NIMPENDENANI
JF-Expert Member
- Nov 2, 2014
- 6,114
- 5,398
Yani ameitupa bahati kwa ujinga wake,anasema yuko tayari hata kua mke wa pili,sijui dunia hii wanao taka mke wa pili wachache sana...Msamaha upi tena? Hakuna cha ku-rewind hapo ndio imetoka tena. Akamsaidie jamaa kukodisha baiskeli kule Tanga.
Nimeshanga sana kwa uwamuzi wake wa ghafla bin vuu,nilitarajia atasubiri mpaka mwamakani halafu baya zaidi amemtumia rafiki yake hela ya kuongezea mtaji wake wa baiskeli sasa sijui anamtukana au nini mpaka sasa sijaelewa maana yake na ameshajua kilichotokea...''ipo siku utajua thamani yangu lakini nasikitika kwa sababu utakuwa umechelewa"
hahahaha..............hii meseji inamuhusu huyo mhusika, kwa sababu saa zingine tunapowaambia Watoto wa kike mna mapepo huwa hamtuelewi....Yani nampa Big up Mshikaji kwa 100%, hata mimi ningefanya vile, yani Ukishakuwa msomi
humaanisha unafanya vitu kwa tathmini ya muda, raslimali na faida. Yani huyo jamaa yupo Bright na nampongeza sana, Mimi ninavyoamini Mwanaume alikwenda shule akajitambua huwa hana mambo ya kurudi nyuma...Dada akate kushoto..
Hyu mdada hajarogwa ulimbukeni ndio ulikua unamsumbua tuu..Tanga bana ha ha ha ha ha ha wanaroga hadi mapenzi
Atawacha kula tena wakati yeye ndio anamwambia bi dada sema unataka gari sema unataka mfanya kazi atakupa sema unataka pesa manake jamaa ----....Jee huyo mshenga alimla "TUMBUA" bi dada?
Alijisahau sana yule alidhani sijui hakuna wakuchukua nafasi yake,anarudi sasaivi Yawapi mashi?Mtu ukijipenda na kujistaajabia sana ndiyo unapoteza hadhi yako !!!!
Ala kuli hali !! hiyo inaitwa "Nasibu" Hongera kwa mdogo wetu.... Na kila mtu atakula rizik aloandikiwa!!Alijisahau sana yule alidhani sijui hakuna wakuchukua nafasi yake,anarudi sasaivi Yawapi mashi?
Hii maada kwa namna moja inaibua swali la msingi. Mshenga awe na sifa zipi? Je bachelor anafaa kuwa mshenga?
Kosa analo mdogo wako,mshenga huwa anatumwa kwa wazazi wa muolewa/binti na si kwa binti mwenyewe.Habari za Asubuhi wanna MMU,
Nna Mdogo wangu wakiume anaishi nje alikuja likizo akakutana na mdada hatimae wanataka kufunga ndoa
tatizo limekuja pale rafiki yake mdogo wangu ambae ndio mshenga kuchelewa kuleta jibu,kama tumekubaliwa
au tumekataliwa,barua imepelekwa tangu dec 2014 na tulipanga harusi ifanyike jul wakati sote tukiwa likizo
chakushangaza huyu biharusi mtarajiwa akaanza demand ooh mie ukinioa unichukue tuondoke sote,sawa,
ooh nataka mfanya kazi, oh nataka niendeshe gari,wakati hata kuwasha gari hajui..
Mwezi wa 2 mwaka huu mdogo wangu amekuja TZ baada ya 1week majibu yakaletwa kua anaolewa basi
mkaka akatafuta mke mwengine hakusubiri nini wala nini kachukua mkewe wako majuu,huyu mdada sasa jana usiku
kaja na kilio anataka kuolewa na kaka,ilibidi tushangae tukamwambia kua unajua kua ameoa na yuko Happy na mkewe
kasema mie hata mke wa pili sinaneno,yule mshenga ndio alinambia atanioa kaniroga nilikua sijielewi zungumzeni na mdogo wenu manake hata cm pia amebadili,mie nimeshanga ivi inakuwaje mtu unakosa haya kiasi hiki?
mshenga hata nyumbani hapiti karudi Tanga kwenye kazi yake yakukodosha baiskeli..
Je nisawa akiombewa msamaha huyu mdada?
Asante lakini ZZ unajua kuna kitu mpaka sasa nashindwa kuelewa yani huyu mdogo wangu juu yakua kasikia alivyofanya rafiki yake lakini still amempa hela M1 ya mtaji sasa sielewi nikwanini...Ala kuli hali !! hiyo inaitwa "Nasibu" Hongera kwa mdogo wetu.... Na kila mtu atakula rizik aloandikiwa!!
huyo mshenga nimkubwa ki umri na ameshaoa ila mkewe anaishi nae kwao yani nyumba ya Babake, mzee wetu haishi TZ na yeye ni family friend tunamchukua kama kaka mkubwa,haya ndio amesha soma.....na walobaki wanasema tutapeleka wenyewe mahari hatutaki mshenga..Kosa analo mdogo wako,mshenga huwa anatumwa kwa wazazi wa muolewa/binti na si kwa binti mwenyewe.
Na unamtumaje kijana mwenzio kuwa mshenga,hili ni fundisho kwa mabinti na vijana wote ambao hawajaolewa/kuoa.
Ushauri wangu wala msipoteze muda kuwasiliana na mdogo wenu,yeye kaishaoa basi.
huyu aliyejiaribia aanze upya wachumba bado wanapatikana.