Mshahara wa TShs 900,000 hautoshi kabisa

Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu na amfanyaye mwanadamu kuwa kinga yake. Na moyoni amemwacha Mungu. Maana atakuwa kama fukara nyikani. Hataona yanapotokea mema. Baali atakaa jangwani palipo ukame,katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Wala hatazaa matunda. Mungu peke yake ndio ana uwezo wa kukutunza. hata upewe milioni kumi au ishirini hazitatosha. Mwanadamu haridhiki, kwasababu ameumbwa amtegemee Mungu. Mshahara haujawahi kutosha. jipangeni kumtegemea Mungu sio serikali haiwezi kuwalipa. Tafakari haya kwa makini
 
Hiyo hata mm nawaunga mkono mm ni just electrical technician sina hata kadiploma lkn mwisho wa mwezi nitakunja lk 8 yangu baada ya mkato na trh 15 ninakunja kaallowance kangu ka lk 250. Naunga mkono madai yenu
 
Ni kweli mshahara wa madaktari uko kwenye higher side. Kwa mgomo huu, wameingia choo chaka. Hawakustahili kugoma. Hawajasoma alama za nyakati.
 

Hakuna ugomvi wowote muajiri wako hana uwezo wa kukulipa huo mshahara unaoutaka...kwa hiyo mkilipwa 7,700,000 nchi ndio itakuwa tajiri? Hamna lolote eti mnasema mnawatetea wanyonge wakati kwenye madai 12 dai 1 tu ndio mmeomba vifaa vya kufanyia kazi madai yote 11 maslahi yenu binafsi...nendeni Ulaya au Amerika nasikia wanalipa vizuri.
 

Hongera sana mkuu huo ndio wito tunaohitaji kuridhika na mshahara unaopewa, kuna Dr mmoja nilipeleka mgonjwa wangu akaniomba rushwa nikasema sina hela akaniambia sasa mbona umeniletea maiti? Na kweli nilikaa masaa 2 bila mgonjwa kuhudumiwa mpaka anafariki. Hawa madr wa mishahara bora wafukuzwe tu maana hawana msaada kwa wananchi wa kawaida, wakatafute kazi nje ya nchi kwetu hawatufai kabisa maana kama huna kitu kidogo ndio unazikwa hata kwa ugonjwa mdogo.
 
Mkuu, Mshahara wa sh 955,000/- ikishakatwa PPF na PAYE inabaki Sh. 720,000/- na sio Laki tano na nusu.
Kimsingi sikubaliani na Mbunge kulipwa 10,000,000/- kwa wiki4 alafu daktari analipwa asilimia 10% ya mshahara wa mbunge.

Mwalimu je anayelibwa 469,000 akikatwa PSPF, PAYE, HESLB, NHIF, CWT anadaka 324,000 mnategemea nini? Tuzinduke!
 

10,000,000 za Wabunge zinatoka wapi?
 
rais wa tano dhaifu
 

hii kali nimecheka sana.!
 
Hivi kati ya Dr na Polisi nani wanafanya kazi kwenye mazingira magumu na hatarishi?
 
HUYO NI DAKTARI AU NURSE....JAMANI SERIKALI IACHE UTANI.

Supervisor wa hoteli, mwenye elimu ya kidato cha sita au Co-ordinator analipwa zaidi ya hiyo hela 750,000/=-1,500,000/= kwa mwezi, analipwa malipo ya huduma (service charge), hii ni kutegemeana na uzo au pato la mwezi la kampuni husika na asilimia walizokubaliana.

Anasaidiwa kupata mkopo tena usiozidi riba ya 22%.

Anapewa chakula, usafiri, hata kama matibabu ni kupitia BIMA ya afya, bado huyu mtu ana amani na kazi yake. Anapatiwa usafiri wa kwenda na kurudi nyumbani pindi awapo kazini. Analipwa malipo ya ziada (Over time).

Mwajiri anachangia katika akaunti yake ya malipo ya uzeeni, hata kama atayachukua kabla ya huo uzee. 10% mwajiri, 10%yeye=20% inaingia katika mfuko wa pensheni. (eg PPF, LAPF,NSSF etc).

Hainiingii akilini kabisa kusikia Daktari...jamani si mmesema Daktari aliyesomea kazi yake(simaanishi hawa wauguzi wa kawaida) Huyu Dr awe na shahada ya uzamili (Masters) au uzamivu (Ph.D) yaani 900,000/=? sikufanikiwa kusikiliza hotuba ya Mhe.Rais lakini nitaipata hard copy yake, nitumieni jamani wapendwa.

Swali kwa wenye weledi wa mifuko ya pesheni......Je kuna riba yeyote au nyongeza kwenye hayo makato pindi wanapostaafu?

Namkumbuka mzee wangu Festus Mogae Aliyekuwa rais wa Botswana), yule mwanaharakati wa masuala ya ukimwi, pamoja na Jerry Rowlings ( Rais wa zamani wa Ghana)hawa wote waliboresha malipo na maslahi katika nyanja hizi ( Hospitals, madaktari wanalipwa hela ya kutosha, Ma-Engineers, na Walimu bila kujali)utaratibu huo haujabadilika bado uko palepale.

Kwanini rais asijifunze kwa John Atta Mills wa Ghana leo? au Rafiki yake Ian Khama Seretse Khama wa Botswana leo?

"BADO SIPATI PICHA" :A S-confused1:
 
Wamelupiwa na serikali hizo shule .matatizo ya elimu ya bure

Tatizo waTanzania mnapenda sana kudanganywa na hamtaki kutumia hata chembe ya ubongo wenu kuchambua ukweli na uwongo. Ni juzi tu HELSB wametangaza kuchukulia hatua za kisheria watu waliopewa mkopo wa elimu ya juu na hawalipi..katika ile list kuna maDaktari zaidi ya 500 wanadaiwa...mimi huu ni mwaka wa 4 nakatwa kila mwezi Tshs 57,000/= kulipia mkopo wangu wa elimu ya juu (uDaktari).....halafu Rais anatangaza bila ya aibu kwenye televeision ya Taifa kuwa tumesoma bure?! Tunalipa kwa nini sasa kama tulisomeshwa bure?!
 
Si Ameshasema waende huko kwenye mishara ya mamillioni sasa tabu ikwapi hapa?
 
HAPO NI Mil 1.050.000/= sasa mimi nikisema 900,000/=haitoshi hawanielewi kabisa...jameni hiyo haitoshi kabisa.....

WAHANDISI
MADAKTARI
WAALIMU

Hata rais naye kafundishwa na MWALIMU, Anatibiwa na DAKTARI, kwa upande wa WAHANDISI amuulize Magufuli kwani si wako karibu hata kama hana fani hiyo lakini ana uzoefu na hilo. MNAMKUMBUKA MTOTO SALMA WA KIGAMBONI ENZI ZILE? INGAWA LEO NI MTU MZIMA KAMA SIKOSEI KANA ANAKUA. (KIPINDI CHA RADIO ONE WATOTO-CHEI CHEI SHANGAZI) KWA WANAOKUMBUKA WATANIELEWA NA WATAJUA UMUHIMU WA MADAKTARI NA WAALIMU.
 
Dr. mi nadhani na nyie mtoe tamko la kukanusha madai ya Rais, Watanzania watawaelewa tu. Mkanushe yote kua hata hiyo M 7 wala haikua lengo lenu ifike hapo
 
Hakuna aliyesoma bure, hata wale waliopewa mkopo wa 20% wanakatwa na wasiofanya kazi wengi wao wameorodheshwa katika huduma za jamii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…