Frank Wanjiru
JF-Expert Member
- Apr 12, 2012
- 21,841
- 38,736
Baada ya kikosi cha Simba Sc, kuruhusu kichapo cha mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya mtani wake Yanga Sc, Afisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza ameibuka na kusema kuwa ni rasmi kuwa watanzania na wanasoka watakuwa wameitambua Yanga B kwenye soka la ‘bongo’ ni timu gani.
Massanza amesema kuwa kumekuwa na kauli nyingi zinazosema kuwa Singida FG ni Yanga B kila wanapopoteza mchezo dhidi ya Yanga hivyo ameeleza kuwa kwa kuwa Simba nayo imepoteza mchezao kwa goli nyingi ambazo wao kama Singida hawajahi kufungwa na Yanga hivyo basi Simba ndiyo Yanga B.
“Sasa nadhani Yanga B mmeiona, sisi huwa tunasingiziwa tu, maana tukipoteza mchezo dhidi ya Yanga tunaitwa Yanga B, je hawa waliopoteza kwa idadi ya goli 5-1 tuwaite vipi?,” amesema Massanza.
Cc: Hussein Massanza