Mshahara wa Mbunge wa mwezi ni Mshahara wa Mwalimu wa Miaka Mitatu

Malipo ya Mbunge sawa na ya mwalimu kwa miaka mitatu
Saturday, 10 December 2011 09:03


Fredy Azzah na Leon Bahati
Mwananchi

WAKATI wabunge wakiendelea kuongezewa posho za vikao, imebainika kuwa fedha anazolipwa mbunge mmoja kwa mwezi ni sawa na mishahara ya mwalimu wa shule ya msingi ya miaka mitatu. Malipo hayo pia yanaonekana kuwa sawa na mshahara wa mwaka mmoja wa daktari msaidizi mwenye shahada moja, anayeanza kazi.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa mbunge mmoja hulipwa Sh7.3 milioni kwa mwezi, ikiwa ni jumuisho la mshahara na malipo mengine ikiwamo posho za vikao. Jumuisho hilo ni pamoja na posho mbalimbali kila mwezi kama vile za mafuta ya magari, ubunge, kukaa jimboni, kuendesha ofisi na simu. Posho ya mafuta ni Sh2 milioni kwa mwezi ikikadiriwa kuwa atatumia lita 1,000 ambazo makisio ni Sh2,000 kwa lita moja. Nyingine ni posho ya kukaa jimboni Sh800,000, posho ya ubunge Sh1 milioni, kuendesha ofisi Sh700,000, simu Sh500,000 na mshahara ni Sh2.3 milioni.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, wakati mbunge akiwa hayupo bungeni inaelezwa bado analipwa posho hizo pamoja na mshahara na kumfanya ajikusanyie Sh7.3 milioni kila mwezi. Wakati wa vikao bungeni, posho zao huongezeka ambazo uchunguzi unaonyesha mbunge hupewa posho nyingine za aina tatu; za kikao, kujikimu na usafiri.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, posho hiyo ya usafiri hupewa bila kujali kuwa ana posho ya kila mwezi ya mafuta ya Sh2 milioni. Viwango vya fedha kwa posho anazopewa mbunge anapokuwa Bungeni kila kikao kwa sasa imeongezeka kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 ya posho ya kujikimu Sh80,000 na usafiri Sh50,000.

Mwalimu Lakini, wakati wabunge wakifurahia neema hizo, uchunguzi wa gazeti hili umebaini kwamba, mshahara wa mwalimu wa shule ya msingi anayeanza kazi, ambaye yupo kwenye daraja la mshahara la TGTS B ni Sh200,000 kwa mwezi.

Kwa mwalimu wa sekondari mwenye stashahada ambaye yupo kwenye daraja la TGTS C, mshahara wake ni Sh300,000 huku yule mwenye shahada wa daraja TGTS D analipwa Sh400,000, mishahara yote ikiwa ni ya kuanza kazi.

Mchanganuo huo unaonyesha kwamba, pia viwango hivyo vya mshahara vilivyoorodheshwa hapo, ni vile ambavyo havijakatwa kodi zozote zile.Kutokana na hali hiyo, mapato ya Mbunge kwa mwezi mmoja yanaweza kumlipa mwalimu mmoja wa shule ya msingi mishahara ya miezi 36 sawa na miaka mitatu.


Mshahara huo pia utaweza kumlipa mwalimu mmoja wa sekondari mwenye stashahada mshahara wa miezi 24, huku yule mwenye shahada akilipwa kwa muda wa miezi 18 kwa mapato ya mwezi mmoja ya mbunge. Fedha hizo zinaweza kumlipa mfanyakazi wa idara nyingine ya umma, ambaye mshahara wake upo kwenye daraja hilo kwa kipindi kama hicho.

Daktari Kwa mujibu wa uchunguzi wa Mwananchi, mishahara ya madaktari wasaidizi ya kuanzia ni kati ya Sh480,000 na Sh600,000 ambayo ili ifikie malipo ya mbunge kwa mwezi, itabidi iwe kati ya mara 15 na 12. Madaktari wasaidizi wenye shahada moja wanapoanza kazi, inaelezwa wanalipwa mshahara wa Sh800,000.

Kauli ya Spika Hata hivyo, Spika wa Bunge Anne Makinda, alisema posho ya vikao kwa wabunge iliongezwa kutokana na hali ngumu ya maisha mjini Dodoma. Wabunge Mbunge wa Jimbo la Ubungo (Chadema), John Mnyika alisema ongezeko hilo linatakiwa kusitishwa kwa kuwa mchakato wake umefanyika kinyume na taratibu na kwamba halina uhalali wala halijazingatia uhalisia wa maisha ya wananchi na uchumi wa nchi.

Mnyika alifafanua kwamba kauli ya Spika Makinda kwamba nyongeza hiyo inatokana na kupanda kwa gharama za maisha mkoani Dodoma haina ukweli, wala mantiki na ina mwelekeo wa upendeleo. Akamtaka Rais Jakaya Kikwete kutolea kauli kuhusu jambo hilo. Alisema utetezi wa Spika Makinda kuhalalisha kupandishwa kwa posho hizo, hauna maana na kwamba kama sababu ingekuwa kupanda kwa gharama ya maisha, ingepandishwa posho ya kujikimu (subsistence allowance) ambayo imebaki pale pale Sh 80,000.

Mbunge wa Kigoma Kusini David Kafulila, alisema suala la kupishana kauli kwa viongozi wawili wa taasisi moja, ni udhaifu mkubwa kwa taasisi hiyo. “Suala la posho inatakiwa litazamwe upya katika mihimili yote ya dola, panapokuwa hakuna kanuni ya kuweka uwiano miongoni mwa mihimili hii, kunasababisha manung’uniko na malalamiko kwa wananchi,” anasema Kafulila.

“Inatakiwa itazamwe upya, hili suala la posho lipatiwe ufumbuzi kabisa, ukiangalia huko serikalini kuna mashirika ya umma ambayo wanalipa posho za Sh400,000 mpaka 500,000, mishahara wanalipa Sh10 mpaka 15 milioni,” alisema Kafulila Mbunge wa Bumbuli, January Makamba, alisema kitendo cha wabunge kuongezewa posho za vikao kwa asilimia 185.7, kinaibua jazba kwa wananchi ambao wanahangaika kila kukicha kwa ugumu wa maisha. “Kwenye jamii lazima kuwe na usawa, kama watu tupo kwenye hali mbaya (ugumu wa maisha) lazima wote tuenende sawa.

Wabunge kuongezewa posho kwa asilimia 185 siyo sawa kabisa, tunajiweka mbali na wananchi na wanatuona tunafaidika sana wakati wao wanateseka kwa ugumu wa maisha,” alisema Makamba.

Alisema kutokana na msimamo wake huo, Juni mwaka huu alikataa posho iliyotolewa na Wizara ya Nishati na Madini baada ya kuhudhuria semina iliyoandaliwa na wizara hiyo. “Tulikaa kwenye semina kwa saa mbili, tunamaliza naletewa karatasi nisaini posho ya Sh280,000 nilikataa. Nilikataa kwa sababu nilitambua kuwa ile ni kazi yangu kama mbunge, sasa unanilipa hela ya kazi gani?” Alihoji Makamba.

Shibuda adai posho muhimu Hata hivyo, Mbunge wa Maswa Mashariki (Chadema), John Shibuda, alisema suala la wabunge kuongezewa posho halina ubaya wowote kwa kuwa litawafanya wasiwe ombaomba.

Shibuda ambaye katika mkutano wa Bunge la Bajeti alipingana na sera ya chama chake iliyokuwa katika Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010 kuhusu posho za vikao, alisema ili mbunge atekeleze majukumu yake vizuri ni lazima alipwe fedha ya kutosha.

“Umefikia wakati Waafrika tulinde fedheha kwa viongozi wetu ili wasiwe ombaomba. Viongozi wakilipwa vizuri wataweza kuitumikia nchi na jamii inayowazunguka, ipasavyo. Kutokulipwa vizuri ndio mwanzo wa viongozi kusaini mikataba mibovu,” alisema Shibuda


 
Du maskini mwalimu wakianza kumlamba makato sijui bima ya afya sijui alikuwa na kamkopo fulani.... n.k anaweza kurudi na bank slip ziro. Hapo ni lazima apige tuituon za nguvu ili ajikimu na maisha.
 
Inabidi tujitahidi sana wakati huu wa maandalizi ya katiba mpya ili tupate sheria nzuri ambazo pamoja na mambo mengine iainishe kwa uwazi mgawanyo sahihi wa keki ya taifa, vinginevyo kwa hali ilivyo sasa hali ni mbaya kwani kinachofanyika hapa ni kwamba serikali ikiwa na mpango fulani mbaya inataka bunge lipitishe inatoa posho mpya wakati wowote kwa kuwa hakuna sheria inayoruhusu majadiliano katika suala hili.
Kwa hiyo ki mantiki hata posho ni mwanzo wa kufikiwa kwa maamuzi mabaya tofauti na alivyosema Mh.Shibuda kwamba kutopewa posho kunachangia mikataba mibovu.
 
Nashindwa kuwaeleweni kwani hujajua kuwa nnchi imeingia kwenye mfumo wa Kibepari? Kenyata aliwaambia Wananchi wake "Mtu akiweza kunyonya anyonye na atakaye kubali kunyonywa anyonywe ambaye hataki kunyonya au kunyonywa aende kwa Julius Nyerere" Zama za Nyerere ndio hivyo zimeshakwisha usikae ukategemea usawa tena.
Kwa hiyo unapendekeza nchi yetu iendeshwe kwa mtindi huo?
 
Walimu wanaonewa sana...lakini ndio wanaotumiwa kufanikisha wizi wa kura kwenye chaguzi zetu wakiwa kama wasimamizi..wenyewe wametulia tu wanaona ni halali wanvyolipwa

Walimu wabadilike. WATAKUFA MASIKINI.
 
[h=3]SAKATA POSHO YA WABUNGE [/h]

Nchi imetumbukia Baharini- Dkt.Slaa
*Atamani zitumike kulipa madai ya walimu
*Alilia watoto wa maskini kukosa mikopo

Na Rehema Maigala

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Dkt. Wilbroad Slaa, amelaani vikali kitendo cha Spika wa Bunge, Bi. Anne Makinda, kukiri na kutetea uamuzi wa ofisi yake kupandisha posho za wabunge huku Watanzania wakitaabika na hali ngumu ya maisha.

Kwa mujibu wa Spika Makinda posho hizo za wabunge zimepandishwa kutoka sh. 70,000 hadi 200,000 kwa siku na tayari wameanza
kulipwa.
Akizungumza na gazeti hili jana, Dkt. Slaa alisema kitendo cha spika kuridhia na kutetea kuwapandishia posho wabunge ni kielelezo tosha kuwa nchi imetumbukia baharini na hakuna msaada wa kuiokoa kwa sasa.

Dkt. Slaa aliyezungumza huku akionesha masikitiko alisema, hakutarajia kama spika angetoa kauli hiyo hasa kwa kuzingatia kuwa bunge ni kioo cha nchi na kwamba jukumu lake ni kusimamia serikali na vyombo vyake vyote kwa masilahi ya wanyonge.
Alisema kauli ya Spika Makinda kukiri kuwapandishia wabunge posho ni sawa na kuwavunja matumaini Watanzania na kwamba wanapaswa kujiuliza ni nani wa kuwasaidia ikiwa wabunge wanajisaidia wenyewe.

"Watanzania wengi wanaishi katika hali ngumu kwa sababu ya maisha kupanda, kipato cha Mtanzania kwa siku ni kidogo ambacho hakiwezi kukidhi matumizi yake ya kila siku.
Lakini Mtanzania huyo hana wa kumsemea wala wa kumpunguzia mzigo mzito ili awe na unafuu wa maisha, hana wa kumsaidia ili awe na maisha mazuri hata kidogo," alisema Dkt.Slaa na kuongeza.

"Watoto wa kimaskini wengi hawaendelei na masomo ya elimu ya juu kwa sababu ya kukosa mikopo kutoka serikalini, kwa nini hizo pesa zilizoongezwa kwa wabunge zisingepelekwa kwa wanafunzi?

Au tunaithibisha ile kauli inayosema kuwa mwenye nacho anazidi kuongezewa?" Alihoji Dkt.Slaa.Alisema wabunge wamekuwa na posho nyingi za kila aina ambazo zingine hata hazistahili kulipwa huku wakiwaacha Watanzania wakiwa na hali ngumu ya maisha.

Alisema kitendo cha Spika Makinda kutetea posho hizo bila kujali maisha ya Watanzania walio wengi ni dalili ya chombo hicho kuwakandamiza wananchi hivyo kwenda kinyume na kazi ya bunge ya kuwatetea wananchi.

Alisema ni aibu kwa wabunge kuongezewa posho bila hata kuwajali wafanyakazi ambao wengi wao wanalipwa mshahara mdogo na kuwataka Watanzania kwa ujumla kutafakari wanatembea katika mstari upi.

Alisema sehemu kubwa ya umaskini wa Watanzania unatokana na viongozi wa serikali kujigawia posho nyingi ambazo hazina maana yeyote kwa taifa.

"Mpaka hivi sasa walimu bado hawajalipwa madeni wanayoidai serikali, wanatishia kugoma ni vyema posho hiyo ingepelekwa kwa walimu ili waweze kutoa elimu bora kwa watoto wetu," alishauri Dkt.Slaa.

Katika mazungumzo yake na waandishi wa habari juzi wakati akizindua ripoti ya Maendeleo ya Wanawake Duniani kuhusu haki kwa mwaka 2011, Spika Makinda alikiri nyongeza ya posho za vikao vya wabunge kupanda kutoka sh.70,000 hadi 200,000 kwa siku.

Alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na kupanda kwa gharama za maisha mjini Dodoma na kwamba wabunge walianza kupokea posho hiyo mpya Novemba 8, mwaka huu.

Akisisitiza umuhimu wa posho hizo alisema sh.70,000 isingemsaidia mbunge kumudu gharama hata za chumba kwa madai kuwa zimekuwa juu kutokana na mji wa Dodoma kuwa kitovu cha elimu ya vyuo vikuu kwa sasa.

"Kila kitu kimepanda bei na kwa bahati mbaya nyumba zile za CDA (Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu) zilizokuwa nafuu zilichukuliwa na wabunge wa bunge la tisa kwa mikataba binafsi na wengi hawajazirudisha hadi sasa ili kuwezesha wapya kuzipangisha," alinukuliwa akisema Spika Makinda akitetea posho hizo juzi.

Mkurugenzi naye awashangaa wabunge


Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti na Utetezi wa Haki za Ardhi, Bw. Yefred Myenzi, amesikitishwa na kitendo cha Spika Makinda kutete posho hizo na kuwataka wabunge kutambua kuwa hali ngumu ya maisha ipo kwa kila Mtanzania na si kwao pekee.
Akizungumza na Majira Dar es Salaam jana, Bw. Myenzi alisema hali halisi ya Mtanzania hairuhusu mbunge kupandishiwa posho kutoka sh. 70,000 hadi 200,000 kwa siku na kwamba hizo ni anasa .
Alisema wabunge wanavyanzo vingi vya mapato mbali na mishahara yao hivyo hawakustahili kuongezewa posho kiasi hicho huku Watanzania wakizidi kulilia hali ngumu ya maisha.
"Hali hii inaonesha ni kwa jinsi gani wabunge walivyo wabinafsi, wanajali masilahi yao wenyewe na kuacha wananchi wakiumia," alisema.

Katibu wa Bunge akanusha

Hata hivyo hivi karibuni Katibu wa Bunge, Dkt.Thomas Kashililah, alitoa taarifa kwa vyombo vya habari akikanusha kuwepo kwa nyongeza hiyo.

Katika taarifa hiyo Katibu huyo wa bunge alikiri kuwa wabunge wanataka waongezewe posho za vikao lakini mapendekezo hayo hayajaanza kutekelezwa.

Alisema mapendekezo ya nyongezo hiyo yaliibuka katika mkutano wa wabunge mjini Dodoma, Novemba 8, mwaka huu walipoiomba serikali iangalie upya suala hilo kwa lengo la kuboroshewa.
Dkt. Kashililah alisema serikali ilikuwa haijatoa taarifa iwapo posho hiyo imeongezeka kutoka sh.70,000 hadi 200,000.

Balozi Seif atetea posho Wakati huohuo, Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, amesema wabunge kuongezwa posho za vikao ni halali kwa kuwa gharama za maisha katika Mkoa wa Dodoma zimepanda.

Alisema ongezeko hilo litalinda heshima za wabunge pindi wanapokuwa wakiendelea na vikao vya bunge.
"Nafikiri siyo heshima kwa mbunge baada ya kumaliza vikao anakwenda kulala kwenye gesti ya sh. 5000 hii ni aibu, ni sawa posho zilivyopandishwa," alisema.

Alisema anakubaliana na uamuzi wa serikali kuwa ni mzuri na ut
ampa nafasi nzuri mbunge ya kuishi wakati wa vikao.
 
Kama ulichosema hapa ni kweli, its sad.Wanawaadhibu wasiohusika - watoto wa wakulima, watoto wa maskini!
Kwani hao hao wanaojilipa mishahara minono, watoto wao wanasoma hizo shule za kata?

Kwani Mtu maskini Tanzania, anayepeleka mtoto wake shule za kata/za serikali anahusika vipi na uonevu wa walimu wanaoendelea na mgomo wa kudumu?
Tunafanya utani lakini tujue hili kama linaendelea, maskini watabaki maskini ilhali matajiri na vizazi vyao wataendelea kuneemeka.
Kumbukeni tuko kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.Tukijikumbusha historia, tutapata kwamba zamani zile watoto wa maskini waliweza kuja kuibuka na kuwa watu kwa sababu ya elimu waliyoipata ndani ya mfumo wa kikoloni.Kizuri kuhusu serikali ya kikoloni ni kwamba, mtu hakuweza kupelekwa ualimu unless awe amafaulu vizuri sana masomo yake ya sekondari. Siku hizi serikali ya huru imeona ni vema kufanya ualimu ni taaluma ya wale walifeli masomo yao, wale walioishia darasa la saba na huenda kikawa ndicho chanzo cha kuwapunja mishahara yao na stahiki zao nyingine! Sad! Wakati ule walimu hawakufanya mgomo bali walifundisha kwa bidii sana kwani walijisikia ni viongozi waliothaminika na kwamba wao ndio muhimili wa taalum.

Viongozi wengi waliokuja kushika madaraka baada ya uhuru hawakuwa watoto wa matajiri, bali walikuwa waana wa wakulima na wafugaji maskini.Mifano tunayo mingi tu.Msemo wa kwamba "elimu ni ufunguo wa maisha" ulileta maana kwenye maisha yao. Huku tunakoelekea, itakuwa "utajiri ndio ufunguo wa maisha " maana utajiri na mali ndivyo vitakupa fursa kupata elimu bora na siyo bora elimu kama sasa. Elimu bora itafungua milango mingi - hata wamachinga wasiokuwa na elimu wataonja joto ya jiwe kama bado hawajalionja, watatupwa nje ya ushindani.Kilimo cha mkulima aliye na elimu bora, kitampatia tija na manufaa na kushindanisha bidhaa sokoni.

Time bomb hilo linasubiri kulipuka!
Ndugu yangu, tangu lini mtu mwenye njaa kali akawa na busara?Si umesikia kule Igunga wananchi wenye hasira kali walimchoma moto mwalimu mpaka kufa eti aliiba mifuko miwili ya sementi? Je walimu wenzake walio shuhudia hilo watapata wapi moyo wa kazi? watawatofautishaje watoto wa kata?Walimu wenye njaa huku wakiwaona wabunge wao waliochaguliwa kwa rushwa ya kanga na kofia wakijishenezea maposho kibao watapata nafasi ya kuchambua madhara ya mgomo wao?
 
Du maskini mwalimu wakianza kumlamba makato sijui bima ya afya sijui alikuwa na kamkopo fulani.... n.k anaweza kurudi na bank slip ziro. Hapo ni lazima apige tuituon za nguvu ili ajikimu na maisha.
Ndugu yangu wee,hiyo inawezekana Dsalaam na baadhi ya miji tu, kunasehemu wanafunzi hata tuition ya bure hawaendi! basi mwalimu katika mazingira hayo anaishia kula 'ugimbi' kwenda mbele,
 
Hii vita ni yetu sote watanzania wote tunanyonywa na si walimu tu kama inavosemekana. Tuungane tuupinge unyonyaji huu.

Hivi hii mentality ya KIPAGANI wanayoi-apply wabunge wa Tanzania kuwanyonya wapiga kura wao, wameitoa kwa shetani yupi ambaye zamani hakuwepo? wabunge hawatambui kama wapiga kura wao wana shida coz wote wamerundikana Dar.
 
Walimu wanaonewa sana...lakini ndio wanaotumiwa kufanikisha wizi wa kura kwenye chaguzi zetu wakiwa kama wasimamizi..wenyewe wametulia tu wanaona ni halali wanvyolipwa

Kha kumbe wao ndo wanasababisha yote hayo? Sas wanamlalamikia nani kama mtetezi wao walimwibia kura zake
 
Wacha matusi wewe, siokweli kuwa walimu wamelidhika na hali hiyo, walimu wanamgomo wa kudumu, kama hujui tembelea sehemu za kazi za walimu ukaone kinachoendelea, au kama huwezi basi waulize wakaguzi wa shule wakueleze. Madhara ya mgomo huu ni makubwa sana, matokea yake kwa mbali yalijionesha ktk matokeo ya mitihani ya kidato cha nne 2010.

Mkuu huo sio mgomo kwani kufanya uzembe ktk ufundishaji nikwamba wanawapotosha vijana na madhara ni kwa vijana hao hao ni bora wangefanya mgomo kama kenya ikaeleweka kimoja kuliko hiyo wanayofanya ambayo haitasolve matatizo yao.
 
Hii vita ni yetu sote watanzania wote tunanyonywa na si walimu tu kama inavosemekana. Tuungane tuupinge unyonyaji huu.

Sidhani kama watz kama tuna umoja wa kutetea haki zetu, na siku huu umoja utakapokuwepo ccm mtalia na kusaga meno
 
Nadhani kuna ukweli hapa. Mimi nina kituo cha kufundisha PRE-FORM ONE. Overall na individual performance ya wale watoto inatia shaka kama kama kauli ya ualimu ni wito kama inafanya kazi tena. Nitawawekea matokeo ya mtihani wa English Grammar ambao niliwapa hivi karibuni. Ni aibu.

Hapo alaumiwe nani? Maana kama walim ni wito sio 7bu yakutolipwa mishahara au kuishi mazingira magum, na nyie serikali kwa kipindi chote hicho mmekaa kimya bila mikakati yoyote yakuwafanyia malipo mkijifanya hamna hela wakati wabunge mnawaongezea posho ambazo hata kwenye bajeti hazipo, maadhisho ya uhuru mmetumia mabilini ya hela huku mambo nyeti kama elim mkiyafumbia macho sijui tz baada ya miaka mi5 itakuwa je
 
Mgomo uliotangazwa ni kukazia ule wa awali ambao walisha uanza siku nyingi. Sasa hivi walimu hawajali tena, watoto wa kifeli kwake ni sawa na wakifaulu kwake haina tija.

Nakubaliana na mdau mmoja hapo juu kuwa matokeo ya kidato cha nne mwaka jana iliku ni matokeo ya mgomo wao wa chinichini, cha msingi hapa ni wao kwa wingi wao kugoma kwa kutokwenda makazini ili kuonyesha kukwera na hali ilivyo sasa.

Mgomo kama huo ni mbaya sana sawa na kumhasi tu ili asipate mtoto kwahiyo hapo ni kulihasi/kuuwa kabisa Taifa ni bora ule wakuingia barabarani kwani hata wakipigwa mabom mashirika ya haki za binadam yanaweza kuingilia
 
Mwisho wake mtu wa hali ya chini anazidi kuwa wa hali ya chini tu kama mtoto wake anapelekwa shule ambayo walimu wako likizo mwaka mzima ni hatari na kamwe hii hali kwa watu wenye uchungu na watoto wao hawawezi kuvumilia hata kidogo
 
Back
Top Bottom