Niko ktka muhusiano na binti mmoja hivi. Ni kama miezi 6 sasa. Ila ana wivu. Binafsi hatujaamua kuishi pamoja ila mambo yake.. Sijui kama na nyie mnafanyiwa haya.
Mfano.
1. Hataki kuniona nna simu, anakurupuka na kuangalia nafanya nn.
2. Nikipigiwa simu anasogeza kichwa asikie naongea na nan.
3. Anapost picha zake kupitia account yangu ya fb. Wakati mwingine huandika Mrs flani, yan mm.
4. Nikimalizia kuongea na mtu kwenye simu anachukua namba na kuifuatilia kwa mpesa au tigo pesa nk.
5. Anaangakia history kwenye apps zangu mfano Opera, nimefungua websites gani.
6. Anasoma emails, sms, post zangu kila siku na kuangalia nan amekoment na kuniuliza kwann amekoment hivo.
7. Hataki anipigie simu akute niko busy. Ananambia nilikua naongea na m/ke.
8. Hataki niwe online hasa whatsapp. Ananambia usiku huu online unafanya nn.
9. Hataki niende kwenye mechi za usiku. Anahisi eti tunaangalia mpira na Malaya.
10. Hataki nichelewe nikienda labda mjini. Anahoji muda wote huo, hapo tuu saa zote hizo.
11. Wakati fkan akaniuliza kuna mwanamke ana nguo ya kitenge kama chako ni nan yako. Au mmeshona sare.
12. Huchukua simu yangu na kuzi-foward sms zangu ktk simu yake na kuzijadili na marafiki zake.
13. Anakagua nyaraka zangu za siri. Yani documents. Mfano vyeti, ID's nk
14. Anafuatilia picha zangu, phone book, na apps mbalimbali na kunihoji.
15. Akituma sms nikichelewa kujibu ananambia nnamdharau.
16. Akipost picha nisipomsifia anachukia. Et wangekua wengine ungeona unavosifia.
Kwa ufupi nimevumilia hadi nimechoka. Nishaurini, sina ham naye tena.