Mshindi wa Miss Albino 2016 apatikana

mbere

JF-Expert Member
Mar 5, 2015
6,967
6,462
ZAWADI DOTTO AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA URIMBWENDE YA "MISS ALBINISM 2016"
1.JPG

Mrimbwende Zawadi Dotto (Pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.

Miss Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshiki katika Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.Mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es Salaam.Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.

2.JPG

Wshiriki Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17), Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18), Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.

3.JPG

Washiriki walioingia Nne bora ambapo kutoka kushoto Hajra Sadru, Furaha Edward, Zabibu Abdallah na Zawadi Dotto

4.JPG

Baada ya Mtifuano mkali hatimae majaji wakatangaza washini. Furaha Edward mshindi wa tatu (Kushoto), Hajru Sadru mshindi wa pili (katikati) na Zawadi Dotto akaibuka kuwa mshindi wa Kwanza (aliepiga magoti).

5.JPG

Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.

6.JPG

7.JPG

Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu

8.JPG

Kampuni ya Visimbuzi (Ving'amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick Makonya ambae ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja zawadi zilizotolewa kwa washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa Kwanza amejinyakulia Simu ya StarTimes aina ya Solar5, Mshindi wa Pili simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.

9.JPG

Baadhi ya Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi.

10.JPG

Alexander Exaud Mutowo ambae ni Mratibu wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION lililoandaa mashindano hayo akizungumza wakati wa mashindano hayo, ambapo amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwemo kuunga mkono juhudi za shirika hilo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jiko katika katika kituo cha kuwahifadhi watu wenye ulemavu wa ngozi Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga.

11.JPG

Fredy Samwel Kaula ambae ni Mwenyekiti wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION akizungumza katika Mashindano hayo

12.JPG

Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS akizungumza wakati wa mashindano hayo

13.JPG

Mwenye kinasa sauti ni Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, akifungua mashindano hayo.

14.JPG

Amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza itaendeleza ushirikiano na Shirika la VUNERABLE FOUNDATION kwa ajili ya kupata wadau wa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi.
Dickson Kiringo a.k.a Mr.White ambae ni Msanii chipukizi wa Muziki wa Kizazi kipya akitoa burudani. Msanii Barnaba Boy aliahidi kumsaidia Mr.White ili arekodi nyimbo mbili katika studio yake ikiwa ni bure kabisa.

15.JPG

Msanii Barnaba Boy akitoa burudani katika shindano la Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.

16.JPG

Majaji ambapo kutoka Kushoto ni Jaji Angelina Chuma, Jaji Mkuu Jalia Mtani na Jaji Lilian Lambo

17.JPG

Wa pili kulia ni Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS pamoja na wadu wengine wakifuatilia mashindano hayo

18.JPG

(Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa BINAGI MEDIA GROUP)
 
Hivi yule mtoto Pendo albino aliyepotea huko Mwanza imekuwaje? Au ndie aliyetolewa kafara kufanikisha ushindi, wetu , kuingia mahali patakatifu.
 
Labda ni mimi tu....., lakini naona hii ina walakini ningependelea zaidi kama ni Miss basi hata hawa wangeenda tu kwenye mashindano ya Miss wengine kama kawaida, kuanza kutenga features fulani kwamba ndio kigezo cha kushiriki........sioni kama inapendeza (unless sijaelewa)
 
Mawazo yako ni kama yangu. Kuna juhudi kubwa zinazofanywa kitaifa na kimataifa ili kuondoa stigma kwa watu wenye ulemavu wa ngozi na badala yake waonekane ni sawa na watu wengine. Sasa hii ya kuandaa shindano kama hili ambalo washiriki wake ni wale tu wenye albinism linawafanya waonekane kama vile wao wenyewe tayari wanajibagua na hivyo kujenga ufa kwenye juhudi zilizopo za kuleta usawa.
 
Labda ni mimi tu....., lakini naona hii ina walakini ningependelea zaidi kama ni Miss basi hata hawa wangeenda tu kwenye mashindano ya Miss wengine kama kawaida, kuanza kutenga features fulani kwamba ndio kigezo cha kushiriki........sioni kama inapendeza (unless sijaelewa)
nimekuelewa sana mkuu japo kwa wengine hawatokuelewa. Kwa hili wamejinyanyapaa kwa kujitenga wenyewe wakiamini kuwa wao hawawezi na hawako sawa na watu wengine. Ingeanzishwa kampeni kuhamasisha albino pia washiriki kwenye mashindano mengine hapo pangekua na usawa na wangeweza kuonyesha vipaji na uwezo walionao
 
Labda ni mimi tu....., lakini naona hii ina walakini ningependelea zaidi kama ni Miss basi hata hawa wangeenda tu kwenye mashindano ya Miss wengine kama kawaida, kuanza kutenga features fulani kwamba ndio kigezo cha kushiriki........sioni kama inapendeza (unless sijaelewa)
Sawa kbsaaa wangejichanganya na mamiss ambao si albino ingekuwa poa zaid lakin hvo ni kama kuwatenga
 
Mbona sijamuona Uncle Lundenga hapo!!????? Ila hawa ndugu zetu wenye albinism huwa wana mvuto sana.
 
Hii hata mimi naona haiko sawa mana tunahangaika kuweka Usawa lakin naona wanajaribu kujitenga, hawa wadada wana sifa zote za kuwania miss Tanzania ya kawaida kabisa
 
Halafu unaweza kuamini eti zawadi kwa washindi wa kwanza, pili na tatu ilikuwa ni Tshs. 100,000/=, 80,000/= na godoro? This is improbable!
 
ZAWADI DOTTO AIBUKA MSHINDI WA MASHINDANO YA URIMBWENDE YA "MISS ALBINISM 2016"
1.JPG

Mrimbwende Zawadi Dotto (Pichani) ameibuka kidedea katika Mashindano ya Miss Albinism Kanda ya Ziwa yaliyofanyika usiku wa Kuamkia leo Jijini Mwanza.

Miss Zawadi mwenye umri wa miaka 17 (mwanafunzi) ameibuka mshiki katika Mashindano hayo ambayo ni maalumu kwa ajili ya Watu wenye ulemavu wa ngozi kwa ajili kuonyesha umahiri wao katika tasnia ya urimbwene hii ikiwa pia ni ishara ya kwamba watu wenye ulemavu wa ngozi wanaweza kushiriki katika shughuli na mashindano mbalimbali.Mashindano hayo yanaandaliwa na Taasisi ya kusaidia Watu wanaoishi katika Mazingira hatarishi iitwayo SAVE VUNERABLE FOUNDATION ya Jijini Dar es Salaam.Mratibu wa Shirika hilo Alexander Exaud Mutowo ametanabaisha kwamba, baada ya mashindano hayo kukamilika kwa kanda zote nchini, Washindi wa Kanda hizo watashindanishwa Jijini Dar es salaam ili kumpata Mshindi wa Kitaifa wa MISS ALBINISM 2016.

2.JPG

Wshiriki Saba wa Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa na umri wao katika mabano ambapo kutoka Kushoto ni Hajra Sadru (22), Antonia Mathias William (17), Furaha Edward John (17), Pendo Faustine (15), Zabibu Abdallah (18), Zawadi Dotto (17) pamoja na Asteria Christopher.

3.JPG

Washiriki walioingia Nne bora ambapo kutoka kushoto Hajra Sadru, Furaha Edward, Zabibu Abdallah na Zawadi Dotto

4.JPG

Baada ya Mtifuano mkali hatimae majaji wakatangaza washini. Furaha Edward mshindi wa tatu (Kushoto), Hajru Sadru mshindi wa pili (katikati) na Zawadi Dotto akaibuka kuwa mshindi wa Kwanza (aliepiga magoti).

5.JPG

Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.

6.JPG

Mshindi wa Miss Albinism Kanda ya Ziwa akivikwa taji lake. Wa pili kulia ni Jalia Mtani ambae alikuwa Jaji Mkuu akitajana Majina ya washindi. Pembeni ni Mshereheshaji Emmanuel Shalali kutoka Sahara Media Group.

7.JPG

Katikati ni Mshindi wa Kwanza, Kulia Mshindi wa Pili na Kushoto Mshindi wa Tatu

8.JPG

Kampuni ya Visimbuzi (Ving'amuzi) ya StarTimes ilikuwa miongoni mwa makampuni yaliyosaidia kufanikisha mashindano hayo. Mwenye Kinasa sauti ni Erick Makonya ambae ni Afisa Masoko wa Kampuni hiyo Kanda ya Ziwa akitaja zawadi zilizotolewa kwa washindi na Kampuni hiyo ambapo Mshindi wa Kwanza amejinyakulia Simu ya StarTimes aina ya Solar5, Mshindi wa Pili simu aina ya P40 StarTimes na Mshindi wa tatu amejishindia simu aina ya B27 zote zikiwa ni android kutoka StarTimes.

9.JPG

Baadhi ya Wageni waalikwa wakiongozwa na Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, wakiwa katika picha ya Pamoja na washindi.

10.JPG

Alexander Exaud Mutowo ambae ni Mratibu wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION lililoandaa mashindano hayo akizungumza wakati wa mashindano hayo, ambapo amewasihi wadau mbalimbali kujitokeza kusaidia utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi ikiwemo kuunga mkono juhudi za shirika hilo kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa jiko katika katika kituo cha kuwahifadhi watu wenye ulemavu wa ngozi Buhangija kilichopo Mkoani Shinyanga.

11.JPG

Fredy Samwel Kaula ambae ni Mwenyekiti wa Shirika la VUNERABLE FOUNDATION akizungumza katika Mashindano hayo

12.JPG

Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS akizungumza wakati wa mashindano hayo

13.JPG

Mwenye kinasa sauti ni Marcella Mayala ambae ni Katibu Tawala Wilaya ya Nyamagana (wa tatu kushoto) ambae alimwakilisha wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Magesa Mulongo ambae alikuwa Mgeni Rasmi, akifungua mashindano hayo.

14.JPG

Amesema ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza itaendeleza ushirikiano na Shirika la VUNERABLE FOUNDATION kwa ajili ya kupata wadau wa kusaidia kutatua changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi.
Dickson Kiringo a.k.a Mr.White ambae ni Msanii chipukizi wa Muziki wa Kizazi kipya akitoa burudani. Msanii Barnaba Boy aliahidi kumsaidia Mr.White ili arekodi nyimbo mbili katika studio yake ikiwa ni bure kabisa.

15.JPG

Msanii Barnaba Boy akitoa burudani katika shindano la Miss Albinism 2016 Kanda ya Ziwa Jijini Mwanza.

16.JPG

Majaji ambapo kutoka Kushoto ni Jaji Angelina Chuma, Jaji Mkuu Jalia Mtani na Jaji Lilian Lambo

17.JPG

Wa pili kulia ni Alfredy Kapole ambae ni Mwenyekiti wa Tanzania Albinism Sociaty TAS pamoja na wadu wengine wakifuatilia mashindano hayo

18.JPG

(Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo wa BINAGI MEDIA GROUP)
"nimefurahishwa sana.. kuona hawa watu wanaonyeshwa kuthaminiwa" god luv all of us
 
Back
Top Bottom