Msichana wangu ana wivu. Nisaidieni

ytara jr.

Member
Feb 6, 2014
61
22
Niko katika muhusiano na binti mmoja hivi. Ni kama miezi 6 sasa. Ila ana wivu. Binafsi hatujaamua kuishi pamoja ila mambo yake.Sijui kama na nyie mnafanyiwa haya.
Mfano;
1. Hataki kuniona nna simu, anakurupuka na kuangalia nafanya nini.
2. Nikipigiwa simu anasogeza kichwa asikie naongea na nani.
3. Anapost picha zake kupitia account yangu ya Fb. Wakati mwingine huandika Mrs flani, yani mimi.
4. Nikimalizia kuongea na mtu kwenye simu anachukua namba na kuifuatilia kwa mpesa au tigo pesa nk.
5. Anaangakia history kwenye apps zangu mfano Opera, nimefungua websites gani.
6. Anasoma emails, sms, post zangu kila siku na kuangalia nani amekoment na kuniuliza kwanini amekoment hivo.
7. Hataki anipigie simu akute niko busy. Ananambia nilikua naongea na m/ke.
8. Hataki niwe online hasa whatsapp. Ananambia usiku huu online unafanya nini.
9. Hataki niende kwenye mechi za usiku. Anahisi eti tunaangalia mpira na Malaya.
10. Hataki nichelewe nikienda labda mjini. Anahoji muda wote huo, hapo tuu saa zote hizo.
11. Wakati flani akaniuliza kuna mwanamke ana nguo ya kitenge kama chako ni nani yako. Au mmeshona sare.
12. Huchukua simu yangu na kuzi-foward sms zangu katika simu yake na kuzijadili na marafiki zake.
13. Anakagua nyaraka zangu za siri. Yani documents. Mfano vyeti, ID's nk
14. Anafuatilia picha zangu, phone book, na apps mbalimbali na kunihoji.
15. Akituma sms nikichelewa kujibu ananambia ninamdharau.
16. Akipost picha nisipomsifia anachukia. Eti wangekua wengine ungeona unavyosifia.

Kwa ufupi nimevumilia hadi nimechoka. Nishaurini, sina hamu naye tena.
 
Huyo anakuletea maigizo ya kihindi, inaonekana wewe ni mtu wa kupeti peti sana. Ukisimama kama mwanaume na kua na kauli zilizo nyooka atarudi kwenye mstari.

Enewei kama amekuchosha zaidi ni pm namba yake.
 
Back
Top Bottom