Ungenielewa hata usingeandika yote haya..mimi naweza kuwa mshamba machoni pako in case si-meet standards zako za ujanja na wewe vivyo hivyo..sasa kuna collective standards ambazo zinalubalika na majority katika jamii..sasa sijui unataka tubishane nini!? We msukuma nini?
Inamaana wasukuma ndo wabishi kuliko makabila yote unayoyafahamu?
Mi kabila yangu Mtanzania.
Kama wewe na kabila lako mnajiona wajanja kuliko makabila yote, basi kuna shida. Kabila hiyo ni ya kuogopa sana ktk nchi hii.
Naona bado unasumbuliwa na roho ya ukabila ndo maana.
Unataka kutambika? [emoji15] [emoji15] [emoji15] [emoji28] [emoji28] [emoji28]
Hivi kuingia Hotel ya kitalii ukiwa umevaa kandambili miguuni ni ushamba au ujanja?
Kuvaa mtepesho hadi nguo ya ndani inaonekana ni ushamba au ujanja?
Kwa mwanamke kuvaa nguo inayooneshe viungo vyake (mapaja na matiti) ni ushamba au ujanja?
Kuendesha pikipiki ukiwa umetundika helmet kwenye usukani wa pikipiki badala ya kuivaa kichwani ni ushamba au ujanja?
Mwenyeji wa eneo fulani kumdanganya njia mgeni ni ushamba au ujanja?
Baada ya kujibu maswali hayo unadhani kuna uhusiano wowote kati ya mambo hayo na makabila?