Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,262
Msemaji wa Yanga Haji Manara ameufya kwa kuamua kujishusha baada ya kumuomba radhi Rais wa TFF Wallace Karia kuhusu jambo ambalo lilitokea Jijini Arusha wakati wa fainali la Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup ASFC, baina ya Yanga SC na Coastal Union.
"Jana mimi na rafiki yangu Heris Said alinisindikiza kwenda kumuona Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania Wallace Karia, na tuliongea kwa furaha sana na kuzungumza mambo ya msingi zaidi nyumbani kwake.
"Kiukweli jambo la Arusha tukio zima halikua na matusi, hilo nataka iwe Very Clear, ambalo watu wengi wananishtumu nalo na waling'ang'ania hapo hapo.
"Ndo maana nilisema pale Airport, kuwa atakayepata tukio lile likiwa na matusi nitajiuzulu kwa kuwa nitakuwa kinyume na hata maadili ya kitanzania na wala si football peke yake.
"Kwa namna yoyote ile naomba msamaha, nilikosea kujibizana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Tanzania Wallace Karia, naomba radhi, na haimaanishi mimi nisichukuliwe hatua.
Kama itaonekana nastahili kuchukuliwa hatua nipo tayari kupokea adhabu hiyo, lakini lazima niombe msamaha bila kujali kamati itaamua nini.
Kingine sina matatizo na Karia, ni Mzee wangu na namheshimu, na nimekuwa mstari wa mbele mara kadhaa kutetea hoja zake.
Naomba radhi, mimi ni mwanadamu na binadamu yoyote yule hukosea, ila kwa kuwa Rais amenizidi kwa vitu vingi sana, sina budi kuheshimu na kuomba radhi kubwa kwake, amenizidi umri na mambo mengi ambayo itakuwa si uungwana kuliacha jambo hili."
Amezungumza Haji Manara kwenye mkutano wake na waandishi wa vyombo vya habari, kufuatia kadhia yake na Rais wa TFF Wallace Karia.