Msemaji wa upinzani katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, amesusa kusoma hotuba

Tusimtafute mchawi kwenye uchaguzi maana wananchi watafika mahala tutachoka na mamabo ya kususasusa, pigeni kazi acheni mambo ya misuso

Wakati wa uchaguzi nani kakuambia kura za wananchi ni muhimu? Wakati wa uchaguzi cha muhimu ni tume kufuata wanachotaka watawala na sio wingi wa kura. Na ikiwa kura ni nyingi kupita kiasi matokeo yanaahirishwa kisha uchaguzi unatangazwa kurudiwa.
 
pic+bungeni.jpg

Msemaji wa upinzani katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira na Muungano, Ally Salehe amesusa kusoma hotuba yake ya upinzani kuhusu wizara hiyo baada ya kulazimishwa kuacha kusoma baadhi ya maneno yakiwamo yanayohusu Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar na mgogoro wa CUF.

Hali hiyo imetokea bungeni leo Jumatatu baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali(AG), George Masaju kusimama na kupinga baadhi ya maneneo aliyotumia kama “Kila wizara imekiona cha moto, wamebanwa mpaka wamevunjwa mbavu” na kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeathirika vibaya na kisu cha ngariba kwa kukata bajeti yake.

Baada ya malumbano, Mwenyekiti wa Bunge, Musa Zungu alitoa uamuzi kuwa maneno yaliyoandikwa kuanzia ukurasa wa tatu hadi wa saba kwenye hotuba hiyo yasisomwe wala kurekodiwa kwenye kumbukumbu rasmi za Bunge.

Baada ya uamuzi huo, Salehe alisema basi asingeendea kuisoma hotuba yake na yaliyobaki anamwachia ngariba afanye anavyotaka.
Ukimwachia Ngariba, upo uwezekano akaondoka na kichwa.
 
Kafu wao ni kususa susa tu.Hasara kwa wafuasi wao wameshindwa kujua kilichomo.
Watu wanataka kusikia njia mbadala ya kutatua kero za muungano,yule mzanzibari analeta mambo ya ngariba sijui kisu chake hakikati govi yanatuhusu nini.
Sefu aliwahi kusema jini kishapanda kichwani,karibuni atataja jina,ni zaidi ya mwaka sasa hatujapewa jina la jini,sijui huyo jini bado yupo kichwani.Haya ndio mambo wanayopenda wazanzibari kuyasikia mpaka wakati mwingine wanaonekana sio watu makini
 
Nadhani katika awamu hii ni vizuri kuelewa kuwa maswala ya kupangiana cha kuandika na kusema hayapoooo!!! [HASHTAG]#WasipangiweChaKuandikaNaKuongea[/HASHTAG] waachwe wapige kazi, Mkulu kashasemaa.
 
Nafikiri msemaji wa upizani angeruhusiwa kusoma yote maana haina madhara bunge lenyewe halioneshwi kiasi kuhofia wananchi watajua killichoandikwa
 
Back
Top Bottom