Msihukumu, msije mkahukumiwa

Msihukumu, msije mkahukumiwa

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
464
Reaction score
687
Mat18:23Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyeamua kukagua hesabu za watumishi wake.
Mat18:24Ukaguzi ulipoanza, akaletewa mtu mmoja aliyekuwa na deni la fedha talanta elfu kumi.
Mat18:25Mtu huyo hakuwa na chochote cha kulipa; hivyo bwana wake aliamuru wauzwe, yeye, mke wake, watoto wake na vitu vyote alivyokuwa navyo, ili deni lilipwe.
Mat18:26Basi, huyo mtumishi akapiga magoti mbele yake, akasema, Unisubiri nami nitakulipa deni lote.
Mat18:27Yule bwana alimwonea huruma, akamsamehe lile deni, akamwacha aende zake.
Mat18:28“Lakini huyo mtumishi akaondoka, akamkuta mmoja wa watumishi wenzake aliyekuwa na deni lake fedha denari mia moja. Akamkamata, akamkaba koo akisema, Lipa deni lako!
Mat18:29Huyo mtumishi mwenzake akapiga magoti, akamwomba, Unisubiri nami nitalipa deni langu lote.
Mat18:30Lakini yeye hakutaka, bali alimtia gerezani mpaka hapo atakapolipa lile deni.
Mat18:31“Basi, watumishi wenzake walipoona jambo hilo walisikitika sana, wakaenda kumpasha habari bwana wao juu ya mambo hayo yaliyotukia.
Mat18:32Hapo yule bwana alimwita huyo mtumishi, akamwambia, Wewe ni mtumishi mbaya sana! Uliniomba, nami nikakusamehe deni lako lote.
Mat18:33Je, haikukupasa nawe kumhurumia mtumishi mwenzako kama nilivyokuhurumia?
Mat18:34“Basi, huyo bwana alikasirika sana, akamtoa huyo mtumishi aadhibiwe mpaka hapo atakapolipa deni lote.
Mat7:1“Msiwahukumu wengine, msije nanyi mkahukumiwa na Mungu;
Mat7:2kwa maana jinsi mnavyowahukumu wengine, ndivyo nanyi mtakavyohukumiwa; na kipimo kilekile mnachotumia kwa wengine ndicho Mungu atakachotumia kwenu.
 
Karibuu mkuu tupatee chakulaa Cha ubongoo
downloadfile-3.jpg
 
Khaaaaaaaaa
Huu mshangao umenitusha! Una tabu gani na mafundisho ya kutokuhukumu wakati hata katika sala ya BABA yetu tunasali, "utusamehe makosa yetu kama sisi tunavyowasamehe waliotukosea"?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom