Mshahara wa Rais kaa la moto

Mshahara wa Rais kaa la moto

kiasi cha mshahara kwa rais yeyote duniani hutegemea na malengo halisi ya mgombea yaliyomsukuma kuomba kazi hiyo ! KWA MTU MWAMINIFU KABISA , IKULU NI MZIGO - JK NYERERE .
 
Ndio Mamburula wetu hawa ndani ya Serikali inayothubutu kujiita eti, "Serikali sikivu" sijui huo usikivu ni kwenye lipi hasa.

Huyo Mama ni mburula tu,hata hako kaelimu alikopata hakajamsaidia kitu.,Eti anamwuliza mwandishi 'wewe unaujua mshahara wa Obama?'Sijui hicho kiti amekikalia kwa vigezo gani.
 
Ndio Mamburula wetu hawa ndani ya Serikali inayothubutu kujiita eti, "Serikali sikivu" sijui huo usikivu ni kwenye lipi hasa.

Serikali sikivu katika kusikilizana na kuelewana na waporaji wafilisi nchi kwa pamoja."Ninafikiri ndio serikali pekee duniani inayokaa meza moja na wahujumu uchumi na kuwaomba wapore kwa uangalifu"~ref EPA.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mnashangaa nini. Rais mstaafu Mkapa hapo anapata 80% ya zigo la Rais Kikwete. Kuna Mwinyi. Acha hao, Kuna Sumaye, Lowasa (huyu nae mstaafu??? Hapa nadanganyika), kuna Warioba (Huyu pamoja na kuvuta za Tume anavuta za ustaafu), Kuna Salim (Nae kama warioba), Kuna Malecela, kuna Msuya, nao wanavuta 80% ya Mzee wa piga tu. Hao tu kwa mwaka tuna MRI au CT Scan kila hospital ya mkoa Tanzania.
 
chakula, malazi, matibabu, mavazi, watumishi wa ndani na nje, umeme, maji, usafiri, hivi vyote ni bure, du! ndo maana hata lile wazo la kurudisha nyumba za serikali zilizouzwa lmezikwa.

Mtu unatunzwa namna hii na bado uiachia ngazi unatunzwa maisha, JE HII IKO KATIKA KATIBA MPYA IJAYO? je sawa hiyo?????????
hataaaaa!!! hii lazima imulikwe. Watanzania tumezidi kwa uchoyo, uroho tamaa na ubinafsi. Ndo maana kila mtu anlilia kuwa mkubwa serikalini.
SIASA SAFI na UONGOZI BORA huu!
 
“Siwezi kutaja mshahara wa bosi wangu wala wa kwangu mwenyewe. Wewe unaujua mshahara wa Obama (Rais wa Marekani)?” alihoji tena.

Huyu mama limbukeni.

Mshahara wa Obama unaulikana

Ona President Obama

Tena si mshahara tu, anaripoti mpaka kipato kutoka nje ya mshahara, kama kwa mfano, mauzo ya vitabu vyake.

President Obama and First Lady report roughly $600K in gross income in 2012, down from 2011 - NY Daily News

Naweza kuelewa dhana ya mishahara kuwa siri katika sekta binafsi. Ambako mshahara ni siri ya muajiri na muajiriwa.

Lakini katika serikali, muajiri ni wananchi, kwa hiyo hakuna siri, kwa sababu ukitaka iwe siri kati ya muajiri na muajiriwa, basi mshahara uwe siri kati ya raia wote wa Tanzania na muajiriwa (Rais, Waziri Mkuu etc)

Itakuwaje mshahara uwesiri kati ya muajiri na muajiriwa?

Unaweza kuajiri mtumishi wa nyumbani halafu usijue mshahara wake?
 
Huyo mama eti ndo alikuwa waziri wa sheria na katiba. Naye kwani ni dada msomi aka 'learned sister'? Teh teh teh....kaazi kweli kweli.

Eti 'wewe unaujua mshahara wa Obama'? Haya bana dada msomi. Nilishagachoka mie kuulizia huu mshahara wa rais maana mijitu ni mijinga kupita kiasi.
 
Wasomi wengine are a big let down. Surely nani asiyejua mshahara wa rais US of A, public knowledge tangu karne ya 17.
 
Halafu mods mngeiunganisha tu hii mada na ile mada yangu ya 2007 kuhusu mishahara ya viongozi wa TZ ambayo ipo kule kwenye jukwaa la Intelligence.
Invisible
 
Last edited by a moderator:
Mugabe ni mzalendo saana. Nikiongozi wa ukweli maslahi ya nchi na wananchi yana pews kipaumbele
 
haya mambo hayatabadilika kama CCM itendelea kubaki madarakani.
 
Marais nchi tajiri wanalipwa mishahara midogo kuliko tz kwel huo ubinafsi mkubwa wa viongoz wetu huko huduma za jamii kama matibabu, elimu, maji, usafiri mbaya viongoz wakineemeka kwa mishara minono kodi ya wananchi masikini ambao huduma zao haitakwi kuboresha cku hadi cku. Watz tubadilike nyeupe tuseme nyeupe na nyeusi tuseme nyeusi.
 
Huo ni mshahara tu,Nahisi posho zao zikiwekwa hadharani hatutaamini

Ni mara tatu zaidi ya mshahara.
 
watu mnashangaa mishahara hawa jamaa hata nyama wanapewa bure nenda pale clock tower kwenye duka la nyama la kongwa..... ndio maana ile ranchi ya taifa haijiendeshi kifaid ni gari za STK tu zinapanga foleni pale kubeba nyama za mawaziri na wakubwa wengine.... yaan tumefika huku v8 zinabeba nyama kupeleka majumban mwa viongozi kwa mishahara hii hadi nyama nayo wanapewa bure tena kama siku za sikukuu mtanzania unayetaka kununua kwa cash pale hupati nyama ni oda za ofisi za serikali tu tena hawalipi!!!
 
Kwa utaratibu huu,ccm ikiondoka madarakani kwa hiyari itakuwa ni muujiza wa karne!
 
Sitashangaa kabisa kama hawa walafi wanalipwa posho chungu nzima kila mwezi. " Posho ya kuwa Rais wa Tanzania" labda ni 10% ya huo mshahara kila mwezi.

Huo ni mshahara tu,Nahisi posho zao zikiwekwa hadharani hatutaamini

Ni mara tatu zaidi ya mshahara.
 
Mwalimu akidai nyongeza ya vijihela kidogo tu kwenye mshahara wake ni vita, atatishwa huyo, atasimangwa mpaka basi. Hivi hatuwezi kuliweka hili kwenye muswada wa katiba mpyua jamani?!!
 
Back
Top Bottom