Mshtuko wa ugaidi, 11 wanaswa Mwanza

Mshtuko wa ugaidi, 11 wanaswa Mwanza

Naomba niulize kwa wa Tanzania maana ya ugaidi tunaelewaje? Maana USA wanasema ni MTU yeyote anayepinga maslahi yao, sasa sisi tunamaanisha nini?
Kukamata vitabu vya kiislam na kofia za jeshi kwa mujibu wa maelezo hapo
 
Ivi ni kweli vijana wawili wanaweza kuwakimbia polisi?kuuwa mumeshauwa lkn ukweli hawakustahiki kuuwawa.jela ipo kwa ajili ya watu kama hao.
uliwahi kuona gaidi anafungwa jela?dawa ya gaidi ni kumuuwa tu.
 
Ni pale utakapo kuta polisi wamechukua silaha story kwaajili ya show off
 
Hivi polisi wanaelewa maana ya ugaidi au wanadhani ni kukutwa na kilipuzi tu? Wanajua ni athari gani zinazoweza kuikumba nchi kwa kutamka msamiati wa "ugaidi"?

Mimi nafikiri, kwa kuwa polisi hawana uelewa kuhusu mambo ya hujuma za kigaidi, ni bora wangepigwa marufuku kabisa kutamka hilo neno maana linaweza kuathiri hata shughuli za utalii nchini.
Mkuu na mimi nimeuliza swali kama lako maana kila siku wanalitamka sana
 
Kwani kuna silaha sio yakivita?

Mkuu zipo silaha za uwindaji wanyama mfano Rifles 375, 458 na short gun kwaajili ya ndege, zipo za kivita kama SMG, AK 47,
LMG, G3 nk mkuu wangu, na
zipo za self defence kama bastola aina tofauti kama hujui mkono
 
Kweli polisi waangalie lugha mbadala ya kutumia pengine tuendako inaweza kutugharimu, huku tukihubiri nchi yetu ya amani, mungu tuepushe na hao wachafu hao.
 
Nlijua hizi sinema zilikua 2015 kumbe hawa nao wanacheza comedy zao kma siro,unatupiana risasi vikindu ucku kucha halafu asubuhi unasema umekamata wamama n watoto kwenye hiyo nyumba.inamaa hizo risasi zilikua zinapigwa n majini mana hata bunduki moja hamkukuta,kweli siasa zinawapeleka kubaya
 
Mkuu zipo silaha za uwindaji wanyama mfano Rifles 375, 458 na short gun kwaajili ya ndege, zipo za kivita kama SMG, AK 47,
LMG, G3 nk mkuu wangu, na
zipo za self defence kama bastola aina tofauti kama hujui mkono
mkuu asante kwa ufafanuzi wako makini
 
JESHI la Polisi mkoani Mwanza, linawashikilia watu 15 wakiwemo watoto 11 wenye umri wa miaka 10 wakidaiwa kufundishwa ‘ugaidi’ katika nyumba moja iliopo Kishiri nje kidogo ya jiji hilo,

Kabla ya kufika kwenye nyumba waliyokuwemo watuhumiwa, polisi walimkamata kijana mmoja kwenye Kata ya Kishiri, Wilaya ya Nyamagana ambaye alidaiwa kuhusika.

Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi, Ahmed Msangi amethibitisha kukamatwa kwa watu hao na kueleza kuwa, walifanikiwa kuwakamata baada ya taarifa kutoka kwa kijana huyo.

Msangi ameeleza kuwa, baada ya taarifa za kijana huyo ambaye aliyeongozana na polisi hadi katika eneo la tukio, waliwakuta watuhumiwa hao.

Amesema, watuhumiwa hao baada ya kugundua kuwa ni polisi, walirusha bomu moja jambo ambalo liliwasukuma polisi kuanza kujibu mashambulizi kwa kupiga risasi hewani na kuwamuru kujisalimisha.

Kamanda Msangi amedai kuwa, baada ya watu hao kujisalimisha, polisi walianza kufanya ukaguzi katika nyumba hiyo na kufanikiwa kukuta bunduki aina ya SMG na magazine tano zilizokuwa na risasi 150.

Ameeleza kuwa, polisi pia walifanikiwa kukamata vitabu viwili vya Dini ya Kiislamu na kofia moja ya Jeshi la Ulinzi wa Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Na kwamba, kitendo hicho amedai kinashabiana na vitendo vya ugaidi na matukio mengine yaliowahi kufanyika jijini humo.

“Kama mtakuwa mnakumbuka vizuri kuna matukio ambayo yalishawahi kutokea hapa Mwanza yakiwemo ya msikitini watu kuchinjwa, na watu wanaodai inaweza ikawa ndio hao wahusika,” amesema Msangi.

Nachoona hizi taarifa zinajirudia sana maeneo tofauti, labda hao police wameweza kuwenda Zaidi ili kujua lengo la hawa watu? maana wanakamatwa wakiwa na style sawa. Wamefautilia na kujua kama hawa watu wana mtandao mmoja au wako scattered with different missions
 
Kuna kosa linafanyika hapa ,kati ya hao 15 wabakizwe wawili wengine piga risasi kama kazi hiyo mnaogopa fanyeni mpango wa kuni hire nitawasaidia bila tatizo
 
Samahani wakuu sina nia mbaya wala sina ubaguzi wowote wa kidini katika hili ila najiuliza kila wakati nikwanini kila jambo linalohusishwa na ugaidi utakuta dini yangu ya kiislam inahusika?
 
Hizi recruitments zinazofanyika gizani kisirisiri maporini na kwenye majumba ya watu hizi inaelekea kuna watu wanataka kufanya mambo yao na agenda zao hazitofautiani na mambo yanayoendelea huko iraq na syria.....
Mungu atusaidie
 
Mpaka hapo kagera na tetemeko lao na Arusha na TOYO zao, hadithi inaenda kuisha na mwenye akili atakuwa ameshapata ukweli.
 
Back
Top Bottom