Msichana huyu alinitoa nishai balaaa.....

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,267
9,651
Leo nataka niwape story ya mkasa flani uliyo nikumba kipindi nimemaliza kidato cha sita.
Wakati niko katika kusubiri matokeo ya mtihani wa kidato cha sita nilikuwa sina kazi maalimu hivyo nilikuwa ni mtu wa kukaa home na kuwatch movies na kuwepo kuwepo tu. Sasa kuna rafiki yangu flani alinipa anuani ya mtandao ambapo nilliweza download application flani ya simu ijulikanayo kama mig33 amabayo inamwesesha mtumiaji wa simu kuweza kuchati na watu mbalimbali kwa instant messages walioko online pia kupga simu kwa garama nafuu via internet as well as kutuma sms katika simu na mpokeaji atajua umetuma kwa simu yako kama kawaida.
Kwa afrika mashariki atumiaj wa mig wengi ni wakenya na wazanzibari hao ni wengi sana ten asana. Kwa muda wa wiki 3 toka nilipojiunga niliweza kupata marafiki wengi na hasa wasichana amabao tulizoeana sana mpaka tukabadilishana namba za simu na ikwa ikitokea sijaonekana online lazima nipigiwe simu kuulizwa nini kimenisibu.
Kati ya hao wasichana kuna msichana mmoja ndiye ningependa kumwongelea siku ya leo. Huyu alikuwa mwaka wa pili chuo kipindi mimi nimehitimu kidato cha sita. Mimi sasa niko mwaka wa tatu. Tulizoeana kuzidi kipimo nay eye ndiye aliyekuwa anapenda sana chat na mimi kiasi kwamba alikuwa na mazoea ya kunitumia vocha ya buku 2 kila siku ilimradi niwe online kwakuwa sometime nilikuwa nashindwa pata ela ya vocha kwakuwa sikuwa na shughuli yoyote kwa wakati huo.
Siku zilivyo zidi kwenda alinizoea sana hadi akaanza niambia mambo yake ya private. Aliniambia kwamba yeye ana mchumba ambaye anatarajia kuoana naye mwez wa kumi nambili huo huo mwaka. Akaniambia ya kwamba yeye alikuwa anaishi nje ya nchi na alikuwa ana mchumba wa kizungu lakini ilitokea siku moja akawa amerudi tz sa wakati yuko maeneo ya posta akakutana na her first love (ndiye huyo mchumba aliyeniambia kuwa amedhamlipia mahari ndoa mwez wa 12) na mara gafla penzi lao la form two likachipua. Kipindi hicho alikuwa chuo mwaka wa kwanza huko huko nje nchi sitoitaja ndiko alikokuwa akiishi na huto bwanake wa kizungu mabaye yeye ni daktari.
Aliporudi huko nje mawazo yake yote yakawa kwa her first love akaamua kumpa mzungu ukweli chuo akaacha akarudi tz akasubiri mwaka unaofuata akaanza tena mwaka wa kwanza chuo flani na wakati huo alikuwa mwaka wa pili keshavishwa pete na huyo mchumba.lakini wakati ananipa hiyo story alidai kwamba tatizo alilokuja kugundua ni kwamba mchumba wake ni bonge la player na ashamfumania zaidi ya mara 4 na alipomfumania mara ya mwisho alimshusia kipigo kwa nini eti anamfuatilia mambo yake.
Ili story yangu iwe fupi siatawapa sababu lakini yeye na huyo mchumba wake hawakuona waliachana lakini kipindi wanaachana huyo msichana alikuwa mjamzito. Sasa katika kuchat si tukajikuta tumeanza mahusiano yeye alikuwa akipenda nitumia picha zake lakini just passport size si mwili wote name pia hivyo hivyo. Bsi tukaendelea mpaka nilipoanza chuo ndipo tukakutana .
Daah yani zile imagination zangu hazikuwa sahihi hata kidogo nilimkuta boooonge sana naye alitegemea mimi nina big body kanikuta wa kawaida sa ikawa ka mtu na dadake au shangazi yake. Nilikuwa namwogopa hat mhug but yeye akaona poa na nilikuta ana mkwanja balaa kumbe alirusiana na mzungu wake.
Tuakendelea na mahusiano lakini nikijua kuwa anamzungu wake coz kuna mda mzungu alikuja nami nikakata mguu mpaka alipoondoka. Tatizo huyu msichana alikuwa na wivu na mimi sana kumbe si aka huck simu yangu yani kila sms nayo tuma nakutumiwa anapata copy yake akagundua kuwa nina msichana mwingine ninaye mpenda na kwake nipo kimasirai zaidi. Ali huck simu yangu kwamisezi mitatu na kwa mda wote hakuniambia kitu wala kuonesha mabadiliko.
Siku tukiwa tumeka bar nikawa nataka shika simu yake akainipokonya. Mimi nikamwambia mbona wajishtukia wewe una nini cha kuficha. Akajibu hata wewe ndo wajishtukia mwenye mpenzi akamtaja jina mpenzi wangu, nikabaki nashangaa amejuaje, mara akanitajia jina mwingine mara password yangu ya fbuk akanitajia mara ya email yangu mara akaanza nionesha message nazochat na galz wengine anazo kwenye simu yake. Nilikuwa mdogo ka pilton nikakosa la kusema nikabaki nashangaa.
Toka siku hiyo mahusianao ya kimapenzi naye tukavunja tukabaki marafiki wakubwa. Hivi navyoongea yuko U.S anasoma masters nan i rafiki yangu mkubwa ila hakuniambia aliweza huck kwa njia gani line zangu.
 

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,558
Duu pole mkuu, nakushauri endeleeeni kuwa marafiki tu kama mlvyo sasa! Maana inaonyesha wazi kuwa wewe unaye umpendaye na ulikuwa kwake kimaslahi ziadi na pia yeye pia hana msimamo, mara na mzungu mara na first love wake loooo!

Umecheki ngoma mwana???
 

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,267
9,651
daaah kupima nshapma na hata hivyo sikufanya lolote naye kwakuwa kama ulisoma vizuri nilipokutana naye nikakuta booonge nkawa hata namuogopa flani na sikuwa na hamu naye kusema kweli.
 

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,267
9,651
amini usiamini lakini ni story ya kweli na imenitokea mimi mwenyewe
 

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
9,547
Mwaka wa tatu then story ziko hivi! Faculty gani mkuu? Bila shaka we daktari.
 

elmagnifico

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
8,267
9,651
sasa wewe ambacho hujaelewa ni nini coz swali lako halina msingi.@nyani ngabu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom