Msemaji wa CUF, Hamad Massoud akamatwa Zanzibar

Msemaji wa CUF, Hamad Massoud akamatwa Zanzibar

Duuh watamuachia tuuu siku zote kila usiku unapokuwa mkubwa zaid ndio mapambazuko ya asubih na kila maudhi vitisho vikizid ndio mafanikio yanakaribia
 
Natamani mijitu ya ccm yote ife kifo cha mdomo wazi

Mungu aliewakatalia kutawala Taifa hili ndie huyo unaemuomba? Allahu Jamiilu yuhibul jimaala (Mungu ni mwema na anapenda vitu vizuri) hapokei maombi ya kifedhuli.
 
Mi basi nnachoka kabisa kuona mzee anapiga selfie na totos huku wenzie wana shugulikiwa
 
Huyu ndiyo alikuwa anaratibu wale wanaotupa mabomu hovyo mitaani.



Mkuu kwanza wewe unapaswa Kuwa-arrested kuhojiwa Na Kuwa responsible before cour2 of law Kwa kushindwa kuzuia kosa.Upo contrarily agains2 Ka2ba ya Jamhuri ya Muungano wa 2anzania.Kinyume Na Sheria Ya makosa ya jinai "Failure 2 prevent felon"

Ulipomuona anara2ibu ulipuaji huo wewe ulichukuwa ha2ua gani? Huoni ndiyo umesababisha madhara Kwa wananchi Wasio Na ha2ia? Pengine ha2a vifo?

Kama makachero mmo humu muanze Na huyu Kwa nini muumize vichwa? Haya Afande Diwali Na Mzee we2 Wa invisible Kazi kwenu
 
s

Sijakuambia anasimamia urushaji wa mabomu ovyo... lakini kauli yake ya juzi akishindwa kuithibisha hilo peke yake ni kosa.
Ok,
maana post uliyoninukuu ilikuwa inahusiana na kurusha mabomu ovyo. Ipitie tena uicheki!
 
Huyu ndiyo alikuwa anaratibu wale wanaotupa mabomu hovyo mitaani.

Kila Mtu anajua nani anafanya uhalifu huo Zanzibar kuwa ni CCM kwa kuwatumia JKU , KMKM NA WAHUNI WENGINE WAITWAO MAZOMBIE.
kuna ushuhuda wa kutosha kuhusu jinai za watu hawa na ripoti nyingi zimepelekwa polisi mara kibao lakini kwa vile lengo lnajulikana hakuna hatua zina zochukuliwa.

mambo haya CCM hawakuanza leo walianza wakati wa Uchaguzi wa mwanzo walikua wakivunja na kutia mavi visima vya maji na kusingizia Raia wema ili kuwapiga tu basi .
Kuna wakati watu walifanya doria na kuwakamata wakiwa na zana zao kule pemba na tangu wakati huo yalisita .

na mara hii mara baada ya uchaguzi oct 2015 walianza tena kupiga vibomu vyao kwa nia ya kuwakamata cuf. lakini wakasahau kuwa Mji wa znz umewekwa camera na ushahidi wa nani amefanya hayo uko wazi ...hivyo wakashindwa kukamata watu kwani raia wema walisema camera zipo..ndio ikawa kimya.
sasa baada ya kuona huku mjini kuna kamera mazomie wamhamishia uharamia wao pemba na maeneo ya ngambo ya mji wa znz. huko hakuna camera.

hii ni false flag ni mbinu ya kizamani ya kishenzi na kijinga.
Jna hao mazombie wamevamia ofisi za cuf na kuvunja kila kitu ndani pamoja na kuiba..tena man in uniform wameiba viti na laptop na vifaa vingine.
wiki tatu ilopita waliunguza ofisi za cuf dimani na hakuna hatua ilo chukuliwa....

hivyo wazanzibari wana elewa na hao ccm wenye japo chembe ya uzalendo wanajua hayawanayo fanya madalali wa znz sio sawa na ni ujinga nchi kuiletea watu kutoka Tanganyika kuja znz na vifaa vya kijeshi, watu wasio jua hata mila na utamaduni wa kiznz.....bila ya shaka nguvu na mapenzi ya ccm itabaki wake wachumia tumbo kwani bila ya haya hawana cha kufanya chengine ..lakini waznz watazidi kuikataa ccm kila kukicha....
huwezi nchii hii ya waislam uwaletee watu wa dini nyengine kujazana na kutisha mitaani.... hakuna chembe ya muislam wa kweli ataridhia ujinga huu kwa mkono wa siasa...
 
1532153_10154729503199478_4625302698254944324_n.jpg
 
Mheshimiwa Hamad Masoud amekamatwa asubuhi hii na Polisi.

Hamad Masoud alikuwa Waziri wa Miundombinu na Mwakilisihi wa Chama cha Wananchi CUF Jimbo la Ole kisiwani Pemba, pia ni Kaimu Msemaji wa chama cha CUF.

View attachment 330066
haijapata kutokea pahala pengine popote katika ulimwengu huu wa Subhannah ambapo dhulma iliwahi kushinda haki .
 
Huyu ndiyo alikuwa anaratibu wale wanaotupa mabomu hovyo mitaani.
Mkuu kama umeshindwa kufikili kwa kutumia MASABULI, tumia hata pua, waznz ni tofauti sana na ninyi waswahili wa Danganyika, wale wanajitambua.
 
Daudi Mchambuzi: huwa natambua wewe ni mtetea utawala wa sheria ili haki itendeke! Wasikamatwe ili nchi isitawaliwe. Ikiwa hivyo wewe na mimi tutakwenda wapi?
si mmeweka vifaru pemba nzima kwa uwiano wa mtu 1 kifaru kimoja , sasa mnawakatia nini tena ilihali wamelengwa na makombora vichwani ?
 
Chagadema hapo tena wataongea sana maana mie nawajuwa awafanyi kitu mpaka serikali wafanye hata serikali wakifanya jambo jema kama hili watakosowa tu maana wameumbwa hivyo.
 
1.jpg

Ikiwa ni siku tatu tangu Mkurugenzi wa Habari Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa Chama cha Wananchi (CUF), Hamad Masoud Hamad, atangaze kuwa baadhi ya wananchi wa Zanzibar wanakimbilia porini kuhofia usalama wao, ametiwa mbaroni.

Kukamatwa kwa Masoud sasa kunafanya idadi ya viongozi wa chama hicho waliotiwa mbaroni na kuhojiwa polisi kufikia wanne tangu kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 28, mwaka jana.
Viongozi wengine waliohojiwa na Polisi na kuachiwa kwa dhamana ni Naibu Katibu Mkuu, Nassor Ahmed Mazrui, Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi, Omar Alin Shehe na mshauri wa mikakati wa chama hicho, Eddy Riyami.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja, Mkadam Khamis Mkadam, jana alithibitisha kukamatwa kwa Masoud, ambaye ni Waziri wa zamani wa Miundombinu na Mawasiliano katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Alisema kiongozi huyo alikamatwa na kitengo cha upelelezi nyumbani kwake mtaa wa Mbweni mjini Zanzibar jana.
Alisema kwa sasa anashikiliwa katika Kituo cha Polisi cha Mwembe Madema ili kusadia uchunguzi juu ya taarifa alizotoa katika mkutano wake na waandishi wa habari na kuzungumzia hali ya amani ya Zanzibar na wananchi wake.

“Tunamshikilia kwa uchunguzi, kuna mambo ya msingi tunaona yanahitaji kufanyiwa uchunguzi na yeye kusadia polisi uchunguzi wake,” alisema Mkadam.

Kufuatia kukamatwa huko kwa Masoud, CUF imelaani kitendo hicho na kusema kuwa kamata kamata hiyo inawalenga viongozi wa chama hicho na wanachama wake pekee.

Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Mazrui alisema matukio yote ya uvunjifu wa amani yaliyotokea visiwani hapa, yamekuwa yakihusishwa na CUF na Jeshi la Polisi huwakamata viongozi wa chama hicho pekee.

“Tunasema huu ni uonevu wa hali ya juu, maana viongozi na wafuasi wa CUF pekee ndio wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi, hii yote inatokana na uchaguzi wa marudio, hivyo kutoshiriki kwetu kwa uchaguzi isiwe sababu ya kuadhibiwa,” alisema.

Aidha, alisema suala la kushiriki au kutoshiriki katika uchaguzi ni hiari ya mtu, hivyo kwa wale ambao hawatashiriki uchaguzi huo, wasiadhibiwe wala wasidhalilishwe na wale ambao wametangaza kushiriki waende wakapige kura.

Kwa upande wa mke wa Masoud, Rahma Issa, alisema askari kazu wasiopungua sita wakiwa na silaha za moto mbili walifika nyumbani jana saa moja asubuhi na kudai wanamhitaji mumewe.
Alisema baada ya kubisha hodi, kijana wake mmoja alifungua mlango na kisha askari watatu waliingia ndani mmoja akiwa na silaha ya moto kifuani.

“Baada ya kuamshwa na kutoka chumbani walimwambia yupo chini ya ulinzi anahitajika kituo cha polisi,” alisema Rahma.

Hata hivyo, alisema baada ya kumkamata, hawakumwambia sababu ya kukamatwa kwake, lakini baada ya kuwauliza wanampekeka kituo gani walimwabia Kituo cha Polisi Mwembe Madema, Zanzibar.

Naye Mkurugenzi wa Mipango na Uchaguzi wa CUF, Omar Ali Shehe, alisema vitendo vya kukamatwa viongozi wa CUF ni mwendeleo wa Serikali ya CCM kuwanyanyasa viongozi na wanachama wake chama hivyo visiwani hapa.

Alisema vitendo vnavyoendelea kufanywa na Jeshi la Polisi vinakwenda kinyume cha misingi ya demokrasia na haki za binadamu.

Shehe alisema matunda ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya kujenga amani na umoja wa kitaifa yameanza kuvurugwa tangu kuingia mgogoro wa uchaguzi mkuu.
Chanzo: Mpekuzi
 
Haya mambo wanayofanya CCM kwa wananchi wa Zanzibar, ipo siku watayajutia. Huu ni uonevu uliopitiliza.
 
Back
Top Bottom