Msigwa atoboa siri

Kwanini hakuyasema alipokua veggies?
Wewe unahisi angepewa teuzi huko angerudi Chadema na kuongea hayo?

Wewe inaonyesha ni mgeni na Msigwa
Watu wamejisahaulisha alipoenda Ccm akasema Chadema wanatekana wenyewe kwa wenyewe.
 
Na aliyosema kuhusu CHADEMA akiwa CCM tuyaamini kwamba wanatekana , wezi chama cha watu binafsi, wachumia tumbo au haya tuachane nayo? Huyo ni malaya wa siasa anaweza akasema lolote tu akiachwa na bwana wake ni kama Chanuo tu yule muigizaji.
 
Hizo ni fikra zako, na zinaweza zisiwe sahihi.

Utambue kuwa kuna wengi wameichukia sana CCM na serikali yake, japo huko nyuma waliipenda sana. Uharamia ule wa watawala na CCM.uliofanywa Oct 29, umegeuza kabisa mioyo ya watu wengi hata ndani ya CCM. Ndiyo maana wengi waliokuwa waungaji mkono wa CCM lakini mioyo yao inathamini uhai na utu wa wanadamu wenzao, kwa sasa wana chuki kubwa dhidi ya wauaji. Cheo siyo kitu kinachoweza kumpofusha kila mtu. Kwani Nchimbi au Polepole hawakuwa na vyeo?Gwajima hakuwa na cheo?
 
Kuna ubaya gani baada ya kukosa uteuzi halafu akaongea ukweli?

Wewe focus na alichokisema hayo mengine ya uteuzi sijui nini achana nayo.

Wapo waliokuwa kwenye nafasi za juu za serikali lakini waliamua kusema ukweli wakiwa kwenye nafasi zao na wengine baada ya kujiuzulu.

Hao nao walikosa ulaji?
 
Nadhani ni muhimu sana kuwa mfuasi wa hoja na si mtu. Hoja yake ukichanganya na zako ina mashiko? Alipokuwa ccm hoja yake ukichanganya na zako ina mashiko?
 
Na aliyosema kuhusu CHADEMA akiwa CCM tuyaamini kwamba wanatekana , wezi chama cha watu binafsi, wachumia tumbo au haya tuachane nayo? Huyo ni malaya wa siasa anaweza akasema lolote tu akiachwa na bwana wake ni kama Chanuo tu yule muigizaji.
Km wewe unaona hivyo..ni sawa pia kwako, lkn kwa wale wenye uwezo wa kuangalia mambo kwa muunganiko wa pamoja..kile alichosema Mch. Msigwa kwamba ccm inamilikiwa na genge la wahuni wachache wanaomiliki pia vyombo vya dola na kuviamrisha wanavyotaka wao..ni ujumbe wa kuwaamsha watanzania juu ya nchi ilipo sasa.. ukielewa chukua, usipoelewa ukaona maigizo ya kuhama vyama ndio ajenda ya maana kwako ni sawa pia, baki huko..
 
Yuko sahihi, ila tatizo ni kuwa kuaminika. Unless alienda kule kuchunguza na kufukunyua.

Lakini awe makini, wanaweza kumpoteza.
Hiyo hofu ya kupotezwa nayo ni ushahidi.Iweje kila anayekosoa/kukataa kuwaunga mkono CCM na vibaraka wake anapotea/anapotezwa?Jibu lipo ubaoni nanyi mnaibiana majibu tena?
Wasiojulikana,wanaowateka,wanaopoteza wenzetu ni CCM.Ukweli usemwe kama ulivyo,hakuna asiyefahamu hilo.
Kinachokuwa kigumu kwa sasa ni wa kusema ukweli na kuthibitisha beyond reasonable doubt.CCM wasijifiche kwenye kichaka cha wasiojulikana maana wanajulikana.
Tunawasubiri wajichanganye na kibuyu cha ushahidi kijae vema.We are coming very soon.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…