Mshahara wa Wabunge upunguzwe

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,944
3,820
kama utapiga mahesabu na kujua ni kiasi gani wabunge wanatek home hela,basi utaona kwa nini serikali inaingia kwenye ufukara kiasi ya kuleta na kujaza kero kwa mwananchi asie hata na kazi ya maana ,pengine hata akilima mazao yanakauka na jua au kuoza kwa sababu ya mvua zisizo isha,na wakati mwengine hata mazao yake yanakosa soko.

Ukweli serikali inapoteza hela nyingi sana kuwalipa wabunge tuseme ni inafanya kufuru., Ubunge ni kazi ya kujitolea kuwawakilisha wananchi katika maamuzi ya nchi na sio iwe mrija na baa la kuwanyonya wananchi kwa utungaji wa sheria kandamizi.

Kila nikifikiria hata siwezi kujua yaani imekuwa kama siri idadi ya hela wanazosanya kwa mwezi tu wachilia mbali hesabu za kila mwaka au baada ya miaka mitano na wengine wanazeekea hapo hapo na kufika hadi kujukuu.

Kama haitoshi wabunge hao huwa na biashara zao majumba yao mashamba makubwa makubwa na maekari yanayogeuka misitu,

Kwa nini hawa wabunge wasiekewe kiwango cha mshahara kisichozidi laki tano ?? na Akiungaunga na vimirija vya hapo bungeni anatimiza japo milioni moja na nusu au mbili.

Hakuna anaelazimishwa kuwa mbunge na wapo wengi wanaweza kujitolea katika kuutumikia wananchi kwa ujira mdogo sana wapo wengi tena watu na elimu zao,leo bungeni kumejaa makanjanja kupiga meza na kushangilia ujinga,na mabishano ya kitoto sana maana ni kama unaangalia comedi,kwa kiwango flani inafurahisha kuangalia bunge umkute Bwege pale ,anachekesha hadi Pilato anajisahau kwa kucheka.

maoni yangu naona ipo haja ya kuupunguza mshahara wa mbunge na uwekwe wazi kwamba unagombea ubunge mshahara ni huu tena umeounguzwa halafu uwe usiopitiliza mipaka kiasi ya watu kuuwana kutafuta nafasi ya kuwa mbunge,ni hatari.
 
Back
Top Bottom