KOKUTONA
JF-Expert Member
- Jan 29, 2011
- 8,651
- 6,109
Rafiki KOKUTONA ndio maana hawataki Watanzania tuijue mishahara yao. Muajiri wao ni Watanzania halafu mishahara wanajipangia waajiriwa tena kwa siri halafu hawataki muajiri wao ajue mishahara waliyojipangia!!!! Wakati huo huo hawataki kuongeza mishahara ya Walimu na Madaktari kwa kisingizio Serikali haina pesa!!! Ila pesa ya kujilipa wenyewe mishahara minene siku zote haikosekani!!! Eti ni kosa kutangaza mshahara wa wanene hadharani!!! Walifungie tena Mwananchi kwa kuvunja sharia ya kuanika mishahara ya wanene hadharani.
Wamekosa utu na huruma kabisa kwa wananchi na walipa kodi. Angalia mishahara yao ilivyo mikubwa na wanaipokea bila aibu kabisa il hali haikatwi kodo lakini bado wanamkandamiza mtumishi ambaye hafikii haata theluthi ya mishahara yao kwa kumkata kodi kubwa eti PAYE, wao PAYE wanakatwa wapi?
Bado wameongeza kodi kibao zisizo na kichwa wala miguu...unajua nini BAK wao machungu hawayasikii sbb kila kitu wanapewa tu hawana machungu yoyote ya kutafuta kwa jasho. Lakini ole nakwambia muda wao utafika watakapoinamisha vichwa vyao kwa aibu. Siku Mungu atakapoamua kusimama na kuanika uovu huu hadaharani.
Last edited by a moderator: