Mshahara wa Mbunge wa mwezi ni Mshahara wa Mwalimu wa Miaka Mitatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshahara wa Mbunge wa mwezi ni Mshahara wa Mwalimu wa Miaka Mitatu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Dec 10, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Dec 10, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Nimesoma kwa masikitiko gazeti la Mwananchi leo kuwa mshahara wa mbunge wa mwezi mmoja ni mshahara wa mwalimu wa msingi wa miaka mitatu na mshahara wa Medical Doctor wa mwaka mmoja. Pamoja na hayo bado wanataka kujiongezea. Kumbe ndio maana watu wanakimbilia ubunge
   
 2. Mwasi

  Mwasi JF-Expert Member

  #2
  Dec 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2010
  Messages: 249
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Walimu wanaonewa sana...lakini ndio wanaotumiwa kufanikisha wizi wa kura kwenye chaguzi zetu wakiwa kama wasimamizi..wenyewe wametulia tu wanaona ni halali wanvyolipwa
   
 3. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #3
  Dec 11, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Ndio tatizo la nchi yetu hilo.
  Yani wale wanaofanya kazi muhimu na zinazoleta matokeo yanayoonekana hawatiliwi maanani. Ni aibu kweli kwamba hilo dara la mishahara lipo na watu wamekaa kimya tu wakiangalia mafisadi (wabunge) wanavyojilimbikizia bila kujali wananchi wao.
   
 4. d

  dada jane JF-Expert Member

  #4
  Dec 11, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Sasa hivi walimu nao wamefunguka. Uliona au kusikia walichokifanya kwenye uchaguzi Igunga?
   
 5. N

  Ndjabu Da Dude JF-Expert Member

  #5
  Dec 11, 2011
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 3,648
  Likes Received: 408
  Trophy Points: 180
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Gwalihenzi

  Gwalihenzi JF-Expert Member

  #6
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 5,117
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 145
  Wacha matusi wewe, siokweli kuwa walimu wamelidhika na hali hiyo, walimu wanamgomo wa kudumu, kama hujui tembelea sehemu za kazi za walimu ukaone kinachoendelea, au kama huwezi basi waulize wakaguzi wa shule wakueleze. Madhara ya mgomo huu ni makubwa sana, matokea yake kwa mbali yalijionesha ktk matokeo ya mitihani ya kidato cha nne 2010.
   
 7. Erickb52

  Erickb52 JF-Expert Member

  #7
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 18,566
  Likes Received: 112
  Trophy Points: 160
  Si kwamba waalimu wako kwenye migomo kila siku,ila kinachotokea mashuleni ni kuwa wamepunguza ufanisi wa kazi na morali ya kazi haipo tena, yan wanafanya wanavyojisikia na si kutoa elimu bora.
   
 8. usininukuu

  usininukuu JF-Expert Member

  #8
  Dec 11, 2011
  Joined: Aug 8, 2011
  Messages: 380
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii vita ni yetu sote watanzania wote tunanyonywa na si walimu tu kama inavosemekana. Tuungane tuupinge unyonyaji huu.
   
 9. m

  mkwegi Member

  #9
  Dec 11, 2011
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 20
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Ndiyo maana kuna matabaka kadhaa kwa sasa...wenzetu wanaonufaika wanatambua kuwa kiini cha maendeleo ya nchi yoyote ni kuwa na jamii iliyoelimika na yenye kuweza kuchanganua michakato na majukumu ya kimaendeleo na usimamizi bora. Wanatambua kuwa ili kupata kada hiyo ni lazima kuwa na mfumo mzuri wa elimu ambao vyanzo ni pamoja na mitaala kidhi (visionary curricula), walimu bora na walio na ari ya kufundisha na kutoa mabingwa wa leo na kesho, n.k. Sasa tabaka miliki/tawala lilipogundua kuwa limekula kianzio cha kuboresha maeneo nyeti, ....wakatabiri anguko la taifa kwa kipindi kijacho na wakachukua hatua...WAKAPELEKA WATOTO WAO KTK MASHULE MAZURI iwe nje au hapa ndani...wakijiamini kuwa pindi taifa litakapoanguka kwa kuwa na wengi wajinga wasio na uwezo, basi ni WATOTO WAO NA WA MARAFIKI ZAO TU ndio watashika taifa!!!!!

  Hivyo kujipanga kwetu na kuchukua hatua kunahitaji umakini wa hali ya juu tukizingatia kuwa hali hii imeanza zaidi ya miongo miwili iliyopita na sasa ni hao WATOTO WAO NDIO TAYARI WANAITWA WATAWALA WA LEO, hawafanyiwi hata interview na ikitokea wakafanya wakionekana wameshindwa maafisa uajiri wanafokewa na wengine kushushwa vyeo, kuachishwa kazi kwa visingizio mbali mbali!!!! Lakini sisi nao hatuko nyuma ijapo kupitia shule zetu za chini ya mwembe na ****** chini bila sakafu...tutawang'oa tu hata kama siyo mwaka huu, mwaka kesho, mwaka kesho kutwa...mwaka....mtondo gooo na watapoteza kila kitu ili heshima ya taifa hili irudi mikononi mwa watanzania wenyewe.
   
 10. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #10
  Dec 11, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Mkiulizia mshahara wa boss wa UNESCO ndiyo mtajua kuwa wabunge wanapata hela ndogo sana.
   
 11. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #11
  Dec 11, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Nadhani kuna ukweli hapa. Mimi nina kituo cha kufundisha PRE-FORM ONE. Overall na individual performance ya wale watoto inatia shaka kama kama kauli ya ualimu ni wito kama inafanya kazi tena. Nitawawekea matokeo ya mtihani wa English Grammar ambao niliwapa hivi karibuni. Ni aibu.
   
 12. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #12
  Dec 11, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu hata hiyo ni aina flani ya mgomo.
   
 13. Wa kusoma

  Wa kusoma JF-Expert Member

  #13
  Dec 11, 2011
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 3,315
  Likes Received: 2,245
  Trophy Points: 280
  Mimi nilishangaa eti mtu ana acha ukamishina wa madini anaenda kugombea ubunge igunga.
   
 14. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #14
  Dec 11, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Mgomo uliotangazwa ni kukazia ule wa awali ambao walisha uanza siku nyingi. Sasa hivi walimu hawajali tena, watoto wa kifeli kwake ni sawa na wakifaulu kwake haina tija.

  Nakubaliana na mdau mmoja hapo juu kuwa matokeo ya kidato cha nne mwaka jana iliku ni matokeo ya mgomo wao wa chinichini, cha msingi hapa ni wao kwa wingi wao kugoma kwa kutokwenda makazini ili kuonyesha kukwera na hali ilivyo sasa.
   
 15. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #15
  Dec 11, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kama ulichosema hapa ni kweli, its sad.Wanawaadhibu wasiohusika - watoto wa wakulima, watoto wa maskini!
  Kwani hao hao wanaojilipa mishahara minono, watoto wao wanasoma hizo shule za kata?
  Kwani Mtu maskini Tanzania, anayepeleka mtoto wake shule za kata/za serikali anahusika vipi na uonevu wa walimu wanaoendelea na mgomo wa kudumu?
  Tunafanya utani lakini tujue hili kama linaendelea, maskini watabaki maskini ilhali matajiri na vizazi vyao wataendelea kuneemeka.
  Kumbukeni tuko kwenye maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru.Tukijikumbusha historia, tutapata kwamba zamani zile watoto wa maskini waliweza kuja kuibuka na kuwa watu kwa sababu ya elimu waliyoipata ndani ya mfumo wa kikoloni.Kizuri kuhusu serikali ya kikoloni ni kwamba, mtu hakuweza kupelekwa ualimu unless awe amafaulu vizuri sana masomo yake ya sekondari. Siku hizi serikali ya huru imeona ni vema kufanya ualimu ni taaluma ya wale walifeli masomo yao, wale walioishia darasa la saba na huenda kikawa ndicho chanzo cha kuwapunja mishahara yao na stahiki zao nyingine! Sad! Wakati ule walimu hawakufanya mgomo bali walifundisha kwa bidii sana kwani walijisikia ni viongozi waliothaminika na kwamba wao ndio muhimili wa taalum.

  Viongozi wengi waliokuja kushika madaraka baada ya uhuru hawakuwa watoto wa matajiri, bali walikuwa waana wa wakulima na wafugaji maskini.Mifano tunayo mingi tu.Msemo wa kwamba "elimu ni ufunguo wa maisha" ulileta maana kwenye maisha yao. Huku tunakoelekea, itakuwa "utajiri ndio ufunguo wa maisha " maana utajiri na mali ndivyo vitakupa fursa kupata elimu bora na siyo bora elimu kama sasa. Elimu bora itafungua milango mingi - hata wamachinga wasiokuwa na elimu wataonja joto ya jiwe kama bado hawajalionja, watatupwa nje ya ushindani.Kilimo cha mkulima aliye na elimu bora, kitampatia tija na manufaa na kushindanisha bidhaa sokoni.

  Time bomb hilo linasubiri kulipuka!
   
 16. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #16
  Dec 11, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Wanchekesha kama semavyo FF!
  HIVYO VITU VIWILI NI KAMA MBINGU NA ARDHI!
  Huyo mbunge wako sana sana aliwadanganyeni kwa kuku na pilau na t-shirt na kofia kama siyo kanga na taulo za akina mama, mkampa kura.Boss wa UNESCO, Ukiacha CV yake iliyoshindanishwa world-wide na magwiji wengine, hizo levels za interview usipime!

  Sasa ulitaka alipwe nini, au umetumia kigezo gani kuona mbunge analipwa mshahara mdogo?
   
 17. No admission

  No admission JF-Expert Member

  #17
  Dec 11, 2011
  Joined: Nov 26, 2011
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nashindwa kuwaeleweni kwani hujajua kuwa nnchi imeingia kwenye mfumo wa Kibepari? Kenyata aliwaambia Wananchi wake "Mtu akiweza kunyonya anyonye na atakaye kubali kunyonywa anyonywe ambaye hataki kunyonya au kunyonywa aende kwa Julius Nyerere" Zama za Nyerere ndio hivyo zimeshakwisha usikae ukategemea usawa tena.
   
 18. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #18
  Dec 11, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Maisha ni kutafuta...hamna mtu anayezaliwa na chapa ya ubunge, ubunge unakuja kwa jitihada za mtu mwenyewe. Walimu nao wana nafasi ya kugombea ubunge ili wajikwamue. Nafikiri mnakumbuka alichokifanya yule mwalimu wa Igunga.
   
 19. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #19
  Dec 11, 2011
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Kaka Rejao, hapa mbona umeniangusha!
  Sasa kila mtu akienda kugombea ubunge, nani atafanya hizo kazi nyingine? Huhitaji madaktari? No wonder wataalamu wengi wamezikimbia fani zao, halafu tunalalamika hudumu mbaya!
   
 20. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #20
  Dec 11, 2011
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,556
  Likes Received: 486
  Trophy Points: 180
  Kinachowadumaza walimu mawazo ni CWT!Chama chao kimeshindwa kuwaunganisha walimu wote nchini.Chama hiki ambacho walimu wanakichangia kimeshindwa kuonyesha tija yeyote kwa walimu.Kila siku wao mgomo wao mkuu ni malimbikizo tu!Kimekuwa ni chama cha kufuatilia madeni ya walimu badala ya maslahi ya walimu!Utafikiri kama hayo madeni ambayo baadhi ya walimu wanadai serikali yakilipwa basi sasa walimu watakuwa na hali nzuri.Vile vitu vya msingi kama mshahara duni wamemwachia Mgaya na tucta yake!Huwa najiuliza kama kungekuwa hakuna walimu wanaodai serikali kazi ya hiki chama ingekuwa nini.Kwanini wasiunganishe walimu kudai mishahara inayoendana na maisha ya sasa na mazingira mazuri ya kazi kwa ujumla?Kwanini wasidai HADHI ya ualimu ambayo serikali imeipoteza?Wenyewe malimbikizo tu na vitu ambavyo haviwagusi walimu wote.Mwalimu ambaye hadai,analipwa mshahara kwa wakati,je ana hali nzuri kimaisha kiasi cha CWT kukomaa na madeni tu kila siku?Hakuna mabadiliko mwalimu ategemee chini ya CWT hii dumazi inayowaza madeni tu!
   
Loading...