Msemo wa Clouds “KATAA KUWA KAA" Unadhani unalenga nini?

Msemo wa Clouds “KATAA KUWA KAA" Unadhani unalenga nini?

KakaKiiza

Platinum Member
Joined
Feb 16, 2010
Posts
11,952
Reaction score
9,469
Nimesikiliza sana kampeni ya kataa kuwa kaa yani kuna mtu kalengwa kwa maana anawivu apendi kuona wenzake wanapaa sikiliza utajua ni hayo tu Ila wanempiga mtu.
 
Bila shaka Mlengwa atakuwa ni "Kaa wa Maji Chumvi"..,
 
Atakuwa ni mke wa Mugabe, hakuna KAA mwengine. Maana yule mama anawivu hatari, hapendi wenzake wafanikiwe. Labda wafanikiwe kupitia yeye, KAA anataka atangazwe yeye tu kwenye vyombo vya habari, KAA anataka aonekane yeye tu kwenye kurasa za mbele ya magazeti. KAA anataka watu wote wawe KAA, hakika KATAA KUWA KAA.
 
...."Chukua ndoo waweke KAA ndani ya Ndoo hata zaidi ya siku hakuna hata KAA hata mmoja ambaye anaweza kutoka sababu kila anayejaribu kutoka atarudishwa chini.
Kama nchi kama tukiwa na tabia za UKAA hatuwezi kufanikiwa ... "
 
Mtoa maada kuna sumu anapunguza, sawa lakini chuki ikimzidi mwanadamu anakuwa mtumwa
 
Nimesikiliza sana kampeni ya kataa kuwa kaa yani kuna mtu kalengwa kwa maana anawivu apendi kuona wenzake wanapaa sikiliza utajua ni hayo tu Ila wanempiga mtu.
Kwa muda wa miaka mingi sana Clouds walikuwa ndio MAKAA wakubwa. Waliweza kumshusha SUGU kwa kutopiga nyimbo zake na pia Lady JD.
Leo wamekutana na yale walio tendea wengine ndio wana piga kele.
Clouds acheni utoto. Tulieni kuleni matapishi yenu.
NYIE NDIO MLIO TUFUNDISHA KUWA KAA
Mtenda akitendewa........
 
[emoji23]nmecheka Kwa sauti acha wale matapishi yao,,, ila Cloud wanaroho mbaya kichini chini huku wamejivika ngoz Ya kondoo
 
Nimesikiliza sana kampeni ya kataa kuwa kaa yani kuna mtu kalengwa kwa maana anawivu apendi kuona wenzake wanapaa sikiliza utajua ni hayo tu Ila wanempiga mtu.
katika watu wana vijembe na wanawake wa uswahilini ni clouds media nazani,siwezi kushangaa kuja na majina ya ajabu ajabu kwa maelengo au visasi vyao.mfano mzuri tunao tu kwa wasanii kama usipo kubali matakwa yao,kila kipindi utakacho fanyiwa au kupewa vijembe vya kila aina ili mradi wakupoteze tu.
kosa linatokea clouds kuendeshwa na hisia ya mtu au watu bila kuangalia wao ndio kioo cha jamii mfano hapa tcra imewalamba faini XXL na jahazi.umejua kuwa ni watu wanao weka hisia zao kupitiliza.
hata kama ni ubunifu jaribu kuweka mazingira ikawa redio ya watu si redio ya mtu na mawazo yake.utagundua kila jambo fulani ambalo kama hawaja pendezwa nalo.ndipo taarabu zao zina kuja na misemo na kujadiliwa kila kipindi ilimradi kutoa ya moyoni.
 
[emoji23]nmecheka Kwa sauti acha wale matapishi yao,,, ila Cloud wanaroho mbaya kichini chini huku wamejivika ngoz Ya kondoo
Mkuu yani wangekuwa na akili wangeacha kabisa hii kitu ya KAA. Tunayajua mengi sana juu ya wao kuwa KAA. Wapo wanamziki wa kike wamesha lalama sana kuwa wamefanyiwa UKAA ndani ya CLOUDS na ikabidi wawevitoweo. Zamaradi imekuwaje alipokataa kuwa KAA?
 
wao wenyewe kaa
kugoma kupiga nyimbo za wasanii wenye bifu nao ni nini
 
Kwa muda wa miaka mingi sana Clouds walikuwa ndio MAKAA wakubwa. Waliweza kumshusha SUGU kwa kutopiga nyimbo zake na pia Lady JD.
Leo wamekutana na yale walio tendea wengine ndio wana piga kele.
Clouds acheni utoto. Tulieni kuleni matapishi yenu.
NYIE NDIO MLIO TUFUNDISHA KUWA KAA
Mtenda akitendewa........
"Mchuma Janga hula na wa kwao!"
 
Back
Top Bottom