Mshahara huu kwenye kampuni ni haki? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mshahara huu kwenye kampuni ni haki?

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by Pretty P, May 11, 2011.

 1. P

  Pretty P Senior Member

  #1
  May 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Habari wanaJF, kuna kampuni moja kubwa kwa jina hapa Tanzania na muhimu katika nchi yetu. Cha kushangaza ni kwamba tangu watuwaajiriwe hawaja sign contract.

  Pili malipo kwa mwezi ni 105000Tsh tu. Na wanalipa kwa cammission, kazi ni ngumu kwani wawezapata wateja hata 600 kwa mwezi but wakiondoa dublication unaweza jikuta unabaki na wateja 300 kwa mwezi hapo kuna kukatwa NSSF.

  Ni sawa kweli wana JF?
   
 2. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #2
  May 11, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Pretty P,
  sijaelewa haki ipi unayozungumzia hapa. Kulipwa malipo unayolipwa, kusaini mkataba ama malipo kwa kamisheni?
  Mshahara ni makubaliano ya mwajiri na mwajiriwa bila kuvunja sheria.
  Sijajua sheria na vifungu elekezi kwa level ya mishahara hasa katika makampuni binafsi.
  Makampuni mengi yanayohusika na sales mara nyingi wanatumia kamisheni kama Bonus payment na motivation kwa waajiriwa.
  Kama unahisi huridhiki na hapo ulipo, ajira ni soko huria hivyo unaweza kutafuta pengine.
   
 3. P

  Pretty P Senior Member

  #3
  May 11, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kusign mkataba, na malipo ni kidogo bse mshahara kimo cha chini ni sh. Ngapi? Je suala la mkataba we huoni linamatter??
   
 4. t

  tizo1 JF-Expert Member

  #4
  May 11, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 857
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  dadavua mambo wewe!sema ni kampuni gani sio unafichaficha!taja jina la kampuni yako na ipo wapi!
   
 5. P

  Pretty P Senior Member

  #5
  May 12, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mmmmh!! S
   
 6. kipipili

  kipipili JF-Expert Member

  #6
  May 12, 2011
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 1,499
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  uoga wako ndiyo umaskini wako
   
 7. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #7
  May 12, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,025
  Likes Received: 744
  Trophy Points: 280
  Kama mmekubaliana na si chini ya kima cha chini,huna cha kulalamika.
   
 8. m

  mushi.richard Member

  #8
  May 13, 2011
  Joined: Jul 31, 2007
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Inabidi urejee kwenye "Government notice No.172 ya 30.04.2010" yenye kichwa cha habari "Regulation of Wages and Terms of Employment Order,2010. Hapo utapata kima cha chini cha mshahara kwa sekta mbalimbali.
   
 9. N

  Ngoswe11 Member

  #9
  May 13, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 87
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sio unalalamika lalamika ovyo wewe kama vipi si uache hiyo kazi? hulazimishwi, kwa mashahara huo inaonekana kwanza Elimu yako ni ndogo sana either form 4, au form 2! so who cares about it! hiyo inaitwa cheap lobour! Everywhere in the world is existing! People/mostly are getting higher salaries in relation to their level of education.

  Sio unatuletea hadith rejea hapa kumbe wewe ni secretary tu wa kikampuni fulani. Tena kazi uliomba kwa kubembeleza leo ohoo mshahara mara mkataba! We vipi bana?

  Kama rudi class, then baadae dai dau la juu, utalipwa tu tena faster
   
 10. TANMO

  TANMO JF-Expert Member

  #10
  May 13, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 8,919
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Jaribu kumweleza Boss wako maneno haya uliyotueleza, utapata ufumbuzi...
  Narejea Kauli ya Kipipili; Uoga wako ndiyo umasikini wako...
  Good luck...
   
 11. L'AMOUR

  L'AMOUR Senior Member

  #11
  May 13, 2011
  Joined: Mar 8, 2011
  Messages: 110
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Naomba nimtetee pretty P kwamba si kweli mshahara unalingana na elimu yake ila nadhani kwa soko huru la ajira ya sasa ni kwamba shida zako ndizo zitakazolingana na mshahara wako. Cha msingi ni kumshauri avumilie wakati anaangalia kwingine kwani kuna wengi sana wanapata mshahara kama wa Pretty P lakini wao huwa hawalalamiki hapa jamvini kama yeye.

  Hii ni kwa kuwa serikali imeruhusu wawekezaji waongeze ajira kwa mshahara wa kufikirika hasa kwenye mambo ya sales. Utasikia wanaanza kwa kusema eti basic Tsh. 105,000 kisha ukipata wateja 600 unapewa 1000( buku) kwa kila mteja kama commission na pia kuna X-mas bonus na utalipiwa nauli ya daladala wakati wa kutafuta wateja na vocha ya buku kumi kila mwezi.

  Sasa kama uko Dar kwa ndugu yako na maisha hayaendi kila siku inabidi kujiingiza tu katika ajira hiyo bila kujali wala kutafakari mahesabu ya mshahara kutokana na pressure ya maisha. Na baadae ukishaizoea kidogo ile kazi na kukutana na watu wanaolipwa vizuri unaanza kulalamika bila kumshukuru mungu kwa kukupa kidogo hicho alichokuanzishia.

  Mimi nadhani hapa ni kutafuta kazi nyingine wakati unavumilia hiyo uliyopo Ukilogwa kutaja jina la kampuni hapa jamvini unaweza kung'olewa hata hicho kidogo usikipate tena. Wadau hapa watakusaidia kupata kazi wewe weka sifa zako na elimu yako hapa maana hata walinzi nafasi zao zipo, madereva pia bila kusahau makatibu muhtasi. Nawasilisha
   
 12. Graca

  Graca JF-Expert Member

  #12
  May 14, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 472
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Good advice L'amour
   
 13. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #13
  May 14, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  sasa mbona hapo mtu ana hela nzuri sana? unapata bonus ya 1000 kwa kila mteja?? kwa mwezi na bonus ya 300,000 + 105000 = 405000

  sasa 405000 kwa mwezi ni hela ndogo???
   
 14. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #14
  May 14, 2011
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  achana na kazi ya kuajiriwa karibu kwenye kilimo na ufugaji! hata kama una mtaji wa 1m utaanza taratibu!! muulize Elnino na Malila
   
 15. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #15
  May 14, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Inawezekana hayo malipo yakawa sahii, kwa siku hizi mishahala ni ya kisekta; hiyo kampuni hiko sekta gani!! Sekta ya madini, kilimo, afya, viwanda au ya ulinzi?
  Siku zote ukitaka kusaidiwa jaribu kuwa wazi ktk kutoa dukuduku lako.
   
 16. D

  DURACEF JF-Expert Member

  #16
  May 16, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 244
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 45
  me nakushauri acha kazi rudi kijijini kalime
   
 17. Mlimazunzu

  Mlimazunzu JF-Expert Member

  #17
  May 17, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 420
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi hiyo sio kazi eti eehhh mbona mie mkewangu ni secretary tena ananizidi mshahara wakati mimi ni injinia??? Acha dharau kijana
   
 18. Osaba

  Osaba JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 1,725
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  acha dharau wewe unajua secretary wa waziri mkuu analipwa sh ngapi wewe?
   
 19. g

  gerald lebbayo Member

  #19
  May 20, 2011
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Siku zote ili upate mafanikio ni lazima uanzie chini, hivyo kama huo mshahara ni mdogo komaa na kazi na ipo siku mshahara utapanda tu. Make kumbuka kuna bodi husika kuhusiana na malipo ya m2 ni sawa na kazi anayofanya na ni sawa na elimu yake ,usikate tamaa
   
 20. b

  banyenza New Member

  #20
  May 21, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata kama salary ni ndogo kiasi gani wewe piga kazi husiangalie mshahara hipo siku utakuta mambo yamekuwa mazuri tu... uvumilivu ni muhimu wana JF....!:mod:
   
Loading...