MSHANGAO: Kura za CCM zimetoka wapi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MSHANGAO: Kura za CCM zimetoka wapi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Uswe, Nov 3, 2010.

 1. U

  Uswe JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  nikiangalia katika mitandao ya kijamii, nikisiliza redio na vyombo vingine vya habari watu wengi wamechoshwa na ccm, utafiti wangu unaonyesha wanaoendelea kuikumbatia ccm ni watu wanaonufaika moja kwa moja na ccm, watoto, ndugu au marafiki wa viongozi na wafanyakazi wa vyombo ambavyo wamiliki wake wanafaidika na ccm, mbali na hapo hakuna watu neutral wanaopenda ccm, sasa nachoshangaa hivi kura zinazosomwa na tume zimepatikana wapi?
   
 2. S

  Silas A.K JF-Expert Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 807
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Miujiza hiyo ndugu yangu,demokrasia hakuna Tanzania.watu wanataka waje na hadithi za kiswahili kwamba walishinda kwa kishindo. wakumbuke tu kwamba umma wa watanzania unaelewa uhuni unaofanyika lakini wanapenda amani iliyopo iendelee kutawala la sivyo tungesikia na kushuhudia mengine
   
 3. MADAM T

  MADAM T JF-Expert Member

  #3
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 3,660
  Likes Received: 940
  Trophy Points: 280
  Hilo naona halikushangazi peke yako hata mimi siamini kama watanzania ni wehu kiasi hiki eti achaguliwe kwa kura zote hizo, huu ni wizi tu!!!!!!:A S angry:
   
 4. s

  shababi Member

  #4
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 10, 2009
  Messages: 15
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nakuunga mkono ndugu yangu uliyetangulia. tuombe Mungu wapatikane wabunge wengi toka upinzani ili washirikiane kuandaa mazingira mazuri 2015. dat will be the death of ccm
   
 5. SUZANE

  SUZANE JF-Expert Member

  #5
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 740
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 45
  Unashangaa nini ss? kwani hujui CCM ni wachakachuaji mahiri?
   
 6. Gosheni

  Gosheni Senior Member

  #6
  Nov 3, 2010
  Joined: Oct 28, 2008
  Messages: 188
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 60
  hivi unashanga nini?mbona kila kitu kipo wazi kinachoendela.wanatumia nguvu za ziada kuiba,hii sio kuiba bali ni kupola(kuchukua kwa lazima).angalia mfano kinachoendelea segerea,ukonga.demeokrasia imebakwa kibaha,kigoma mjini,shy mjini,tarime,busanda,geita mjini,mby vijijini,mbozi mashariki.kote huku ccm imeshindwa ila wametumia kuiba huku mwenye mali anaona,hana cha kufanya kwa kuwa amezidiwa nguvu(ni sawa na jambazi anapo kuingilia usiku akiwa na bunduki,hapo hufanya chochote ananchotaka).tunashukuru Mungu ht kwa tulichopata.iwapo uongozi wa chadema wakaishi kwa amani kwa miaka5 hii,ccm baibai 2015.
   
 7. P

  Pattie Member

  #7
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hawa mwaka huu lazima tuwashitaki kwenye mahakama ya kimataifa
   
 8. M

  Mundu JF-Expert Member

  #8
  Nov 3, 2010
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  ...na sasa hivi tumeona mwanga. Tunawaombea uzima viongozi wote wa upinzani waliochaguliwa; ambao CCM imeona haya kuiba kura zao.Tunawaombea heri na baraka katika kazi yao.

  Kitu cha kwanza watakapoingia mjengoni ni kudai na kushinikiza uwepo wa TUME huru ya uchaguzi. Kama Zanzibar uliweza kupatikana muafaka, inshallah na hili litafanikiwa Tanzania Bara.

  Vyombo vya habari, taasisi huru za kiraia lazima ziandike kuhusu kuwepo kwa tume huru, hadi haki ipatikane. Kwakuwa huu mfumo ni wa vyama vingi, haiwezekani hata kidogo viongozi wa tume na taasisi nzima, kuwajibika kwa serikali.

  Na wale wananchi wenzangu na mimi ambao pamoja na ku enjoy machungu ya maisha magumu yanayosababishwa na serikali ya mabavu ya CCM; lakini hawaoni mfano wa wenzao ambao wameamua kusema sasa basi, nawatakia mateso mema. Hongereni Ubungo, Kawe, Kigoma kaskazini, Hai, Rombo, Arusha mjini na kweingineko, mliotutoa kimasomaso watanzania.

  Naungana mkono na mchangiaji mmoja hapo juu kwa kuwatafadhalisha wabunge wa CCM, wafanye kazi kwa maslahi ya watanzania. watambue kwamba 2015 si mbali.

  Tanzania bila Kikwete na mafisadi wenzake na CCM yao inawezekana.
   
 9. eucalyptos

  eucalyptos JF-Expert Member

  #9
  Nov 3, 2010
  Joined: Jan 23, 2010
  Messages: 381
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Zimetoka kwenye UCHAKACHUAJI.

  Hakuna anayeweza kupinga kuwa 80% inatafutwa hapo.

  Siku moja tu kabla ya uchaguzi, masaa ya jioni nilipanda daladala lililotokea Kariakoo, siku hiyo ndio chama cha jembe na nyundo kilikuwa kinafunga kampeni hapo Jangwani.
  Mtu mmoja akatamka tu "pamoja na yote mwaka huu sisiem itashinda" (hapo tupo ndani ya basi). Baada tu ya kauli hiyo moto uliwaka; "acha ujinga, unadhani sisi waTZ wajinga sana eeh?"... Walizungumza watu utadhani jamaa kawaambia anawapeleka jehanamu. Mimi nilikaa kimya kabisa nikitaka kujua waTZ wana hali gani kisiasa.
  Pamoja na mengi waliyozungumza kabla sijashuka na kuacha mjadala mkali ni; SISI TUMECHOKA SANA, SISI HATUDANGANYWI TENA, HATUWEZI KUPELEKESHWA NK.
  Kwa kundi hili dogo la watu kati ya 25-30 ambalo kila m2 ana yake anasema na kuona "mafisadi hawafai" halafu uniambie "tunaongoza"?

  Kwa kifupi ninachotaka kusema ni; USHINDI WA jembe na nyundo NI WA KUPIKA. Some things must be wrong. Hata kama wapo wanaopinga na kukataa, watajua tu siku moja kuwa "upandacho ndicho utakachovuna".

  Ni kweli waTZ wazalendo seem to be "very weak" and can do nothing even in demanding their "rights" but GOD WHO CREATED TZ & THE PEOPLE WILL FIGHT 4 THEM.
   
 10. rugumye

  rugumye JF-Expert Member

  #10
  Nov 3, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 561
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tusubiri vita tu hapa Tanzania si salama tena kwa mchezo huu, kwaani kinachofanywa na police na huyu wakara wa CCM NEC hatuwezi kuvumilia miaka yote, imefika wakati watu kusema basi nguvu ya umma ifanye kazi. sure i tell you siku zinakuja, hatuwezi kuendelea kuwasikiliza huku wakiendelea kunywa mvinyo na nyama huku watanzania tukitaabika. for sure NO.
   
 11. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #11
  Nov 3, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Haiwezekani JK amzidi kura Slaa Hai, yaani ni sawa sawa na sisimizi kumpa mimba tembo
   
Loading...