Mshtuko: Mloganzila hospital hawana maji

Nahisi mabwawa yamekauka...ila kuna mradi wa kuleta maji kutoka USA wazee wapo huko wanafanya mipango msihofu soon tatizo la maji litakuwa historia.

Hao Wagonjwa kwasasa wawe wavumilivu kesho VP kutoka Washington atakuja na ndoo kadhaa kwenye airforce.
 
LIPIA TANGAZO
 
Siyo kweli,haiwezekani donar country ambayo imetoa msaada kwa Uturuki Hospitali yake muhimu kama hii ikose maji
 
Si muda mrefu tuliambiwa zimetoka billions of shillings kufufua visima vya maji vilivyopo Kigamboni ili kupunguza tatizo la maji mjini Daslama
- MRADI UNAENDELEAJE?
-Umefika hatua gani?
  • Lini tutegemee maji kutoka Kigamboni?
  • Pesa zote za mradi zimeshatolewa?

Huku kwetu huku, maji ya bomba yanakuja kwa zile Bowser! Tunalipa sh 15,000 kwa lita 1,000. Leo ni wiki 2 kamili tangu tumeagiza watuletee, wanasema hakuna maj! Na si kusema labda tunachota ndoo moja moja, la! Anakuja, anamwaga lita 4,000 sehemu nyingine 5,000 anaondoka, lakini hawajaonekana kwa wiki 2.

Kuna mgao, hatujui! Hakuna maji, hatujui! Mvua haijanyesha, sio kweli.

Bilioni 2.3 kwenda Uturuki, zisingetosha kuipa Mloganzila mfumo wa kuvuna maji ya mvua na kuhifadhi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…