Massanza: Simba ni tawi la Yanga

Labani og

JF-Expert Member
Sep 15, 2020
15,783
24,215
SIMBA NI YANGA B

Baada ya kikosi cha Simba Sc, kuruhusu kichapo cha mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya mtani wake Yanga Sc, Afisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza ameibuka na kusema kuwa ni rasmi kuwa watanzania na wanasoka watakua wameitambua Yanga B kwenye soka la ‘bongo’ ni timu gani.

Massanza amesema kuwa kumekuwa na kauli nyingi zinazosema kuwa Singida FG ni Yanga B kila wanapopoteza mchezo dhidi ya Yanga hivyo ameeleza kuwa Simba nayo imepoteza mchezao kwa goli nyingi ambazo wao kama Singida hawajahi kufungwa na Yanga hivyo basi Simba ndiyo Yanga B.

“Sasa nadhani Yanga B mmeiona, sisi huwa tunasingiziwa tu, maana tukipoteza mchezo dhidi ya Yanga tunaitwa Yanga B, je hawa waliopoteza kwa idadi ya goli 5-1 tuwaite vipi?,” amesema Massanza.

Hamsa 5 G
 
Mkuu, michuano ile ilipangwa mapema. Laiti kama wangesubiri mpaka tulipocheza fainali CAFCC tungeenda sisi na tusingeishia pale.
Inawezekana pia walimchukua kolo....kama pazia la kumpitishia Al ahly
 
SIMBA NI YANGA B

Baada ya kikosi cha Simba Sc, kuruhusu kichapo cha mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya mtani wake Yanga Sc, Afisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza ameibuka...
Au hao Simba na wenyewe watuambie kama walipokea bahasha kutoka GSM, au la.
 
Back
Top Bottom