 
mbona maneno yako yamekaa kivurugu vurugu? yaani ni kama unatishia kwamba amani itapotea siku chadema ikifutwa? huwezi andika kitu cha maana kidogo zaidi ya hiki ulichoandika?
 
Kwani wewe unaonaje ,siku ikifutwa amani itakuwepo tu?
mleta mada kaandika kwa hisia Kali sioni kama anatishia vurugu.
Watakaoleta vurugu ni wale waliopanga kufuta vyama Unadhani nini kitatokea mkuu?
 
Tutaenda ACT WAZALENDO, NCCR au CUF MAALIM, wakifuta vyama vyote tunasubiri CCM ipasuke makundi mawili ili tuchague kundi mojawapo. Ni suala la muda tu, hao madiwani/wabunge wanaokaribishwa huko na kupewa nafasi 2020 watavurugana maana CCM kindakindaki hawawezi kuona eti waliotoka upinzani wakiendelea kupewa shavu huku wenyewe wakiendelea kuwa waenezi wa tawi la CCM mtandaoni ( kwenye mitandao ya kijamii) tu
 
mbona maneno yako yamekaa kivurugu vurugu? yaani ni kama unatishia kwamba amani itapotea siku chadema ikifutwa? huwezi andika kitu cha maana kidogo zaidi ya hiki ulichoandika?
Vurugu lazima zitakuwepo, ina maana wewe hujiulizi? Unawezaje kuzima sauti za mamilioni ya watu, kumbuka kwamba upinzani ni Sehemu ya watu kutema nyongo zao sasa ukiwazuia kutema nini kitajili?
 
Kama Kuna mtu anafikiri kuifuta cdm kwa sasa mwambieni afikiri upya..mwambieni kipindi cha uangazi miti hupukutisha majani yote lakini haimaanishi kwamba mti unakufa..kipindi chake kuchanua upya kipo karibu.kuifuta cdm kwenye makaratasi inawezekana ILA SIO KWENYE AKILI ZA WATU
 
mbona maneno yako yamekaa kivurugu vurugu? yaani ni kama unatishia kwamba amani itapotea siku chadema ikifutwa? huwezi andika kitu cha maana kidogo zaidi ya hiki ulichoandika?
Mtumwa wewe ulitaka aandike Je?! Oh Jaji plz usitufute?! Jambo lililopo kisheria na kikatiba siyo la kumbembeleza mtu yeyote, hata kama ni huyo anayedhani kufuta vyama ndiyo maendeleo wanayotaka waTz .
 
Chadema inaweza kufutwa na kusitokee chochote, we sema tu mshipa wa aibu bado haujakatika.
 
Kuna watu humu wanashangilia kimya kimya baada ya msajili wa vyama kuwalima barua nyingine CHADEMA akidai kuwa hakuridhishwa na majibu ya barua ya awali waliyojibu kuhusu vurugu za Kinondoni zilizopelekea kuuawa kwa Acqulina baada ya police kurusha risasi.
Kwanza nataka mtambue kuwa, CHADEMA siyo Tundu Lissu, siyo Mbowe, siyo Mnyika, siyo Halima Mdee, siyo Sugu, siyo Lema na wengineo ambao mnawaona Kero kiasi cha kushindwa hata kunywa maji vizuri.
CHADEMA ni umma wa watanzania waliochoshwa na utawala mbovu wa ccm wa miaka zaidi ya 50,utawala uliojaa ahadi hewa miaka nenda rudi.
Hao kina Mbowe ni wapiga kelele tu,ila kuna umma upo ambao ndo mtajua unafananaje siku mkisema eti tunaifuta CHADEMA.
kufanya jaribio lolote la kuifuta CHADEMA, ni kuweka nyasi kavu juu ya makaa ya moto,ukijidanganya kuwa eti unafukia makaa hayo.
Ahadi ya Rais ni kuwa na Tanzania ya viwanda.
Nyie mnaolala mkiota eti CHADEMA itafutwa mtasubiri Sana.

Ukweli umpa mtu nafasi kubwa ya kufikuri na kutenda. Kwa hiyo ktk kutenda ukienda kinyume dhamira humuumbua mtu kwa muda husika. Kwa ujumla lazima tufike mahali tutanbue haya mapambano ni ya kiitikadi na kama ni ya kiitikadi lazima yatakuwa na machungu kwa wengi wanaoziishi hizo Itikadi.

Chochote kinachoishi roho kama imani siku zote Mtu akienda kinyume na wanaoziishi tegemea zuri au baya lakini yote hayo ni Mungu aluyetuumba na kuziweka Itikadi. Kwa hiyo Itikadi ni Imani kakamili kama ilivyo Imani nyingine hapa duniani. Kwa hiyo ktk maamuzi yoyote lazima yazingatie mazingira
 
We wajaze upepo tu wakifute kweli kweli mchana kweupee.

Hata Sugu tuliaminishwa akifungwa mbeya haitakalika lkn pako shwari tu watu wanakula starehe kama hapajatokea kitu vile.
 
Kwa hiyo mlimfunga sugu Kama jaribio la kupima reaction za watu kuelekea lengo lenu la kufuta cdm, huo Ni mzaa, wahenga walituambia mzaa mzaa hutumbua usaa
 
Nadhani unamaanisha MZAHA na sio mzaa.

Halafu mimi sihusiki na mambo ya kumfunga Sugu,niko zangu napambana na hali yangu mtaani siko huko serikalini.

So kuhusu kumfunga Sugu waulize CCM+SERIKALI.
 
Vurugu lazima zitakuwepo, ina maana wewe hujiulizi? Unawezaje kuzima sauti za mamilioni ya watu, kumbuka kwamba upinzani ni Sehemu ya watu kutema nyongo zao sasa ukiwazuia kutema nini kitajili?
mamilioni wapi unajidanganya!upo wewe na yule dada ako wa marekani tu ndio mnataka kuleta vurugu.
 
Back
Top Bottom