Msichana ana mpenzi, Namimi nimempenda

Geniustin

JF-Expert Member
Mar 15, 2013
4,371
2,832
Heshima yenu wadau,

Ni hivi juzi kati wakati namtupia mawili matatu(Namtongoza) Msichana mmoja hivi, Jibu alilionipa alisema ana mpenzi.

Wadau naomba ushauri wenu nifanyaje/nimwambiaje kuSolve hiyo Situation? Na Hilo jibu lake niweze kuliNeutralize?

Maana hilo jibu liliniacha njia pande, nikawa nakosa niseme nini!

NB;
Tuchukulie ni kweli ana mpenzi,
Naomba ushauri niseme nini/kufanya nini ili tu niwe naye na nina mpenda.

NOTE;
Kasema ana mpenzi, na pia kakiri kunipenda, Ila anataka nimpe cha kumwambia huyo mpenzi wake wa sasa, ili aweze kuachana naye.

Ushauri Wakuu.
 
Wewe mhonge tu hela nyingi.
maneno ya kumwambia bwana ake atayafahamu tu. ili aachane nae
Asante kwa ushauri Mkuu,Hela anazo sasa, au niendelee kujiweka kwa ukaribu na kumjali ili hayo maneno ya kumwambia Huyo jamaa ayapate yeye mwenyewe!

Coz anataka "Eti atamwambiaje huyo jamaa aliye naye"

Ngachoka mie
 
mnunulie basi hata ka helicopter kama ka gwajima. angalau muwe mnapaa angani. huku ukimfundisha maneno ya kumwambia. na wewe ,hata hujiongezi
 
Na wewe akimpata wa kumwambia la kukuambia ujue na wewe atakuacha tuu....

Mwanamke ambaye hana msimamo sio kabisaa
Duuuuuh! Anachoniuliza ni kwa nini Siku zote hizo sikumwambia huo mtongozo!

Hadi leo ana mtu,na anasema afanyaje sasa! Amwambiaje huyo mtu?
 
fanya kama shareholder tuu ili ummiliki vizuri uwe na share nyingi kuliko mwenzako haya mambo yakumjibu sio wewe tena ni yeye tu automatic atafanya
Sawa Kiongozi, Nimekupata sana
 
fanya kama shareholder tuu ili ummiliki vizuri uwe na share nyingi kuliko mwenzako haya mambo yakumjibu sio wewe tena ni yeye tu automatic atafanya
Ila naona huyu Msichana ni muoga, sio mzoefu wa Haya mambo.
Ndo maana anajiuliza afanyeje!
 
Back
Top Bottom